Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ahsante kwa kushukuru chief.
Lakini pia nakushauri uchukuwe tahadhari sana kwa hasa wale watakao jifanya msaada wako, na kisha kuku tumia kwa kupata fedha kwakuwa tu wanakuona unashida na unahitaji msaada.
Nakushauri jipe tahadhari sana na neno hili "njoo PM
 
Yes kama nikila embe,nanasi, (citrus zote)soda,majuis ya dukani,vitu vya baridi,viazi,nyama yaani kifupi sina chema tumbo linanivuruga wakati wote.Nikila kidogo tumbo linajaa gesi.Nimekua mkali kama pilipili.kila saa mahasira.Na mind vitu vya kijinga hadi wakati mwingine najishangaa
Hivyo ni vidonda vya tumbo bila shaka
 
Epuka kula vyakula ambavyo vinapelekea gesi tumboni. Achana na mawazo maana nayo huwa yanapelekea kuzidi kwa maumivu. pole utapona.
 
Ambition plus,
Pia kapendekeza matumizi ya tangawizi, kitunguu swaumu, mtindi, apple vinega, green tea, kabichi, embe tamu (nyuzi nyuzi ni muhimu) asali. Lakini nikigusa asali tumbo linavurugika vibaya sana,

Hapo sikushauri mkuu, hivyo vitu alivyokushauri huyo mpendwa sio rafiki kabisa kwa hali yako.Tumia dawa inaitwa Altapham Syrup chupa moja kwanza halafu ulete mrejesho,tumia mpaka umalize chupa kutokana na maelezkezo ya mfamasia au Daktari, kisha nitakushari zaidi nini cha kufanya.
 
Kwa experience ya mtu wangu wa karibu sana ambaye vyake vilikuwa chronic.

Niliwahi kumletea mkunazi umechanganywa na shubiri niliyoinunua safarini na akawa vizuri kiasi..

Tiba ambayo anaiamini ni majani ya mstafeli. Huwa anayachuma na kuyatwanga na ubichi wake. Anamix maji kiasi halafu anakunywa kama juice

According to yeye hiyo ndio huwa inamsaidia vikicharuka maana bado hataki kufuata restrictions za vyakula.
 
Nitakutafuta jioni kuna jamaa amekuwa akisumbuka na maumivu ya tumbo akipima anaambiwa ni vidonda vya tumbo amekuwa akijua ni vidonda vya tumbo kwa takribani miaka kadhaa ila akaja kupata ukweli baada ya vipimo vingine , akirudi jioni nitamuuliza alafu anipe maelekezo vizuri
 
Ushimen, Well said. Unajua nimegundua hili tatizo ni la wengi. Hakika kama kuna mwenye dawa ni vema tukazungumza hapa hapa. Na baada ya matumizi nitakuja na mrejesho pia itakua msaada kwa wengine. Asante.
 
Mie pia nina shida kama hii tangu 2011, nimefanya vipimo vingi na kuna kipindi nilijiaminisha nina cancer ya utumbo , ya kwanza wakasema ni diverculitis ya pili wakaniambia hpylori, ya 3 haikuonyesha chochote.

Dr alinishauri niache vyakula vingi tuu ambavyo ni common kwa sisi Waafrika, especially vyakula vya kukaanga na vyenye asili ya mafuta, spices, jamii ya karanga na vitu vyenye caffeine. Pia kula kwa wingi mboga mboga ambazo hazijapikwa pamoja na maji ya kutosha, bila kusahau kupinguza uzito.

Nimejitahidi kufuata huo ushauri wa Dr na baada ya kama miezi 8 naona maumivu yamepungua sana tuu, sijapona ila naweza kwenda hata wiki nzima bila sijahisi maumivu.
Well said.Unajua nimegundua hili tatizo ni la wengi.Hakika kama kuna mwenye dawa ni vema tukazungumza hapa hapa.Na baada ya matumizi nitakuja na mrejesho pia itakua msaada kwa wengine.Asante
 
Jaribu tiba za kisuni, hasa hasa jaribu kufuatilia kuhusu Black Seed oil mafuta ya Habat souda. Ni nzuri sana wanasema inatibu magonjwa yote isipokuwa kifo ukizingatia dozi.
 
Jaribu tiba za kisuni, hasa hasa jaribu kufuatilia kuhusu Black Seed oil mafuta ya Habat souda. Ni nzuri sana wanasema inatibu magonjwa yote isipokuwa kifo ukizingatia dozi.
Black seed nimetumia mkuu haikunipa matokeo yeyote
 
Pole sana nilikuwa naumwa ulcers 2012 sana nilienda kwa wakorea pale ubungo garage nikafanyiwa tiba mpk leo sijawah kuumwa tena , jaribu tiba mbadala .
 
Back
Top Bottom