SoC03 Uhai wa kilimo na mifugo yangu katika nchi yangu

SoC03 Uhai wa kilimo na mifugo yangu katika nchi yangu

Stories of Change - 2023 Competition

Mabula marko

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
44
Reaction score
38
Uhai wa kilimo na mifugo yangu katika nchi yangu

Utangulizi
Tunapozungumzia kilimo na mifugo katika nchi yetu ya Tanzania tunagusa Nyanja ambazo kwa muda mwingi zimebaki kuwa mihimili ya vyanzo vya mapato kwa jamii nying sana za kitanzani shughuli hizi mbili daima zimekuwa na mchango mkubwa pia hata katika pato la taifa ikiwa kilimo kinachangia asilimia 30 na mifugo ikichangia asilimia 7, pamoja na kuchangia ukuaji wa pato la taifa lakini pia shughuli hizi mbili zimekuwa msaada kwa watanzania walio wengi katika kuwatoa katika umasikini ulio pitiliza (extremely poverty), kwani wengi wao kupitia kujishughulisha na kilimo na mifugo wamekuwa wakipata kipato kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za kila siku.

Pamoja na kwamba kilimo na mifugo kimekuwa uti wa mgongo kwa taifa letu na nchi yetu ya Tanzania kuwa namba tatu kwa wingi wa wanyama mtakubaliana name kuwa bado tuko nyuma katika uzalisha na ushindani katika masoko ya kimataifa, bado pia kama taifa wananchi wengi wanalia njaa, watoto wengi wamekuwa wakilipotiwa kuw na utapia mlo, wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini wamebaki tegemezi kwa serikali na ndiyo maana tumekuwa na TASAF, wakati tuna rasilimali kilimo nyingi ambazo zinaweza kutumika kuongeza tija na kuchochea uhai wa kilimo na mifugo yetu hali hii inatoa viashilia vya uzembe katika kila kona ya rasilimali wezesha kilimo na mifugo na pia mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakiondoa kabisa uhakika wa kilimo.

Tatizo liko wapi katika uhai wa kilimo na mifugo yangu

Uhai wa kilimo na mifugo katika nchi yetu umekumbwa na changamoto kazaa ikiwa nyingi ni kutokana na uzembe katika kutimiza wajibu katika kona wezeshi za kilimo na mifugo ingawa mabadiliko ya hali ya hewa nayo ni changamoto.

Mabadiliko ya hali ya hewa, hii ni changamoto ambayo inayo fifisha uhai wa kilimo na mifugo yetu kwani ukosefu wa mvua za uhakika katika nchi yetu imechangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa maji ambayo hutumika katika kuotesha mimea au mazao na pia marisho na maji ya kunywa kwa wanyama hali ambayo imekuwa ikizoofisha uhai wa kilimo na mifugo katika nchi yetu.

Upotevu wa rutuba asilia katika udongo, hali hii imekuwa ikijitokeza kutokana na momonyoko wa udongo na matumizi ya holela ya mbolea za viwandani ambazo mara nyingi zimekuwa zikidhoofisha mbolea.

Migogoro ya wakulima na wafugaji, siku za hivi karibuni tumeshuhudia wimbi la ongezeko la kuwepo kwa vita vya wakulima na wafugaji inayosababisha watu kupoteza wanyama, mazao na hata uhai na makazi yao hali ambayo inatokana na uzembe mkubwa wa kundi hili katika kukaa na kutimiza wajibu wao ipasavyo na pia uzembe wa kiutawala katika kugawa maeneo ya sehemu za kufanyia shughuli hizi tofauti.

Ukosefu wa malisho na maji, hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na uzembe wa wafugaji wenyewe kuto kuhifadhi vyakula vya wanyama wao lakini pia serikali na wataalamu wake kuwa wachoyo wa maarifa ya namna bora na sahihi ya kuhifadhi vyakula na maji kwa ajili ya wanyama wao hasa wakati wa kiangazi ambapo tumeshuhudia wanyama wengi wakiasirika na kufa kabisa.

Migogoro ya wahifadhi misitu, mbuga za wanyama na wafugaji, hali hii imekuwa ikijitokeza kwa sababu ya wafugaji kutafuta marisho kwa ajiri ya wanyama wao hii imekuwa sababu ya watu kuuawa na wahifadhi mifugo kuuliwa, wafugaji kupolwa mifugo yao na wahifadhi na kuwaacha watu masikini.

Upungufu mkubwa wataalamu wa kilimo na mifugo, hali hii ndiyo kilio kikubwa cha wakulima na wafugaji walio wengine, mtakubaliana nami kuwa katika nchi yetu hadi sasa tunamfumo wa Daktari mmoja wa mifugo kuhudumia wilaya nzima hali ambayo imekuwa ikishusha ufanisi kwani walioko chini kwa wakulima ni watu wenye vyeti alafu daktari yuko ofisini wilayani,pia maafisa ugani ni wachache kutosheleza wakulima.

Teknolojia duni, hali hii imechangia kiasi kikubwa kufifia au kuwa na mwamko mdogo wa udhalishaji katika kilimo na mifugo lakini pia hali hii imechangia kuwa na mazao yanayokosa sifa katika masoko yenye ushindani hasa masoko ya kimataifa.

Upungufu wa elimu kwa wafugaji na wakulima juu ya kilimo biashara, uongezaji thamani na kilimo chenye tija.

Namna gani tunaweza kuchochea kuongezeka kwa uhai wa kilimo na mifugo nchini mwetu. Yafutayo ni muhimu tuyazingatie kurejesha uhai wa kilimo na mifugo yetu.

Ujenzi wa mabwawa katika kila madaraja yaliyopo nchi ya saizi ya katika na makubwa nchini hii itasaidia kuwepo kwa maji ya kutosha katika kufanya kilimo cha umwagiliaji na pia maji ya kunywesha wanyama kupitia madaraja tutavuna maji mengi wakati wa masika.

TANAPA, TAWA na wahifadhi wote waje na mradi wa kuvuna manyasi katika maeneo ya hifadhi na kuwauzia wafugaji wote kwa bei nafuu hii itasaidia wafugaji kutoingiza mifugo hifadhini.

Wataalamu waongezwe na wawajibike vizuri katika nafasi zao hii itasaidia sana.

Kupunguza uharibifu wa mazingira tuanze kilimo na ufugaji ulengao kuhifadhi hewa ya kabonidaioksaidi (carbon farming) katika ardhi ili itumike kama mbolea.

Ubunifu unahitajika pia katika kuzuia migogoro ya wafugaji na wakulima ikiwepo matumizi ya mafuta ya simba ya kutengeneza ili kuzuia wanyama kuingia katika mashamba.

Wafugaji wafundishwe namna ya kuhifadhi na kuvuna manyasi wakati wa masika ili yawasaidie wakati wa kiangazi.

Wafugaji na wakulima wapewe elimu juu ya kuchimba visima na mabwawa madogo yatakayohifadhi maji ambayo watayatumia kutekeleza ulimaji wao mdogo na kunyweshea wanyama wao.

Serikali waongeze mawakala wa pembejeo za kilimo ili kuhakikisha kila mkulima apate mbegu bora
Serikali ianzishe mradi wa kugawa mbegu za wanyama kwa wakulima ili waweze kufanya uzalishaji wenye tija.

Serikali na watalamu wake waje na ubunifu mpya wenye lengo la kuwasidia na kuwanufaisha wakulima na sio serikali kufanya kitega uchumi kama katika mfumo wa heleni hizi za kielektroniki kwani hazimsaidii chochote mkulima, kwa saivi teknolojia imekuwa kuna heleni zinazoweza kuunganishwa na simu ya mfugaji ikawa inamsaidia kujua kama mnyama anaumwa au anakalibia kuzaa na kazalika.

Hitimisho
Mwisho uhai wa kilimo na mifugo yangu katika nchi yangu unategemea sana ushiriki wa kila Nyanja kwa uhai na umahiri, hivyo kama kona wezeshi zote zitawajibika ipasavyo tutaongeza tija ya uzalishaji nchi na hata kutoa ushindani katika masoko ya kimataifa, tutaondoa ama kupunguza umasikini pia na baa la njaa na pia nchi yetu inaweza kuwa kiwanda cha vyakula katika nchi za Africa mashariki na kati.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom