Ugunduzi wa Erasto Mpemba, (Maji ya moto kuganda haraka kuliko ya baridi) 'The Mpemba Effect' kwanini hatukufundishwa mashuleni?

Hii ni nadharia (theory) tu ,haijathibitishwa (proven) na pia sio ugunduzi yaani Invention kwa hiyo sielewi comment zako zinalenga nini hasa wakati hata jina la hiyo observation wameipa la huyo jamaa.
Yeah it's just a merely theory,but it takes a courage of one to develop a such theory.You and I have dared to develop nothing ,and after all his mere observation has been appreciated and published in physics journals ,
Tukubali tu ,jamaa alikuwa na kitu special kutuzidi,hizi roho za kwanini hazitupeleki popote.
 
Kwa kweli ugunduzi huu wa mpemba kama ungetiliwa mkazo, najua angekuwa mbali sana na katika vitabu vya wagunduzi basi angekuwa mmoja wao..tena wagunduzi nguli wa fizikia
ushatiliwa mkazo sana mpaka majibu yakapatikana
 
Nimemsikiliza bwana Erasto B. MPEMBA clouds TV kuhusu maisha yake na ugunduzi wake aisee haki ya mungu kwa sayansi hii hatutaendelea na hatutapata wanasayansi wabobezi hasa bongo
 
ugunduzi ndivyo ulivyo hata wewe unaweza umekalia ugunduzi hapo ulipo mwingine
atausemea
 
ugunduzi ndivyo ulivyo hata wewe unaweza umekalia ugunduzi hapo ulipo mwingine
atausemea
Hata Archimedes alifanya ugunduzi wakati anaoga ijapokua yeye co wakwanza kuoga ila ugunduzi ni pale unapoweza kujibu maswali haya juu ya udhani huo
HOW? WHY? And significance of it
 
Kiukweli theory ni nzuri na yakipekee ila nauliza mpemba effe inafaida gani katika universe
 
Kiukweli theory ni nzuri na yakipekee ila nauliza mpemba effe inafaida gani katika universe

Huwezi kupata faida kabla ya kupata uthibitisho wa kisayansi. Mpemba aligundua lkn hakuweza kutoa maelezo ya kwa nn hutokea hvyo. Naamini mwisho angetengeneza formula ambayo ndio huwekwa ktk application.
Kinadharia mpemba effect ni Freezing is directly proportional to temperature...lzm atafute constant( unknown) ambayo angeita mpemba constant...! Angeprove hyo constant ndipo ingeweza kuingia ktk application kirahisi.
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
nimemwona leo clouds tv jamas analalamika sana ugunduzi wake umemnufaisha m criatia najiuliza hivi akina newton walinufaikaje!?
 
Huyu jamaa kwanini haenziwi???
 
Habarini wanabodi.

Jana katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii, twitter, nikakutana na kitu ambacho nilikua sikijui. Kwamba kuna mtanzania Ndugu, Erasto Mpemba, ndiye aliye gundua kuwa maji ya MOTO yanapoa haraka zaidi kuliko maji ya baaridi endapo yote yatawekwa kwenye jokofu!!!!



Swali langu ni kwanini hatukufundishwa hii kitu mashuleni, kwanini huyu ndugu Erasto Mpemba hakua promoted na serikali kiasi tukamjua na kutambua mchango wake kwa jamii ya kitanzania na dunia kwa ujumla?



Ninaimani kuna watanzania wengi ambao huwa wanafanya vitu vingi vizuri ila the same questions, huwa ni kwanini hawa jamaa huwa hawapewi promo na support na serikali yetu? Nilikwisha sikia na kuona watz wakitengeneza majenereta, ndege, radio, na vifaa vingine vya umeme kwa ujuzi wao binafsi ila baada ya hapo kimya kabisa...shida huwa ni nini??



Nadhani kuna umuhimu wa kuenzi na kuvipenda vyakwetu. Tuachane na Elimu ya kukaririshana kutoka kwenye mitaala ya wazungu inayoandaa waajiriwa badala ya watengeneza ajira.



Naomba kuwasilisha.

Asubuhi njema.
 
Selikali yenyewe haijasoma vitu ivyo ,,vitapewa vipi kipaumbele ??[emoji53]
 
Mtu mweusi hana thamani. angekuwa mwingereza ua mmarekani angesifika sana dunia nzima, na sisi tungemuweka katika mitaala yetu (kama tulivyoweka newton's law of motion, archmedes principle, darwin sijui nini nini...)

Tatizo ni mfumo wetu. elimu yetu inategemea sana mitaala ya wazungu, vitu vingi tunatoa kutoka kwao hasa kwa masuala ya sayansi. mwisho wa siku tunabaki kuwa inferior tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…