Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Jamani wana JF kwa wale ambao mmeshasikia au mmeenda kwa babu Loliondo,je babu anatibu vidonda vya tumbo?? Nna tatizo hilo.. Pa1 wakuu
 
mtafute rahabu anatibu
.watu wanaenda kimyakimya na kurudi kimya.
Nasikia siku hizi ana simu, mpigie muulize.au nenda kanywe dawa, ukipona unajua anatibu usipopona unajua hatibu.
 
Mtafute Rahabu anatibu

Unapokunywa dawa ya rahabu lazima uchukue tahadhari ya kutokaa mbali na choo. Ni kujisaidia mtindo mmoja tena mzigo wenyewe mkubwa sana na harufu yake hata inzi hawaipendi. Hali hiyo itakupata kipindi chote cha dozi kinachoanzia miezi miwili na kuendelea. Mimi nilijaribu niliishia njiani kutokana na aina ya kazi ninayofanya.
 
anaponyesha ndugu kwani dada yangu alikunywa na sasa anapiga maharage kwa sana sasa.
 
Ufahamu Ugonjwa wa Vidonda Vya Tumbo (Peptic Ulcer Disease Imeandikwa Na Dr Khamis
I

Stomach-Ulcers-300x234.jpg
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu.
Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.
Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kamaHelicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenachuweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kamaduodenum.
Makundi ya PUD
Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu
1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (Gastric ulcers)
2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers)
3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo (Oesophageal ulcers)
4. Vidonda vijulikanavyo kama Merckel's Diverticulum ulcers.

Source:Tumbo
 
Ingefaa zaidi ungeongezea kuhusu visababishi vya ugonjwa huo ili tujue namna ya kujilinda
 
Tujulishe namna ya kutibu au kuzuia hivi vidondo vya tumbo, au huduma inapatikana katika clinic yako, tujuze iko wapi mkuu.
 
Tujulishe namna ya kutibu au kuzuia hivi vidondo vya tumbo, au huduma inapatikana katika clinic yako, tujuze iko wapi mkuu.
Dawa ya Vidonda vya tumbo, Kinga (Urine) wako Mwenyewe kipimo cha glasi moja uwe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja kisha nenda kapime hivyo Vidonda vyako vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yak0 yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii mtu hiyo dawa imewasaidia wengi.
 
Asante ndugu, ila ingenoga zaidi kama ungeandika na visababishi na jinsi ya kuepuka ugonjwa huu kama inawezekana. Thanks
 
Hivi kuna tatizo huwa tunaliita 'kiungulia'......lina uhusiano wowote na 'vidonda vya tumbo'? (ni vitu tofauti au ni kitu kimoja?)
 
Dawa ya Vidonda vya tumbo, Kinga (Urine) wako Mwenyewe kipimo cha glasi moja uwe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja kisha nenda kapime hivyo Vidonda vyako vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yak0 yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii mtu hiyo dawa imewasaidia wengi.
Ni nini hasa kipo kwenye mkojo kinachoponya vidonda vya tumbo?
 
Dawa ya Vidonda vya tumbo, Kinga (Urine) wako Mwenyewe kipimo cha glasi moja uwe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja kisha nenda kapime hivyo Vidonda vyako vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yak0 yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii mtu hiyo dawa imewasaidia wengi.
Jamani hivi ni kweli au unataka kutuchekesha tu?
 
Tujulishe namna ya kutibu au kuzuia hivi vidondo vya tumbo, au huduma inapatikana katika clinic yako, tujuze iko wapi mkuu.
hahaha clinic yake iko loliondo huoni picha. (jokes)
 
Back
Top Bottom