Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Mabandiko mengine sio mabandiko ya kitoto!, ukijiona huelewi, we jipitie tuu!.

Angalizo la Alama ya Kuuliza "?".
Mimi mwenzenu jameni, nimewahi kuitwa mahali na kufikishwa mbele ya kamati fulani kwa kutuhumiwa nimesema statement fulani!, kumbe masikini mimi, sikutoa statement, niliuliza tuu!. Aliyenituhumu, hakuiona alama ya kuuliza, hivyo naomba kutoa angalizo la alama ya kuuliza?, bandiko hili sio la statement ni bandiko la swali.

Bandiko hili ni moja ya mabandiko yangu ya dhana dhanifu kuwa kuna uwezekano na huyu naye pia anadanganywa na amedanganyika!.

Leo nimeisikia tena dhana ya uhaini, ikitajwa mahali!, the voices behind inaniambia anadanganywa na amedanganyika!.
Hii issue ya uhaini nimewahi sio tuu kuizungumzia humu, bali nimeiandikia makala Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo
Humo nilisema Uhaini Tanzania..., My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika?. Mimi ni Tomaso, I Don't Believe This at All!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!.

Nimesema hili sio bandiko la watoto kwasababu natafuta the motives behind such lies ili kumjulisha mtu wetu inawezekana kuwa anadanganywa na watu wake, hivyo kama mtu ukidanganywa na watu wako unaowaaminia bila wewe kujua unadanganywa, ukidanganyika sio kosa lako wewe
unaodanganywa,; kwasababu hao wanaokudanganya ni watu wako unao waaminia, hivyo kudanganyika ni halali yako!, ila kosa ni la hao wanao kudanganya, na siku ukiujua ukweli kuwa ulikuwa unadanganywa, ndipo utaelewa kuwa ni kweli hapa duniani kuna watu na viatu, wengine ukiwaona machoni ni kama watu, lakini mioyoni ni mashetani wakubwa wamwaga damu za watu!.

Hii sio mara ya kwanza kwa hao watu kufanya vitendo na madudu ya ajabu ajabu kisha kudanganya mamlaka juu ku justify udhaoimu wao.

Enzi za Nyerere, alikataa na akawatundika msalabani baadhi yao na kuwafagia toka juu mpaka chini, ndio maana enzi za JPM, tulishauri TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Nyerere aligoma kudanganywa, Mwinyi akadanganywa, Mkapa akadanganywa kwenye ubinafsishaji. Jakaya akadanganywa sana tuu kwenye rasilimali zetu. Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?

JPM mwanzo aligoma kudanganywa na kudanganyika kwenye rasilimali zetu, akakaza, akabana na kukaba, tukauliza humu ataweza? Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? kiukweli JPM alikuwa ni chuma, alikaza, vyuma vikabana, akabana akabana mwisho akaachia!
Mimi ni mtu wa mastori stori, kuna watu wanapenda mastori mastori na wana muda wa kusoma makitu marefu, na kuna wako wako busy hawana time na mastori, wao wanataka vitu short and clear. Wale wa mastori tuendelee, wale wa short and clear, just jump to the conclusion
Baadhi ya matukio ya ajabu ajabu kisha kuvalishwa uongo
Huu uhaini unaoelezwa sasa, ni uhaini wa aina gani?!.

Inawezekana yule Mzee wa watu (Mungu amuweke mahala pema peponi), kwa vile ni mstaafu wa jeshi, anawezekana anahesabika ndiye the strategist, hivyo kuhesabika ni mtu hatari he had to go!. Watekelezaji wakajua tukiharibu sura kwa acid hatatambulika tena!. Mwili umeokotwa Ununio Jumamosi asubuhi, ni polisi wameuchukua na kuu dump mortuary ya hospital ya Mwananyamala. Jumamosi mchana polisi haikutoa taarifa yoyote kuokota mwili wowote, bali Kamanda Musiime alitangaza Jeshi la Polisi kumtafuta huyo Mzee!. Jumamosi usiku ndio ndugu wanautambua mwili!.

Kufuatia kelele nyingi, CinC akatoa amri ya kufanyika uchunguzi wa kina!. Sasa ili kujikosha na kujisafisha, ikabidi itengenezwe script ya movie ya uhaini, ili ku justify kwa CinC why ameshughulikiwa!, wale mnao subiria taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo, endeleeni kusubiria, kama ni wasiojulikana, taarifa itatolewa lakini kama ni 'wasiojulikana', tutasubiri sana kama taarifa ya tukio la pyu pyu za Tundu Lissu!.
Binadamu wote ni sawa, thamani ya uhai wa mtu na roho ya mtu, inalingana, huwezi kumtoa mtu uhai kivile, baada ya kelele za kitaifa na kimataifa, unaamua kutunga script ya uhaini!, na kweli jana CinC kakasirika kweli kweli!, yeye hajui kuwa ni script!.

Huu ni ushuhuda wangu jinsi PT wanavyo bambikia watu kesi mbaya, hawachelewi kubambikia watu uhaini!.
Conclusion
The bottom line ni polisi wetu wana bambika watu kesi mbaya hadi za mauaji!, hivyo hawezi kushindwa kubambika uhaini!.

Hivyo mtu ukihisiwa tuu wewe ni hatari kwa usalama wa the status quo, unabambikiwa kesi, unapotezwa, na sasa hadi uhaini unazungumzwa!.

Kwa vile mimi ni Tomaso, siamini kabisa dhana ya uhaini mpaka tuthibitishiwe!.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Mungu Ibariki Tanganyika.
 
Pascal, hii ndio kazi, na nafasi yako Kwa umma na Dunia ya uandishi
 
Andiko limenikosha sana Pascal Mayalla
Spin doctors wamefanya yao na kaingia mkenge kichwa kichwa.
Punde tutasikia kesi za uhaini ziakazo kwenda mpaka Kwisha uchaguzi mwakani
Mbona sishanghai Musiba kurudi ulingoni ila nashangaa waliomuunda mara ya kwanza bado wapo na wana uwezo wa kumrudisha.
 
Umesema ukweli broo.
Hivi kati ya madaraka na uhai wa binadamu, kipi cha thamani?.
Mungu atusamehe sana.
Lakini mheshimiwa rais(nampenda sana), naomba afumue vikosi vya ulinzi na usalama, hasa jeshi la polisi na TISS.
SIAMINI kama TISS inaundwa na watu intelligent kweli.
 
Waache kutuchezea Watanzania, imetosha sasa, hapa inatafutwa hoja kuzima mambo ya utekaji, mauaji. Tusitolewe nje ya mstari.
Watu wanalalamika hakuna raia ama kikundi kinaweza fanya hayo, linaibuka eti la uhaini. Hebu tuache kucheza na uhai, kisa madaraka. Damu hizi zitarudi kudai haki walizokatishwa kinyama.
 
Hakuna vichwa na kama wapo ni wachache mno na hawapewi nafasi wa kuonyesha weledi wao, ila chawa ndio wanatamba idarani, pia uchu na hofu ya madaraka Kwa huyo mama yataondoa maisha ya wengi,kayumba mno Kwa kauli zake jana
 



Kazi ipo.
 
Mkuu P. Sipo in side ila jini katoka kwenye chupa anaham na dam. Niliandika kwa deep Mh Rais asipo angalia mambo mengi kwa jicho la tatu atajikuta kwenye mkwamo.
Kwa wale tunaona kwa jicho la tatu mpaka la nne tunaona ule wakati unazidi kukaribia. Yapo mambo ni siri sana ila kwa wenye hayo macho waliona siku za mwanzo alipochukua Taifa. Na kwa bahati mbaya alifungua code tena kwenye kikao cha jana akiwaonya wanasiasa juu ya 4R zake.
Jambo kubwa nadhani bado hajalijuwa nikuwa jamuhuri ya wana kusadikika nijamuhuri hatari kuiongoza hasa ukiweka hisia na chuki pasipo shirikisha ubongo. Ikumbukwe wanawake wote wanawndeshwa na hisia lazima hapa awe makini zaidi ama atajikuta kwenye mkwamo binafsi...
Check picha ya Biteko na Majaliwa...
Check picha ya wana siri na mabadiliko ya report line from waziri mkuu to ofisi kuu sijuwi kama unajuwa hathari ya maamuzi haya kwa kiti.....
Anaglia picha lakina makamba vs serikali ya tano na yasita 4R
Anglia picha la kwenye chungu cha pesa na hatima ya uchumi wa wana kusadikika let me funga domo langu. RIP Wazee wa Taifa la kusadikika
 
Inawezekana kweli kuna uhaini unaratibiwa chini chini tusipuuze. Kuna mengi nyuma ya pazia raia hatuyajui.

Nashauri watuhumiwa washughulikiwe kisheria, yaani kufikishwa mahakamani.
Wakikutwa na hatia basi adhabu ya kifo ndipo itekelezwe, isiwe adhabu ya kifo kabla ya kujitetea mahakamani.
Vipi kama mtu katengenezewa
zengwe (kubambikiwa)?

Hatuoni tunaweza kumpoteza mtu ambaye angesaidia kumjua mhaini halisi anaye watumia watu kutekeleza uhaini pengine bila wahusika kujua?

Zingatia Kanusho (Disclaimer):
Sijasema kuna mtu amepewa adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mahakamani.
 
Mkuu embu soma hii kutoka kwa nicola Machiavelli
 
Tomaso! Umeongea vizuri sana uzuri ni kwamba Bi. Mdashi huwa anapita humu kuangazia maoni ya wadau ukiwemo wewe.

Kama atakuwa ameondoa ule ukiziwi wake basi atayafanyia kazi maoni yako, kwa kumalizia huwa naskitika sana kuona anapelekewa washauri ambao kila siku wanamuingiza chaka, na kuwaacha watu kama ninyi kwa sababu ya husda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…