Ugumu wa maisha ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia ongezeko la changamoto za afya ya akili

Ugumu wa maisha ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia ongezeko la changamoto za afya ya akili

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Ikiwa leo ni Siku ya Afya ya Akili Duniani, Msaikolojia Tiba wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Arafa Ali Arajiga, amesema ugumu wa maisha ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia ongezeko la changamoto za afya ya akili, hususan kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 50.

Akizungumza katika mahojiano maalumu jijini Dodoma, Arajiga amesema sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa ajira, misukosuko ya mapenzi, pamoja na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili vijana na watu wazima.

Amesema changamoto hizo huathiri kwa kiasi kikubwa utimamu wa akili na kuchangia matatizo kama msongo wa mawazo, huzuni ya muda mrefu, na hata hatari ya watu kujiua.

Mtaalamu huyo ametoa wito kwa jamii kuchukua hatua mapema kudhibiti mazingira yanayochochea matatizo ya afya ya akili na kuwasaidia wahanga kupitia ushauri nasaha na matibabu stahiki.

Siku ya Afya ya Akili Duniani huadhimishwa kila Oktoba 10, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya afya ya akili na kuhamasisha juhudi za kimataifa katika kuzuia, kutibu na kusaidia watu wenye changamoto hizo.
 
Back
Top Bottom