Unaijua MPEMBA THEORY?
Ni rahisi Sana kwa wanafunzi wa kitanzania wakakujibu iwapo utawauliza kuhusu Archimedes Principle, Pascal's law, Avogadro's Law, Newton's law au theory nyingine maarufu
Lakini iwapo utawauliza kuhusu mpemba theory kati ya wanafunzi laki moja wa kitanzania Hakuna hata mmoja anaeweza kukujibu
Basi ni hivi.........
Mpemba's theory ni theory iliyogunduliwa na mtanzania anayejulikana kama Erasto B. Mpemba mwaka 1963 akiwa kidato cha tatu katika shule ya secondary magamba iliyopo lushoto mkoani Tanga
Nadharia yake ina sema kwamba " MAJI YA MOTO NI RAHISI SANA KUGANDA KULIKO MAJI YA BARIDI"
nadharia hiyo imeendelezwa na wanasayansi wengine akiwemo Profesa Osborne wakasema kuwa unapo yarusha juu maji ya moto kwenye sehemu za baridi kali ni rahisi Sana kuganda na kuwa vibarafu kuliko ukirusha maji ya baridi
Tangu Mtanzania huyu kugundua kanuni hiyo iliyopewa jina la Mpemba effect, mpaka leo ni miaka 50 lakini hatambuliki kabisa na taasisi za kisayansi wala zile za kitaaluma kama vyuo hapa nchini. Jambo la kushangaza, Mpemba ni maarufu sana kwenye taasisi za kimataifa, wanayansi wamehangaisha vichwa kujua sababu ya maji ya moto kuganda haraka zaidi kuwa barafu kuliko yale ya baridi.
Mwaka 2013, The Royal Society of Chemistry, baada ya kuwatangazia wanafunzi wote wa sayansi duniani wanasoma shahada ya uzamili kuwa wafanye tafiti za kugundua sababu za suala hilo.
Kwanini, zaidi ya miaka 50 tangu mpemba atambulishe nadharia yake lakini Hakuna anayemjua Tanzania zaidi ya kujulikana kimataifa?