Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Nimekuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo msaada tafadhari nisaidieni kwako mzizimkali nimefuata kanunu za dawa bado sija changanya kwa navyo asali+adapt soda nisaidie jamani naumwa nichanganye vip
MARADHI YA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS): Haya ni maradhi ambayo hufanya vidonda upande wa ndani ya ukuta wa tumbo. Kuna Duodenal ulcer na Gastric ulcer. DALILI: (1) Kupata maumivu makali chini ya kifua kwaupande wa ndani. (2) Kuchoka bila sababu. (3) Kuumwa kwa mgongo au kiuno. (4) Kupungua kwa nguvu za kiume. (5) Kuwa na

kichefuchefu baadhi ya wakati. (6) Kuwa na kiungulia . (7) Tumbo kujaa gesi. (8) Tumbo kuwaka moto. (9) Kukosa choo na wakati mwingine kupata choo kigumu kama cha mbuzi. (10) Kukosa hamu ya kula. (11) Kutapika damu au wakati mwingine

kutapika nyongo. (12) Maumivu makali baada ya kula vitu vikali au chakula cha moto.

TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua asali robo lita uchanganye na unga wa arki susi vijiko vinne vikubwa kisha ukoroge kwa mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya pili: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili.

Kanuni ya tatu: Chukua lozi gramu 30 halafu usage iwe unga. Changanya lozi hii yote ndani ya kikombe kidogo cha maziwa ya moto kisha uongeze asali vijiko viwili vikubwa. Kunywa kikombe kimoja robo saa kabla ya kula chakula cha asubuhi. Fanya hivyo kwa muda wa mwezi na utapata shifaa.

Chaguwa Moja kati ya hizi dawa itakayo kuwa ni kwako rahisi kuitumia na kuipata Uguwa pole. Usikose kunipa feedback.
 
Ninatatizo la vindonda vya tumbo takriban miaka 6 sasa,awali nilikuwa nikitumia dawa za hospital zilikuwa zinanisaidia,ila kwasasa hazinisaidii,tafadhal kwa yeyote aliyetumia dawa ya NETRAGEN naomba anielekeze inapatikana wap mana nasikiwa imewasaidia sana watu,au kama unaushauri wowote au dawa yoyote unayoifaham naomba pia msaada wako.
Nawasilisha,asante.
 
Pole. Changanya mdarasini na asali, kunywa utapona. Hicho ndicho nilichotumia mimi na kupona.
 
Mzizi mkavu mteja wako huyo,, pata ajra bure,, allah akuzidishie duniani na akhera unasaidia wengi
 
Hi wana jf naomba kujua dawa ya vidonda vya tumbo vinanisumbua sana sasa ni mwaka mmoja
 

MZIZI leo umeteleza ameuliza dawa hiyo aliyotaja na akaongeza .....au ashauri na dawa ingine inayoweza msaidia ,please kamanda hebu mpe link ajimwage!
Mkuu KYALOSANGI kutokana na jinsi huyu

Mkuu Tumaah Amesha taja dawa (NETRAGEN) ambayo ana imani akiipata itaweza kumsaidia hivyo vidonda vyake

vya tumbo kuna umuhimu gani tena wa kumwambia dawa ya Vidonda vya tumbo? Tunawasaidia watu wenye kuja hapa

kueleza shida zao kama wamesha kwenda Hospitali kujitibia na hawakupata nafuu yoyote ile ndio tunaweza kuwasaidia

ila mtu anataja Dawa ambayo anahisi akiipata itamsaidia kumtibu maradhi yake ya vidonda vya tumbo hakuna haja ya

kumwambia dawa ingine tena.
 
Last edited by a moderator:
mkuu. Mzizi mkavu tupo wengi wenye hayo maradhi kwa gaida ya wengine tusaidie mkuu
 
Last edited by a moderator:

Huu ugonjwa unanimaliza, nashukuru wataalamu wanatuelimisha hapa jukwaani.
Ninatumia dose ya Omeprazole na pia Hyoscine bado sijaona mafanikio.
 
Msaada tafadhali, hizi dawa zinazotangazwa kwenye TV na hasa siku za hivi karibuni za kampuni ya "HERBOWORX" na zile za "DR. RAHABU" kama kuna mtu amewahi kutumia na zikamsaidia naomba anijulishe, akiweka na bei zake itakuwa poa sana.
 
Vidonda vya tumbo husababishwa na bacteria aina ya'Helicobacter pylori'& Non steroidal ant inflammatory drugs.

Pia watu wanaotumia sigara na vileo wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

Helicobacter pylori huishi kwenye kuta za tumbo na kutengeneza vimeng'enya "enzyme"iitwayo urease inayopunguza athari za asidi kwenye tumbo.

NSAIDS-hizi ni dawa zinazotumika kwa ajili ya kutuliza maumivu mfano aspillin,dicrofenac,pcm,ibuprofen n.k,dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo husababisha vidonda,dalili za ugonjwa huu ni(1)maumivu makali ya tumbo(2)maumivu makari sana unapokuwa na njaa(3)kukoswa hamu ya kula(4)kujisikia kichefu chef(5)kupungua uzito(6)kupata choo cheusi/kilicho changanyikana na damu(7)kutapika damu n.k.kama ni H.pylori ndo aliyesababisha antibiotics hutumika,kama ni NSAIDS tumia dawa hizi zitakusaidia Omeprazole,Esomeprazole&Lansoprazole.Nina dawa inayotibu tatizo hilo kwa siku 14 tu unakuwa safikabisa.

Kama unahitaji ntafte 0759217720.
 

DAWA YA KIENYEJI AU AINA gANI?
 
ni ya mizizi au maana Esomeprazole zinatuliza tuu, funguka tukuelewe vizuri
 
Ni dawa ya mitishamba,ni dawa nzurisana inatibu kwa mda wa siku14tu.Kama unatatzo hilo eb jarib kunitafuta utaona manufaaa.
 
Habari zenu wana JF. Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo toka mwaka jana.

Nilipoenda hospital wakasema vipo katika utumbo.

Kuna dawa nilizigharamia kwa sababu niliambiwa nitapona.

Nilipokunywa hizo dawa vikatulia kwa miezi 3 sasa vimeanza tena.

Msaada wako wako muhimu nitumie dawa gani vipone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…