DOKEZO Uhaba wa watumishi wa afya unavyochochea rushwa Maswa

DOKEZO Uhaba wa watumishi wa afya unavyochochea rushwa Maswa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Zipo tuhuma kwamba baadhi ya wagonjwa katika Halmashauri ya Maswa mkoani Simiyu wamekuwa wakitoa rushwa kwa wahudumu wa afya ili wapatiwe huduma mapema wanapofika katika vituo hivyo.

Ni mbinu ya wagonjwa kukwepa misururu mirefu kupata huduma za afya.

Mara nyingi malalamiko ya vitendo vya rushwa hutolewa na wananchi wakilalamikia watoa huduma, lakini kwa Maswa hali ni tofauti kwani watoa malalamiko ni watoa huduma wa afya ambao wamekuwa wakishawishiwa na wagonjwa kuwapatia rushwa ili waweze kupata kipaumbele cha kupatiwa matibabu.

Jambo hilo si zuri halikubaliki na ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa baadhi ya wagonjwa hushawishika zaidi kutoa rushwa wao wenyewe kwa watoa huduma.

Hali hii inatokana na uhaba au uchache wa watumishi wa afya hasa katika zahanati zilizoko katika wilaya ya Maswa hali kusababisha mlundikano na misururu mirefu ya wagonjwa katika zahanati hizo huku wakitumia muda mrefu kusubiri kufikiwa na huduma za tiba.

Katika wilaya ya Maswa zipo zahanati ambazo zina mhudumu mmoja tu ikiwemo ile ya kijiji cha Jija ambayo mgamga wake pekee aliyepo, inahudumia wakazi zaiidi ya 14,000 ambao ni wakazi wa vijiji vya Jija na Ilobi.

Mganga huyo Dk Herbert Kambaulaya Ilamba ambaye ni Mganga pekee aliyepo katika zahanati ya kijiji cha Jija ,anasema kuwa amekuwa akishughulikia majukumu mengi ambayo kimsingi yanahitaji timu nzima.

Hali kama hiyo pia ipo katika zahanati ya kijiji cha Mwamanenge ambayo ina mhudumu mmoja ambaye ni muuguzi akiitwa, Kwiligwa Shija. Zahanati hiyo inahudumia vijiji vitatu ambavyo ni Mwamanenge, Inenwa na Mwanghonoli, vyote vikikadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya 12,000.

Hali inapaswa kuwaje?

Mwongozo wa utumishi wa Umma wa mwaka 2014 umeagiza kuwa kila zahanati iwe na watumishi wasiozipungua 10, lakini hali ni tofauti katika baadhi ya zahanati za Maswa na kusababisha kuzorota kwa utoaji wa huduma za afya.

Mwongozo huo unawataja watumishi wanaotakiwa kuwepo kwenye zahanati ni pamoja na Matabibu (2), Wauguzi (2) ,Mteknolojia wa maabara,Mtoa dawa,Mkunga,Afisa Afya ya jamii,Afisa Kinga na Wahudumu wa Afya.

Licha ya serikali kujishughulisha na uimarishwaji wa sekta ya afya kwa kujenga miundombinu ya majengo, vifaa tiba, dawa na raslimali watu lakini suala la utoaji wahuduma kun atatizo la upungufu wa watumishi wa kada ya afya hasa kwenye ngazi ya zahanati.

Hali ilivyo wilaya ya Maswa

Kutokana na upugufu huo hasa wa Matabibu inabidi wilaya hiyo kuwatumia Wauguzi kuongoza zahanati hizo kama ilivyo kwa zahanati ya kijiji cha Mwamanenge.

Kuna athari kubwa kuwatumia wauguzi kuwa wafawidhi wa Zahanati badala ya Matatibu na kwamba miongoni mwa changamoto ni za kiutawala kama vile kupanga bajeti na kusimamia wafanyakazi.

Athari nyingine ni pamoja na kuwapatia mzigo wa kazi kutokana na kuwapatia majukumu ya ziada ya usimamizi ambayo yanaweza kusababisha uchovu wakazi na kuathiri utendaji wao wa kitaalam.

Hivyo ni vizuri kwa serikali kuliona suala hili japo imejenga miundo mbinu ya afya zikiwepo zahanati na vituo vya afya lakini hazina watumishi wa kutosha.
 
Back
Top Bottom