Ukosefu wa mbegu za kiume/zero sperm count/azoospermia unaotokana na uwiano usio sahihi wa vichocheo hasa ule unaosababishwa na kiwango kikubwa cha kichocheo cha FSH kuliko kile cha LH na Testestorone, hot tubes nk nini chanzo chake? Je, kwa level yetu ya tiba kitaifa inawezekana kurekebishika kama si kutibika kabisa? Tafadhali nahitaji maelezo ya kitabibu. Hospitali yetu ya taifa MNH hakuna vipimo vya kawaida tu kama hormonal tests!!! nk. Kwa wenzetu majuu mf: Dr.Turek na wenziwe wameonyesha mafanikio makubwa katika tafiti zao juu ya ugumba wa aina mbalimbali kwa wanaume. Tusaidiane kwa anaefahamu vizuri, Ahsante.