Salaam,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,siku ya jana nililazimika kufika hospital hasa kwaajili ya kuchunguza afya yangu na kwabahati mbaya nimegundulika na vidonda vya tumbo.
Hospital wamesema wao wanazo dawa lakini kupitia mama yangu ambaye alishawahi kuugua vidonda vya tumbo na kisha alipona kupitia tiba mbadala kwa urahisi na kwa muda mfupi na kwasasa unakula vile vyote vinavyokatazwa kwa wenye vidonda vya tumbo pasipo madhara yoyote.
Changamoto niliokutananayo mama amepoteza mawasiliano ya mjuzi aliyemtibu na hakuna namna anaweza patikana tena.
JF ni kila kitu kwani ni imani yangu nitashauriwa vizuri hata ikibidi tiba yake,japo imani yangu inaniambia humu JF ninaweza mpata mtu aliyewahi kuugua vidonda vya tumbo na hatimae akapona baada ya tiba huyo ni rahisi kunipa dira sahihi kwani licha ya kuwa kweli mama alipona kwa urahisi lakini matapeli pia wapo.
Pia ni rahisi humu kupata ushauri wakidaktari.
thnx