Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

ubarikiwe kwa somo zuri ulilolitia bila gharama.

nisaidie mimi wa bara, nimepata kizungu zungu kwa malighafi tajwa namba 2&3
2)kitunguu thomu
3)habati sauda.

bado naona chenga chenga
Hahahahhhhah!
Usijali,huku bara tumezoea kuviita vitunguu swaumu.
Na habat sauda unaweza kuipata kwenye maduka ya wauza dawa za kisuna,maduka ya waarabu,wahindi nk.
 

VIDONDA VYA TUMBO-CHANZO NA TIBA YAKE

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao unatokana na pale utando unaofunika kuta za tumbo na kuzikinga dhidi ya madhara ya tindikali zilizo tumboni unapoharibiwa ama kuchubuliwa. Kwa kawaida tabaka la juu la utumbo hulindwa na ukingo maalum (gastric mucosal barrier) kwa kutengeneza ute (mucous) na alkali za madini ya baikaboneti (bicarbonate ions) dhidi ya tindikali na kimeng’enya (enzyme) cha pepsini. Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) hutokana na hitilafu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Tindikali za tumboni (kwa mfano hydrochloric acid) husaidia kwa karibu kumeng'enya chakula. Madhara ya kuharibiwa kwa utando huu dio hupelekea ktokea kwa vidonda vya tumbo.
Mgawanyiko na utengenezwaji wa seli mpya za tabaka la juu la utumbo pamoja na uwepo wa damu ya kutosha ni baadhi ya vigezo vingine vinavyosaidia kulinda tabaka hili na utumbo dhidi ya kumomonyoka au kutoboka.
Kuwepo kwa kigezo chochote kitakachoingiliana na ulinzi dhidi ya tabaka la juu la utumbo hupelekea kumomonyoka kwa tabaka hilo na kusababisha kidonda au vidonda vya tumbo ambavyo huweza kupelekea hata kutoboka kwa utumbo iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa
Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.
Kuna makundi makuu matatu ya ugonjwa huu-
A. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani ndani ya kuta za tumbo (Gastric ulcers).
B. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers).
C. Vidonda vinavyotokea kwenye koo au umio (Oesophageal ulcers)
AINA YA VIDONDA VYA TUMBO;
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo;
1. gastric ulcers, Hii ni Aina ya kwanza ni ile inayoathiri tumbo
2. peptic ulcers, Aina ya pili ni ile inayoathiri utumbo mwembamba wa duodenam(duodenum).
Hapo zamani ilikuwepo dhana kwamba msongo wa mawazo (stress) na mlo (diet) husababisha vidonda vya tumbo.Baadaye watafiti wa masuala ya afya ya binadamu waligundua kuwa tindikali izalishwayo tumboni na vimeng’enya vya pepsini inachangia kiwango kikubwa katika kusababisha vidonda vya tumbo.

Asilimia kubwa ya waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo ni watu wenye umri zaidi ya miaka arobaini (40) na wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake.Waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo huwa wembamba kutokana na kutokula wakihofia kupata maumivu pindi walapo chochote. Dalili kubwa ya wagonjwa hawa ni;-
Maumivu ya tumbo (chembe). Maumivu yake huwa yenye majira maalum ambapo huanza punde tu mgonjwa alapo chakula na hupungua baada ya chakula kuisha tumboni au kwa kunywa kimiminika chenye alkali.
Hamu ya kula huwa nzuri lakini baadhi yao waweza kutapika.Kutapika damu (haematemesis) na kupata choo chenye damu (malaena) huweza kuambatana na aina hii ya vidonda vya tumbo.
Uzito wa mwili hupungua kwa kiasi fulani kutokana na kutokula vizuri.
Kusambaa kwa maumivu mpaka mgongoni kwaweza kutokea iwapo kidonda kimetoboka na kuhusisha kongosho (pancreas).
b) VIDONDA VYA UTUMBO MDOGO (DUODENAL ULCERS) NA DALILI ZAKE
Aina hii ya pili kwa upande mwingine huathiri watu wenye umri chini ya miaka arobaini (40) na kama aina ya kwanza,waathirika wengi ni wanaume.
Maumivu yana tofauti na aina ya kwanza, hutokea kati ya masaa mawili na nusu hadi manne bada yamlo ambapo chakula huwa kimeisha tumboni (hunger pains)
Maumivu pia hutokea zaidi mapema asubuhi au nyakati za jioni.Nafuu hupatikana kwa kula chakula.
Kutapika hutokea kwa nadra sana kwa wagonjwa wa aina hii. Kutapika damu na kupata choo chenye damu hutokea mara nyingi zaidi kuliko aina ya kwanza.
Hamu ya kula kwa wagonjwa wa aina hii huwa nzuri na hupenda kula mara kwa mara hivyo huwa na miili yenye afya nzuri tofauti na wagonjwa wa aina ya kwanza.
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Bacteria wanaoitwa Helicobacter Pylori (H.pylori)

Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya duodenal ulcers.
Jinsi H.pylori anavyosababisha vidonda vya tumbo
Vimelea vya H.pylori huweza kusambaa kupitia chakula na maji.Vimelea vya bakteria hawa pia hupatikana kwenye mate hivyo vyaweza kuambukizwa kupitia kinywa haswa iwapo mtu atabusiana na muathirika wa vimelea hivyo.Watu wengi pia huathirika na vimelea hivi utotoni.
Vimelea vya H.pylori huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana. Hapo hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho ambayo hupunguza makali ya tindikali izalishwayo na tumbo yaani gastric juice/acid.Ili kukabiliana na hali hii,tumbo hutengeneza tindikali nyingi zaidi ambayo huathiri tabaka la juu la utumbo.Vimelea hivi pia hudhoofisha ute ulindao tabaka la juu la utumbo hivyo kushindwa kulinda tumbo na utumbo mwembamba sawasawa.Bacteria wa H.pylori husababisha takribani 80% ya vidonda vya tumbo (gastric ulcers) na 95% ya vidonda ndani ya duodenum(duodenal ulcers). Aidha,vimelea vya H.pylori hujiegesha kwenye seli za tumbo.Hali hii hudhoofisha mfumo wa ulinzi wa tumbo na kusababisha maumivu na hatimaye madhara katika eneo lililoathirika.
Kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.
Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia huharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
2. Non-steroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs)
Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa mfano za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo. Vidonge kama vile hivi ni kama asprin,naproxen,diclofenac, na ibprofen.Dawa hizi hudhoofisha kuta zenye utando (mucus) za tumbo na kufanya iwe rahisi kutobolewa na tindikali.
3. Uvutaji wa sigara:
Uvutaji sigara huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo kwa kiasi fulan,maana sumu ya nikotini na cafein iliyomo ndani ya sigara huamsha uzalishwaji wa tindikali ya gastric kwa wingi na kusababisha kiwango cha tindikali kuwepo kwa wingi tumboni hali ambayo husababisha ukuta wa utumbo kubabuka/kuchubuka.
4. Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu:
Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo..
5. Unywaji wa pombe:
Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
6. Msongo wa Mawazo
Msongo wa mawazo hausababishi vidonda vya tumbo badala yake huongeza maumivu kwenye kidonda kilichopo.Hufanya hivyo kwa kuongeza zaidi utengenezwaji wa tindikali tumboni.
7. Kafeini (Caffeine)
Kafeini ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vinywaji kama soda, kahawa n.k huchangamsha utengenezaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua ukuta wa utumbo na pia hutonesha kidonda kilichopo kama mtu ni mwathirika tayari.
TIBA YA CRYSTALL CELL KUPONYA VIDONDA VYA TUMBO
Crystal CELL
hufanya kazi ya kukarabati, kuboresha na kuchochea uzalishwaji na utengenezwaji wa seli mpya za tabaka la juu la utumbo pamoja na husaidia kulinda tabaka hili na utumbo dhidi ya kumomonyoka au kutoboka.
Crystal CelL huimarishana kurutubisha kinga ya seli na kuta za utumbo dhidi ya vimelea vya H.pylori ambavyo huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana. Huondoa utengeneza wa kimeng’enya kiitwacho urease ambacho ambayo hupunguza makali ya tindikali izalishwayo na tumbo yaani gastric juice/acid.
Crystal cell huboresha kazi ya gastrin ambacho ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo,Crystal cell itaboresha mfumo wa gastrin ilikubalance na kuepuka uzalishaji wa gastric acid kwa wingi ambayo hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
Snowphyll huflush sumu zinazotokana na madawa, kaffine na nikotin kutoka kwenye sigara. Pia hutoa harufu mbaya ya mdomo huboresha mfumo wa damu mwilini. husaidia kuondosha matatizo ya upatikaniji wa choo(constipation). Antioxidants help fight chronic inflammation, which occurs when the immune system reacts to particular health issues, such as arthritis, stomach problems, skin issues.

KWA MAWASILIANO JUU YA UPATIKANAJI NA MAELEZO ZAIDI JUU YA HIZI PRODUCTS
0682315816
 
Pole mkuu kuna mtu ana dawa ipo kama spirit yupo mwanza so kuna staff mwenzangu alikuwa kama wewe alikunywa akapona, ila meanwhile jaribu unga wa komamamanga
 
Agha khan dar au vipimo viligharimu bei gani
 
Habarini madaktari!

Naombeni mnisaidiekutatua hii changamoto, Mimi ni mtumiaji mzuri wa maziwa fresh kuanzia mtoto hadi Leo, ila miaka kama 10 iliyopita nilithibitika kuwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na nilitibiwa kisasa( hospital) ila mpaka sasa bado havijaisha,
Majuzi niliambiwa maziwa fresh sio mazuri kwa vidonda vya tumbo, nijaribu ya mgando, kweli nilijaribu ila ninapata maumivu makali ( yalianza taratibu ila yame ongezeka sana) sasa naombeni mnisaidie je ni mazuri kwa afya ya vidonda vya tumbo? Je niendelee nayo au niache?

Sky Eclat @georgeousmimi Mzizi mkavu na madaktari wote!
 
Habari!

Pole kwa tatizo la vidonda vya tumbo.

Maziwa mgando pia sio mazuri kwako Kwani MAZIWA MGANDO YANATAKIWA YACHACHUSHWE (YAHARIBIKE KIDOGO). hivyo kuna bakteria (hata kama ni kwa kiwango kidogo).. Hivyo KAA NAYO MBALI KWA SASA.

afyakliniki inakushauri utafute matibabu kwanza.

Wasiliana nasi kwa PM au njoo Instagram ukurasa wa @afyakloniki kwa msaada zaidi.

Asante na Karibu.
 
Mmmh hawa Madr sasa,mi ninavyo pia ila maziwa fresh ni moja ya tiba na nayatumia muda mrefu,ila sasa sina shida tena kwa miaka kadhaa kwa dawa niliyotumia metronidazole(fragile) na Amoxicillin.....tangu 2013 havijarejea tena
 
Mmmh hawa Madr sasa,mi ninavyo pia ila maziwa fresh ni moja ya tiba na nayatumia muda mrefu,ila sasa sina shida tena kwa miaka kadhaa kwa dawa niliyotumia metronidazole(fragile) na Amoxicillin.....tangu 2013 havijarejea tena
duh hivo vidonge si ndio vinachimba utumbo kabisa
 
Bicarbonate soda ile ya maandazi ni dawa nzuri ya vidonda vya tumbo Mimi ilinisaidia na Niko vizuri kwa sasa. ....unaeka kijiko kimoja cha chai kwenye maji glass moja unakologa unakunywa asubuh kingine jioni kabla hujala chochote ikipita nusu SAA unakula chakula
 
ndo zile chapamandash mnaita?
 
Mmmh hawa Madr sasa,mi ninavyo pia ila maziwa fresh ni moja ya tiba na nayatumia muda mrefu,ila sasa sina shida tena kwa miaka kadhaa kwa dawa niliyotumia metronidazole(fragile) na Amoxicillin.....tangu 2013 havijarejea tena
Dawa ulizotaja ni 1st Line Drugs for PUD Treatment.

Lakini inabidi kwanza kubini chanzo cha tatizo (sio vidonda vyote vya tumbo ni sababu ya H.Pylori).

Chanzo cha tatizo kikijulikana matibabu stahiki hutumika

Asante na Karibu afyakliniki
 
Dawa ulizotaja ni 1st Line Drugs for PUD Treatment.

Lakini inabidi kwanza kubini chanzo cha tatizo (sio vidonda vyote vya tumbo ni sababu ya H.Pylori).

Chanzo cha tatizo kikijulikana matibabu stahiki hutumika

Asante na Karibu afyakliniki
Japo saiz sisumbuliwi but vp mnapatikana wapi cos nina jamaa yangu ni leo tu alikuwa hospital kwasababu hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…