Wakuu JF,
Mimi niko nje ya DAR na nimesikia kuna Mtu anaitwa DR. RAHABU amegundua dawa ya kuponya vidonda vya tumbo, ULCERS .
Je wakuu, habari hizi zina ukweli wowote wa kitaalamu?
Eti dawa hiyo inatolewa kwa mazingira ya kutatanisha kama si ya kitaalamu?
Naomba kujuzwa.
hiyo ya Dr. Rahabu hata mimi huwa naona kwenye Tv na watu walioitumia wakitoa ushuhuda wao kuwa wamepona tena yeye dawa zake anasema zimethibitiswa na wizara ya afya. hivyo zina viwango na hazina madhara.
ili uende kwake na akupe hizo dawa lazima uwe na cheti cha daktari kinachoonyesha kuwa kweli unavidonda. hivyo kwa nionavyo mimi sio tapeli kama wengine wanavyoita. kama ni kweli amegundua hiyo dawa na imethibitishwa na watu wanapona tunampongeza. ni hatua moja mbele kwa taifa letu. maana hata hizo dawa mseto na quinini za malaria na yinginezo nyingi zinazotumika mahospitalini zinagunduliwa na binadamu kama sisi, au kwa kuwa ni watu weupe ndio tunaziona za maana sana wakati zimejaa 'side effect' kibao? ila akigundua mtanzania au mtu mweusi ataitwa tapeli, mganga njaa, na majina mengimengimengineyo. Loh!
kwa stail hiyo hatuachaa kutemewa mate. kwa sababu vilivyo bora kwetu hatuvioni.
ukiumwa kichwa kidogo hospitali, mtu mweusi akikwambia kichwa kikikuuma kunywa maji mengi ni dawa ila maumivu yakizidi ndio umuone daktari pengine kitakuwa kuna kitu kingine kinakusumbua utamwambia ni tapeli. Bora ukanunue panadol unywe hahaaa. ndio yale yale.
Mimi nionavyo mtu anayetumia ramli, au dawa za mashariti sijui ukinywa chungulia ******, au ukipaka kakae kwenye kaburi, ukioga chini ya mbuyu n.k hao ndio matapeli. lakini mtu anayekwambia chukua asali na limao unywe kutwa mara tatu, punguza kula vyakula vya aina ya mpira vinasababisha kufunga choo, au majani ya chai yana caffein punguza au acha, au pendelea sana kuwa vitunguu swaumu vina kinga nyingi za magonjwa utapeli wake ukowapi? limao hakununuli, unanunua mwenyewe, asali unanunua mwenyewe na ukiangaliwa vitu vyote hivyo vinafaida katika mwili wa binadamu ila kwa kuwa ulikuwa hujui na mtu anayejuwa kuwa vitu hivyo ni dawa na ametokea akasema ili wale wenzangu na mimi tusiojua tujue tusishindie kula chips, kuku, mayai, bia, nyama choma kila siku kwa kuwa tu tunaweza kuvipata kila siku basi ooh tapeli, mganga njaa n.k.
Ndio maana vitambi, presha,kisukari, shapeless(hujui kiuno kiko wapi, tumbo liko wapi na mgongo uko wapi), n.k havituishi lakini vyote ni chanzo cha malaji mabaya. ni watu wangapi hivi sasa wanasumbuliwa na constipation, na hayo magojwa mengine na hosipitali ni ngapi zipo kila kona hata za madaktari feki? kwa nini wagonjwa hawaishi hospitalini? Watoto wangapi ukiwaangalia leo hii ni vinene, vinene, tu kwa ajili ya chips na mayai lakini akili kichwani hakuna wanasubiri kuiba mitihani. lakini mabibi, mababu zetu na wazazi wetu wa miaka hiyo walikuwa strong kwa ajili ya natural food na akili za shule walikuwanazo waliosoma walioma hasa hawakusubiri kununua paper, ilikuwa mtu akifaulu mpaka anapelekwa shule za wenye vipaji kweli anastahili. sio vyakula vya sasa vingi vya viwandani ambavyo vina expire date,chips, chocolate, nyama choma na nyama zenyewe zilizonenepeshwa na vikorombwezo viingi lakini mwisho wake hata akili kichwani zinapungua, magonjwa ya kila aina kila siku yanazuka mapya. tumefika kwenye point of no return ya kuchanganyikiwa hivyo akitokea mwema akiwaambia vitu asilia ni dawa atakoma hayo majina atakayoitwa mpaka atashiba.