Ugumu wa maisha ndiyo utakuja kuiangusha CCM

Ugumu wa maisha ndiyo utakuja kuiangusha CCM

In real sense hakuna kitu kama CCM (kwa maana ya chama cha SIASA) Bali kuna kagenge flani kanakotumika kupora rasilimali za Watanzania kwa kutumia state apparatus
 
Wananchi wanateseka sana kwa ugumu wa maisha na kila kukicha afadhali ya jana. Bei ya bidhaa, vifaa vya ujenzi, mafuta kila kukicha unakuta bei ya jana siyo ya leo.

Leo nimesoma kuwa bei ya mafuta kwa mwezi huu wa Aprili imepanda tena. Kama jirani zetu hapa Kenya, Zambia bei ya mafuta kwao ni nafuu mbona Tanzania kila mwezi bei inapanda kulikoni? Msione wananchi wako kimya wanaumia sana na matokeo yake ni siri yao.

Tusubiri uchaguzi wa mwaka huu na mwaka ujao.
maisha magumu yakuchape wewe binafsi na uvivu wako, halafu uje kutushia wachapa kazi zao kwa bidii....
 
CCM haianguki bali baadhi ya wanachama ndiyo wataanguka.
 
Maneno KUNTU sana haya...upo vizuri kiongozi...Hakika,wengi hawafahamu uhusiano wa Maisha na Serikali iliyopo madarakani..Wanaamini UGUMU huu umeletwa na Mwenyezi Mungu

Shukrani mkuu na ni kweli, ukiona nchi kama Kenya zinaandamana kwa ajili ya bei ya unga ujue wananchi wanajua fika sehemu ya serikali katika kuupandisha na kuushusha bei kupitia kodi.
Kwetu wanalaumiwa wafanyabiashara na magumu yakizidi tunarudi madhabahuni kama ulivyosema.
Hiyo ndio tofauti 🙏🏽
 
Wananchi wanateseka sana kwa ugumu wa maisha na kila kukicha afadhali ya jana. Bei ya bidhaa, vifaa vya ujenzi, mafuta kila kukicha unakuta bei ya jana siyo ya leo.

Leo nimesoma kuwa bei ya mafuta kwa mwezi huu wa Aprili imepanda tena. Kama jirani zetu hapa Kenya, Zambia bei ya mafuta kwao ni nafuu mbona Tanzania kila mwezi bei inapanda kulikoni? Msione wananchi wako kimya wanaumia sana na matokeo yake ni siri yao.

Tusubiri uchaguzi wa mwaka huu na mwaka ujao.
unaota ndoto za mchana. uchaguzi ukikaribia mambo yatabadilika hadi mwenyewe utashangaa!
 
Back
Top Bottom