Inasikitisha kuona watoto wanasoma wakiwa wamekaa kwenye matofali, mifuko, mabox, nk wakati kuna mwalimu mkuu, kamati ya shule, mratibu wa elimu, wazazi, afisa elimu, mkurugenzi wa halmashauri, mbunge nk. Huu ni upuuzi unaopaswa kukomeshwa. Watanzania tumekosa uwajibikaji kuanzia kwa watu binafsi, familia hadi viongozi wa ngazi za juu. Imefikia muda sasa tumwogope Mungu.