Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Boloyoung

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
682
Reaction score
652
Ebu fikiria dada anayechoma mahindi maeneo ya manzese darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku, kwa siku moja ana uwezo wa kuchoma mahindi 50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/= na anauza kwa sh 600/=

Hiyo ina maana mahindi 50 ananunua kwa shilingi 5000/= akichoma na kuuza anapata sh 30,000/= akitoa pesa ya mtaji ( 5000/= ya mahindi na 1500/= ya mkaa) anabakiwa na sh 23,500/= kwa siku.

Hivyo kwa mwezi huyu mchoma mahindi atakuwa ameingiza kiasi cha sh 705,000/=

Mwalimu mwenye degree anayeanza kazi analipwa 584,000/= akikatwa kodi pamoja na makato mengine ya mifuko ya jamii anabakiwa na sh 425,000/=

Tofauti ya mwalimu wa degree na muuza mahindi ni kuwa mwalimu kaajiliwa, muuza mahindi kajiajiri. Mwalimu anafanya kazi masaa 9 kwa siku, muuza mahindi anafanya kazi masaa 3 kwa siku ( saa 12 jioni hadi 2 usiku) mwalimu anatumia muda wake wa ziada kusahihisha mitihani na homework mchoma mahindi anatumia muda wake wa ziada kutafuta fursa nyingine za kupata hela.

Uoga wako ndio umaskini wako.
 
Ni kweli kuchomea mahindi mtandaoni na hesabu hesabu nzuri nzuri inatoa matokeo makubwa kweli

Utata ni unapoingia field sasa.Leo wateja wachache,kesho mmekimbizana na wagambo,keshokutwa mvua imenyesha umeshindwa kwenda etc etc
 
Ni kweli kuchomea mahindi mtandaoni na hesabu hesabu nzuri nzuri inatoa matokeo makubwa kweli

Utata ni unapoingia field sasa.Leo wateja wachache,kesho mmekimbizana na wagambo,keshokutwa mvua imenyesha umeshindwa kwenda etc etc
Safi sana, kuna watu mawazo yao ni zaidi ya mgando anawaza side A pekee bila kufikiria na side B
 
Back
Top Bottom