Feisal2020
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 1,113
- 2,656
"Serikali yenu, tunajua tatizo la ajira na tutajitahidi kutengeneza fursa mbalimbali ili vijana wapate ajira.” Leo ni tarehe 9 Juni, 2024, takribani miaka miwili na miezi yake kadhaa tangu kauli hiyo itolewe na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Suala la iwapo Serikali i'ME'jitahidi au bado wa'TA'jitahidi kutengeneza hizo fursa lina maoni tofauti tofauti, hayo tuyaache, kwa sasa tuwasaidie kuwakumbusha baadhi ya mambo muhimu wakiwa 'wanajitahidi' au watakapoanza 'kujitahidi' kutengeneza hizo fursa wayazingatie.
Mheshimiwa Raisi vijana tunatambua na kuthamini juhudi zako na Serikali yako tukufu katika kukuza sekta ya kilimo, tumeona namna ambavyo Serikali inajitahidi kuboresha miundombinu kwa wakulima na hata ule mkakati wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), hakika unaupiga mwingi sana hongera! Lakini mheshimiwa sio kila kijana anataka kulima, maisha yana milango mingi ya kutokea.
Hapa nchini kuna wimbi kubwa la
watu linatafuta ajira, huko mitandaoni kuna ajira nyingi zinatafuta watu, kitu pekee kimekaa katikati ya hivyo vitu viwili ni maono na mikakati dhaifu ya viongozi wa nchi hii.
Huko Fivver, UpWork, Freelancer na TrueLancer kuna watu binafsi na makampuni mengi yanahitaji watu kwa ajili ya:
BILA KUMUNG'UNYA MANENO, KISWAHILI KINATUFELISHA!
Ndio nimesema hivyo, na ninarudia tena KISWAHILI KINATUFELISHA!
Naelewa kwamba tunao wajibu wa
kujivunia, kulinda, kuthamini na kukuza lugha yetu hii adhimu, kitu abacho tunakifanya sana.
Wanyakyusa, Wamasai, Wameru n.k, wakikutana watahitaji lugha moja ( Lingua Franca) ili kuwezesha mawasiliano baina yao, lugha hiyo imetokea kuwa Kiswahili. Vile vile Watanzania, waamerika, wajerumani, wakenya n.k wakiingiliana watahitaji lugha (Lingua Franca) kuwarahisishia mawasiliano, lugha hiyo imetokea kuwa Kiingereza.
Hatuwezi kusema tunataka kwenda sawa na Gig Economy
huku tunaendelea kufundisha watoto wa shule za msingi kwa lugha ya Kiswahili! Hizo ajira hatoi Malisa wa kule Rombo, hatoi Mwakalinga kule Tukuyu wala Manyesha wa kule Shinyanga kwamba utahitaji Kiswahili kuwasiliana nae au kufanya kazi husika kwa lugha hiyo.
Majukwaa ya Freelancers na fursa nyingi za mtandaoni zinahitaji watu wenye uwezo mkubwa wa kuwasiliana kwa lugha ya Kiingereza, bahati mbaya sana ukosefu wa ujuzi wa Kiingereza kwa vijana wa Tanzania imepelekea tushindwe kushindania fursa hizo. Tuendelee kufundisha watoto wa shule za msingi kwa kutumia Kiswahili tu kama tunataka kuwanyima fursa kwenye Gig Economy,
ikiwa lengo ni kinyume na hivyo basi kiingereza hakikwepeki.
Wengi tuliosoma kutumia huu mfumo wa elimu tuna unyonge wa kuwasiliana kiufasaha kutumia lugha ya Kiingereza hata kama tulifika vyuo vikuu kwani kipindi tuna uwezo mzuri wa kuelewa tulifundishwa kwa Kiswahili, kisha tukaja kukaririshwa kwa Kiingereza kuanzia sekondari na kuendelea.
Sio tu kwamba unyonge wetu huu unafanya ajira nyingi za mtandaoni ziwe kwa ajili ya Wakenya, Wanaijeria na Waafrika Kusini, lakini pia unadhoofisha hali ya kujiamini, uwezo wa kufikiria na kuendana na utandawazi.
"Usipowinda utawindwa" -
Dizasta Vina, "If We are not monsters we are food" -
Kane 'Sully' Robinson; kwa sababu sisi hatujishughulishi kuwezesha watoto wetu kujua kiingereza kwa ufasaha, hata hizi kazi za kutafsiri kiingereza kwenda kiswahili au kinyume chake zinachukuliwa na wakenya ambao wao wanamudu lugha zote mbili, kalagabaho sisi tunaokazania kiswahili tu tuendelee kusubiri zije hizo kazi za kutafsiri kiswahili kwenda kiswahili.
PAYPAL NI MPESA YA DUNIA, TURUHUSU KUITUMIA KUPOKEA MALIPO
Tunaishi kwenye dunia ambayo watu jamii zinahitaji kujenga madaraja zaidi ya kuta baina yazo. Sisi kama nchi kuendelea kujitenga na dunia haifanyi dunia isimame kutungoja.
Moja ya mambo muhimu sana kwenye Gig Economy
ni hitaji la msingi kabisa la kuruhusu na kutumia platform za malipo za kidunia kama vile PayPal.
Kwenye dunia ambayo mtoa kazi (client) yupo London, na mfanyaji kazi (freelancer) yupo Igawilo, tunafikiri watatumiana malipo kupitia TigoPesa au pesa itatumwa kwenye kimbinyiko?!
Kuna ugumu gani kwa viongozi kuwafungulia dunia wajasiriamali, freelancers na wafanyabiashara wadogowadogo waweze kufikia masoko ya kimataifa kwa kutumia mfumo salama wa malipo wa PayPal? Kutoruhusu malipo kwa njia hii ni tatizo kubwa kwa vijana wanaotamani kujihusisha na Gig Economy au tu kufanya biashara zao kimataifa.

- Kubuni grafiki (nembo za makampuni, matangazo n.k)
- Kuandika Maudhui
- Kutafsiri/Kukalimani
- Huduma kwa Wateja, n.k n.k

Upvote
1