SoC04 Uhakika na Usalama wa Chakula nchini Tanzania

SoC04 Uhakika na Usalama wa Chakula nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 25, 2023
Posts
45
Reaction score
32
Utangulizi

Nazi, Pilipili, Karafuu, Iliki, Uji Lishe, Maziwa, Kisamvu, Mihogo, Mahindi, Mchele, Samaki Wakubwa, Visamaki Vidogo (dagaa na uono), Asali, Sukari, Kuku wa Asili, Nyama ya Ng'ombe Mbuzi na Kondoo, Mayai, Matembele, Mchicha, Machungwa, Mananasi, Maboga, Mboga ya Maboga, Maembe, Tangawizi, Karoti, Nyanya, Chumvi, Mafuta, n.k.

Hivi vyote ni vyakula na viungo vya vyakula japo bado haviishii hapa, kwani orodha ya vyakula na viungo vyake ni ndefu mno. Chakula ili kiweze kuliwa na mwanadamu, ni lazima kipitie hatua kadhaa za maandalizi.

Maandalizi ya chakula ni nini?

Maandalizi ya Chakula ni Utayarishaji wa chakula kwa kupitia hatua kadhaa ili kuhakikisha chakula ni salama na kitamu chenye ladha nzuri inayohitajika kwa matumizi ya mwanadamu.

Maandalizi ya chakula yanatakiwa kuhakikisha kuwa chakula kinachoandaliwa kinaweza kuliwa na mwanadamu yeyote yule pasipo kumsababishia hatari ndogo ya madhara ya papo kwa hapo au hatari kubwa ya madhara baada ya muda mrefu katika afya yake.

Moja kati ya vitu ambavyo vinatugharimu sana watanzania katika ulimwengu wa leo; tuna mvutano wa makundi mawili kuhusu suala na mtazamo wa chakula.

Kundi la kwanza ni kundi la watu wa Pwani ambalo mimi mwenyewe mwandishi wa andiko hili nikiwa mmoja wapo, tukiongozwa na Mzee wetu Mzee Jakaya Mrisho Kikwete. Kundi hili ni la watu ambao tunaamini raha ya chakula ni ladha nzuri na raha ya chakula kiwe kitamu. Kwa mujibu wa Mpishi wa Ikulu kwa awamu tano za Urais, Ndugu Edgard Ndoroma; amewahi kuzungumza kuwa, Mzee Jakaya Kikwete anapenda sana chakula kitamu. Alipokuwa akiona mfululizo wa vyakula vyenye ladha asiyoitaka yeye bali iliyoshauriwa na madakari alikuwa akiwaita wapishi wake na kuwaambia wajiongeze. Kundi hili la kwanza, kutokana na chakula kuwa na ladha nzuri na kitamu, mlaji hufurahia na kula chakula chake mpaka ashibe, japo anaweza kujikuta anakula na kupitiliza kiasi hivyo kusababisha uzito uliopitiliza, magonjwa ya moyo, presha, kisukari, na kadhalika.


View: https://youtu.be/X6nQL9sk2Ho?si=XK4UKW0DifFR3dum

Kundi la pili ni kundi la Madaktari na Wataalam wa Afya; akina Professor Janabi. Kundi hili ni kundi ambalo linaamini kuwa chakula sharti kiwe salama, hivyo hata kama hakina ladha we pambana nacho tu. Kwa mujibu wa aliyekuwa Mpishi wa Ikulu, anaelezea kuhusu namna ambavyo makundi haya mawili yalikuwa yanasababisha huenda wapishi wakune vichwa kwasababu wao ndio walikuwa katikati ya Mzee wetu Mzee Jakaya Kikwete huku Daktari Professor Janabi pia hakuwa nyuma. Katika kundi hili la pili, kutokana na chakula kukosa ladha kwa upungufu wa chumvi, n.k; husababisha walaji wasifurahie chakula chao hivyo hata ulaji hupungua na kupelekea huenda mlaji asishibe sawasawa. Hii huweza kuwa jambo zuri kwa wenye uzito mkubwa sana na wanaotaka kupungua kidogo ili wawe na uzito wenye afya njema, lakini ni hatari kwa wenye kilo za wastani kwani huweza kupelekea changamoto za underweight (udumavu).

Mwandishi wa andiko hili, nimejaribu kuwaza namna ambavyo ingekuwaje kama mimi ningekuwa ni mmoja kati ya wapishi wa Ikulu nyakati za Mzee Jakaya Kikwete?

Jibu nililolipata ni kwamba, ningetumia elimu ndogo ya Kemia niliyoipata nikiwa Kidato cha Kwanza mpaka Kidato cha Nne; kuongeza maarifa ya Kikemia kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Kikemia nchini na duniani kote, kisha ningeongeza na Ujuzi wa Sanaa ya Upishi nilionao; kuanzisha Jiko Kemia ambalo linge - 'balance' mizani ya chakula na viungo vya chakula ili kupika chakula kitamu na chenye ladha nzuri sana lakini pia kilicho salama kisicho na hatari ya presha, kisukari, magonjwa ya moyo, kipindupindu, uzito uliopitiliza, wala magonjwa yoyote ya kuambukiza na yasiyoambukiza.

Jiko Kemia ni matumizi ya Sayansi Kemia jikoni; ambako Sanaa ya Upishi hufanyika. Kumbe basi, Maandalizi ya Chakula yanahitaji Sanaa ya Upishi ili chakula kiwe kitamu na chenye ladha nzuri, pamoja na Sayansi Kemia ili chakula kiwe salama na kinachoweza kuliwa na mwanadamu yeyote yule pasipo kumsababishia hatari ndogo ya madhara ya papo kwa hapo au hatari kubwa ya madhara baada ya muda mrefu katika afya yake.

Hatari ya kutumia Sayansi pekee katika kuandaa chakula ni kuzalisha chakula ambacho ni kizuri kwa afya lakini kisicho na ladha nzuri wala kitamu lakini pia hatari ya kutumia Sanaa pekee katika kuandaa chakula ni kuzalisha chakula ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana lakini kilicho hatari kwa afya.

Ili kuhakikisha Usalama wa Chakula nchini Tanzania na kuepukana na uzito uliopitiliza, uzito pungufu, udumavu, magonjwa ya kuambukiza na magonjwa yasiyoambukiza kama vile kipindupindu, magonjwa ya moyo, kisukari na presha; inatupasa Tanzania kama Taifa kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya yafuatayo:-​

  1. Kuanzisha Kozi Fupi ya 'Kitchen Chemistry' katika Vyuo vya VETA​
  2. Kuanzisha Kozi Fupi ya 'Kitchen Chemistry' katika Vyuo na Hoteli zinazotoa Kozi za Hotel Management na Mapishi.​
  3. Kufadhili Scholarships za Masomo ya Kozi Fupi za Sanaa na Sayansi ya Mapishi ya Vyakula zinazofanana na 'Kitchen Chemistry Short Courses' kwa wapenzi wa Sanaa za Mapishi pamoja na Masomo ya Kemia kwenda kusoma kwenye hoteli za mataifa yanayosifika kwa Vyakula Vitamu na Vyenye Afya Njema; Mfano Japan na New Zealand, kisha kurejea nchini na kuanza kushughulikia changamoto hizo hasa katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe lakini pia taifa zima.​
Umuhimu wa Taifa kuwa na wapishi wenye utaalam wa Kemia ya Jikoni ni;

Vipo vyakula ambavyo vina viambata vya sumu inayoweza kumdhuru mlaji papo hapo au baada ya muda mrefu pasipo kujua. Sumu hizi za vyakula huweza kuwa Cyanide, Sumukuvu na nyinginezo ambazo ni sumu asilia, lakini pia zipo sumu ambazo huweza kutokea kwa kuchanganya vyakula, viungo, n.k. bila kutumia mizani ya kikemia; na sumu hizo ni kama vile cholesterol.

Sumu hizi ndizo zinazoweza kusababisha magonjwa ya moyo, presha, vifo, na kadhalika.

Utaalam wa Kemia ya Jikoni husaidia maandalizi bora ya chakula pamoja na kujua 'meal plan' inayoweza kuokoa bajeti ya chakula kwa kila mtanzania, hivyo kuzisaidia familia zisipike chakula kinachoweza kubaki na kutupwa kama takataka (food waste).

Hitimisho

Hii ndiyo Tanzania Tuitakayo ndani ya miaka 5 mpaka 25. Tanzania ambayo watu wake wana furaha na afya njema. Tanzania ya Jiko Kemia na Tanzania yenye si tu Uhakika wa Kupata Chakula Salama (Food Security) bali pia Tanzania yenye Uhakika wa Kupata Chakula Kitamu na Salama.​
 
Upvote 3
Kabisa, ukivijua vitu vimeundwaje unakuwa na uwanda mpana wa kuvichezesha vilete ladha tamu na bado vilete viinilishe vinavyotakiwa. Jiko kemia, kitu kipya hiki sijawahi sikia🤩
 
Back
Top Bottom