Ugunduzi: Kijana Mtanzania atengeneza mpira wa miguu wenye viwango vya kimataifa

Ugunduzi: Kijana Mtanzania atengeneza mpira wa miguu wenye viwango vya kimataifa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kijana wa chuo cha DIT Amani Simba amemshangaza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robert kwa uwezo wake wa kufuma mpira wa miguu wenye viwango vya kimataifa alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho mwishoni mwa wiki hii.

Kwa Maelezo ya Mkurugenzi wa Chuo hicho tawi la Mwanza Dkt Albert Mmari, kijana huyo ameonyesha kipaji cha kipekee tangu ameanza masomo chuoni hapo.

 
Wekeni picha ya huo Mpira tuuone
 
Hivi Kugundua ni nini ?

Na suala la mipira Bora au Bata hawakuwahi kuzalisha?

Tatu viwango vitapimwa kwa mpira mmoja mmoja au baada ya kufanya mass production na kutoa maelfu ya mipira kwa dakika ?, Anyway kama tumefika hapo tusipoteze muda TFF waanze kununua kutoka hapa ila huenda ukakuta cost of production ya hapa na mipira ya huko ni mbingu na dunia ?

Am not a Hater ili hawa wataalamu wetu huko vyuoni wangekuwa wanashindana kutatua changamoto zetu na kwa ulimwengu wa sasa kushindana na kina Adidas na Nike katika utengenezaji wa mipira its a tall order unless otherwise ni ya bei nafuu sana tuweze kuitumia locally. Kudos kwa Kijana ila as a Country we have a long way to go.
 
Saf sana
Tunataka ona mambo kama haya
Siyo kila siku sjui nandy,baba levo,mobet,
Mndi knde wanaonekana wao tu kama ndy
Wanafanya mambo muhimuuu

Ova
 
Kijana wa chuo cha DIT Amani Simba amemshangaza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robert kwa uwezo wake wa kufuma mpira wa miguu wenye viwango vya kimataifa alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho mwishoni mwa wiki hii.

Kwa Maelezo ya Mkurugenzi wa Chuo hicho tawi la Mwanza Dkt Albert Mmari, kijana huyo ameonyesha kipaji cha kipekee tangu ameanza masomo chuoni hapo.

View attachment 1933162
Ugunduzi ni kufanya kitu kipya ambacho hakikufanywa hapo awali.

Huyu kakopi tu hakuna ugunduzi hapo.
 
Miaka hiyo watoto wa kibongo walikua wanatengeneza kwa mikono yao wenyewe vifaa vyao vya kuchezea wakitumia locally available materials

Walitengeneza models za magari, nyumba, mipra ya kuchezea na vitu vingine vingi tena vizuri sana kwa kile wazungu wanaita "state of the art". Waliokua wakifanya hivyo ni watoto wa shule za msingi hasa nyakati za likizo zao.

Siku hizi eti hata manati wanatengeneza watu wazima na jamii inazishangaa!!! Naamini kama nchi ingeendelea kuweka restrictions za kuagiza hadi wanasesere kutoka ughaibuni kama ilivyokua enzi za Mwalimu, basi kizazi cha watoto wa Kitanzania wangekua wamesha develop na kufanya mambo makubwa zaidi kuliko kuja kushangaa mwanafunzi wa chuo tena course ya Engineering(in what?) ku assemble mpira wa kuchezea!!!
 
Umepimwa na nani kwanza hadi kusema umefikia viwango vya kimataifaaa..
...Mheshimiwa kaungalia tu kwa Macho kaamua ni Mpira Bora!![emoji853]
Tunapenda kuingiza Mizaha kwenye mambo yetu Mengi....Ndio Maana yanaishia hapo hapo!
Hata hili baana ya 'Breakin News' hii hutalisikia teena...!!
 
Back
Top Bottom