Ufahamu Ugonjwa wa Vidonda Vya Tumbo (Peptic Ulcer Disease Imeandikwa Na
Dr Khamis
I
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu.
Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.
Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama
Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya
Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama
Aspirin au
Diclofenachuweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (
stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama
duodenum.
Makundi ya PUD
Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu
1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo
(Gastric ulcers)
2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo
(Duodenal Ulcers)
3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo
(Oesophageal ulcers)
4. Vidonda vijulikanavyo kama
Merckel's Diverticulum ulcers.
Source:Tumbo