Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MARADHI YA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS): Haya ni maradhi ambayo hufanya vidonda upande wa ndani ya ukuta wa tumbo. Kuna Duodenal ulcer na Gastric ulcer. DALILI: (1) Kupata maumivu makali chini ya kifua kwaupande wa ndani. (2) Kuchoka bila sababu. (3) Kuumwa kwa mgongo au kiuno. (4) Kupungua kwa nguvu za kiume. (5) Kuwa naNimekuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo msaada tafadhari nisaidieni kwako mzizimkali nimefuata kanunu za dawa bado sija changanya kwa navyo asali+adapt soda nisaidie jamani naumwa nichanganye vip
kichefuchefu baadhi ya wakati. (6) Kuwa na kiungulia . (7) Tumbo kujaa gesi. (8) Tumbo kuwaka moto. (9) Kukosa choo na wakati mwingine kupata choo kigumu kama cha mbuzi. (10) Kukosa hamu ya kula. (11) Kutapika damu au wakati mwingine
kutapika nyongo. (12) Maumivu makali baada ya kula vitu vikali au chakula cha moto.
TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua asali robo lita uchanganye na unga wa arki susi vijiko vinne vikubwa kisha ukoroge kwa mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili.
Kanuni ya tatu: Chukua lozi gramu 30 halafu usage iwe unga. Changanya lozi hii yote ndani ya kikombe kidogo cha maziwa ya moto kisha uongeze asali vijiko viwili vikubwa. Kunywa kikombe kimoja robo saa kabla ya kula chakula cha asubuhi. Fanya hivyo kwa muda wa mwezi na utapata shifaa.
Chaguwa Moja kati ya hizi dawa itakayo kuwa ni kwako rahisi kuitumia na kuipata Uguwa pole. Usikose kunipa feedback.