Uhaba wa mafuta unaisogelea Dar, bei ya Petroli kwa Kibaha yapanda kutoka Tsh. 2,700 hadi 3,700 ghafla

Uhaba wa mafuta unaisogelea Dar, bei ya Petroli kwa Kibaha yapanda kutoka Tsh. 2,700 hadi 3,700 ghafla

Hivi Serikali inaposema mafuta yapo harafu bei zinapanda Kwa kiasi hichi tuwaelewaje?
Nenda kawaulize,unangoja nini!!!

Siyo wewe kila siku kila saa unakata kata viuno humu kuwasifia hao wanaoruhusu watu kupandisha bidhaa jinsi wanavyotaka wao?
 
Nipo hapa Manyovu border to Burundi nao wanakimbilia TZ kununua mafuta nasema hivi ile kauli ya Mwigulu naenda itimiza soon kuhamia Burundi tu
 
Tulieni mama anafungua nchi😂😂 anaupiga mwingi
 
Woga wako tu, mimi ikifika 14,000
Changamoto ya uhaba wa Petroli sio jambo geni tena kwenye masikio ya watu hapa Bongo, lakini binafsi nilikuwa sijaona changamoto hiyo kwa Dar na maeneo ya karibu na Mji huo.

Kila siku tumekuwa tunasikia mikoani tu kuwa uhaba wa mafuta na mara bei inapanda, inadaiwa kuna mgomo wa kimyakimya ambao unafanywa na Wafanyabiashara wakitaka bei ya mafuta ipande.

Serikali kupitia EWURA na Waziri Makamba naona wanakanusha kila siku kuwa hakuna changamoto hiyo lakini naona kabisa wanaanza kuzidiwa nguvu katika hiki kinachoendelea.

Usiku wa kuamkia leo nikiwa mitaa ya Kibaha Maili Moja kabla ya saa sita usiku bei ya mafuta ya Petroli Lita Moja ilikuwa shilingi 2,700, lakini ghafla ilivyofika saa sita usiku vituo vyote vikapandisha bei na Lita Moja kuwa shilingi 3,700.

Kinachosikitisha ni kuwa EWURA hawajatangaza mabadiliko hayo lakini tayari bei imepanda na kila siku tunamsikia Makamba na EWURA yake wakiishia kupiga mikwara.

Vituo vya kukuza mafuta vya Njuweni hadi Picha ya Ndege vyote bei imepanda ghafla, nimeshuhudia watu wengi walilalamika tu huku wakiwa hawana namna nyingine ya kufanya.


Uoga wako tu, mimi ikifika Tsh 24553 kwa liter ndo nitashtuka, ila chinj ya 24552 kwa liter wala hakuna shida.
 
Back
Top Bottom