Ugumu wa kufanya biashara Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Matatizo mengi ya ugumu wa kufanya biashara Tanzania yanasababishwa na tamaa za serikali za pesa za haraka. Kufungua LLC company Tanzania ni 600,000 ili uweze kufanya biashara kama kampuni sio binafsi. Baada ya mwaka tu hiyo licence ya 600,000 muda wake unaisha.

Kibaya zaidi hata kama hujatengeneza pesa unatakiwa kulipita tena na ukichelewa kuripoti unadaiwa 200,000 fini. Sasa ujue kwamba hapo umefungua biashara na hujaanza hata kupata faida. Vilevile ni lazima uwe na ofisi . Sasa cha ajabu ni kwamba kwa nini ni lazima niwe na ofisi wakati naweza kutumia nyumbani kwangu kama ofisini.

Pili kwanini license ni ya mwaka wenzetu wanaweka miaka mitatu maana biashara mpya mwaka mmoja hautoshi kwa licence. Tatu je serikali ina nia ya kukushanya kodi kutoka kwa biashara au hizi fees maana wenzetu wanaweka fee ndogo ili wengi wafungue biashara maana serikali inatakiwa ikusanye kwenye kodi. Hii inasababisha watu wengi kufungua biashara bila leseni.

Serikali vilevile haiangalii kwa upana faida za biashara. Watu wengi wanafungua biashara na kufunga baada ya mwaka kwasababu wanalipishwa sana kabla ya biashara kufanikiwa
 
Brilliant
 
Ukiishapata leseni ukafungua biashara, kutoka halmashauri , naongelea retail shop ,unalipia shilingi 85,000. baada ya wiki anapita afisa wa halmashauri na barua ya madai ya service leavy ya shiling 60,000 . Ukiuliza hiyo imekaaje, unaambiwa ni 0.003 ya mauzo yako. unauliza tena ndo nimeanza biashara nina wiki mbili tu hata wateja hawajazoea hapa dukani. unapewa siku 14 uwe umelipa la sivyo utapigwa faini na kufungiwa
Yaani hii nci ni shida sana
 
Watapatikana wachache kuchangia na wengi wao watamuita mpiga dili badala ya kuchangia na kupanua mawazo ili serikali ijue wapi wanakosea
Magufuli na watu wake wamekosa ubunifu, sio waelewa na wala si wasikivu. CCM na Mataga wote kwa ujumla, Uzi kama huu ni mtaji kwenu, ufanyieni kazi
 
Hivi hawa maprofesa wetu wanashindwa kitu gani kumshauri rais juu ya hali halisi ya uendeshaji wa biashara zetu ili kufungua milango ya kukuza uchumi wetu?
 
Hivi hawa maprofesa wetu wanashindwa kitu gani kumshauri rais juu ya hali halisi ya uendeshaji wa biashara zetu ili kufungua milango ya kukuza uchumi wetu?
Biashara tz. ukifanya kama wanavyotaka hutoboi kamwe, miaka miwili nyuma nilijaribu ku formalise biashara in terms ya kampuni ndogo ya....baada ya kujitamburisha tra, almashauri na kwingineko, miezi sita ilitosha kabisa kurudisha nyuma biashara na miezi michache inayofuata ninge turn tu zero, nikafunga kwa dharura, nikaua kampuni formally nikafungua tena biashara kwa namna ambayo inafaa zaidi, sasa mambo ni poa kabisa.
Biashara inaitaji ujasiri sana kwenye nchi kama tz.
 
ha ha ha,nyie wananchi hamjui tunapokuwa madarakani huwa tunanogewa munoo,haya mambo madogo madogo huwa hata hayatushughulishi,,wewe lipa tu bana,kama hutaki hamia msumbiji hatubembelezani hapa
 
Nakuelewa sana mkuu maana wote tumepitia huko huko
 
Wengi wamesha sepa zao
ha ha ha,nyie wananchi hamjui tunapokuwa madarakani huwa tunanogewa munoo,haya mambo madogo madogo huwa hata hayatushughulishi,,wewe lipa tu bana,kama hutaki hamia msumbiji hatubembelezani hapa
 
Na ole wako ufungue biashara ya bidhaa au huduma zinazodhibitiwa ndo utakama. Kila mamlaka itakuja na na madai yake.
 
Kwenye nchi ambayo ina mfumo mbovu wa ukusanyaji kodi na sera mbovu za uchumi ni rahisi sana kuepuka hizo kashi kashi kupitia kwenye informal sector.
 
Hahahahaha hapa "Nikaua kampuni formally nikafungua tena biashara kwa namna ambayo inafaa zaidi, sasa mambo ni poa kabisa" hapa nimekuelewa mkuu bila kifanya biashara kwa namna inavyofaa kwa bongo hutoboi. Nilikuwa na biashara nalipia zaidi ya milioni moja kwa mwaka kwa huduma ambazo haziongezi tija kwenye biashara. Nikajakuongeza mpesa na mitungi ya gesi kwenye ofisi. Hapo nikaalila tena watu wengine wakaja halimashauri Wanataka leseni ya mpesa 80,000/ ya gesi 80,000/ hapo nimeisjalipia leseni ya biashara kama 200,000/ wakaja fire mtungi 60,000/ fire certificate 100,000/
 
Nchi hiii hii ??
 
Kutoboa biashara Tanzania ni ngumu sana mazingira hayatupi nafasi ya kufanikiwa labda usiende wanavyotaka wao...badala ya wao kufikiri kukuza biashara wao ndio chanzo kikuu cha kuua wanaoanza kufanya biashara malipo ni mengi hata biashara bado haijaanza haijafanyika...
 
Hivi hawa maprofesa wetu wanashindwa kitu gani kumshauri rais juu ya hali halisi ya uendeshaji wa biashara zetu ili kufungua milango ya kukuza uchumi wetu?
njaa ndo kitu inasababisha mtu kufanya mambo kinyume na inavyotakiwa
 
Du hii nchi ni balaa, yaani, unawambia mtaji ni shs 2,000,000, TRA, wanasema Lipa Kodi 500,000, Leseni 80,000. Nyumba ya bisshara 480,000 kwa miezi Sita. Unakuta pesa yote umemaliza. Du TANZANIA NGUMU SANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…