Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Vidonda vya tumbo vina dawa nyingi mno, ni suala la muda tu.
 
Ni mwezi sasa tangu nimekutwa na huyo H. Pylori! Nashukuru naendelea na Dawa alizoniandikia Dr
 
Nashukulu kwa somo ila nna daut kwenye soya product mim huwa nawashauli wagonjwa wangu watumie soya apo vp au nawapoteza
 
Asante kwa somo zuri nakumbuka vilinisumbua sana kama miezi miwili ila hiyo kabeji mchanganyiko na karoti dawa tosha nilipiga juisi yake ndani ya wiki na nusu mambo shwari kabisa
 

Nyie ndo mnaotuulia watanzania kabisa!

Asilimia 90-100% ya watu wenye vidonda vya tumbo lazima wamesabibishiwa na bacteria anaitwa H.Pyroli.
Rejea hii tafiti The prevalence of Helicobacter pylori in peptic ulcer disease. - PubMed - NCBI

Katika visababishi vyako vya vidonda vya tumbo haujataja huyo mdudu umeishia kutaja vitu kama msongo wa mawazo ambavyo vilishaacha kuaminika kuleta vidonda vya tumbo.

Katika tiba zako hizo hakuna tiba inayoweza kumuua H.Pyroli hivo unawaua watanzania wazi wazi maana complication ya hivo vidonda ni kwamba kuna siku vinaweza toboka usipovi control au kuvitibu na unajua tumbo likitoboka usipofanyiwa upasuaji wa ku repair unakwenda na maji...Majirani zako wanaishia kusema utakua ulilogwa kumbe haukutibu vidonda vya tumbo inavyotakiwa.

Kuna dawa kama Diclopa ambazo watanzania wengi wanazitumia na wnegine huzitumia kwa mda mrefu labda wale wenye joint pain au maumivu ya mgongo.

Dawa hizi jamii ya NSAIDS zinapunguza ile mucus/ute unaolinda kuta za tumbo dhidi ya acidi inayotolewa kwenye mfumo wa chakula!
Hivo ukiondoa ute huu kwa kutumia hizo dawa unazidi kujimaliza!

Nafikiri itabdi niandae somo kwa ajili ya vidonda vya tumbo ili watanzania walioko humu jukwaani waache kudanganyika!
 
Mahitaji
-kiini cha kabichi
-kiazi kitamu 1

Matayarisho
-chukua kiini cha kabichi na kiazi kimoja ukimenye na ukate vipande vidogo vidogo
-weka maji kikombe kimoja ..saga kwa pamoja
-chuja
-juice yako itakua tayari kwa matumizi

Matumizi
-tumia mara moja kwa wiki ..ila kama utaweza waweza tumia mara mbili kwa week (haileti madhara)
Fanya ivyo ndani ya mwezi mmoja utabaki tu kusimulia wenzio kua ulikua na vidonda vya tumbo

Ahsanteni
 
Hivi jamani vidonda vya tumbo vinatibika kwa dawa gani, nina ndugu yangu katumia dawa za hospital lakini hajapona. Kwa yeyote anaefaham dawa ya huu ugonjwa tafadhari

Bongo sihami ng'oo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…