Uhakika wa Ubingwa wa NBC premier league 2021/22 kwa Simba unatokana na nini?

Uhakika wa Ubingwa wa NBC premier league 2021/22 kwa Simba unatokana na nini?

mjogoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
882
Reaction score
652
Nimekuwa nasikia tambo na majigambo toka kwa viongozi, makocha na hata mashabiki wa Simba juu ya uhakika walionao kubeba ubingwa wa NBC premier league msimu huu.

Lakini mimi kwa uelewa wangu ni kwamba NI LAZIMA Yanga apoteze points zaidi ya mchezo wa watani (assuming that Simba will win that match) ndipo Simba atakuwa na uhakika (kama yeye atafanya vizuri).

Sasa ikiwa hivyo ndivyo, na ikiwa timu hizi mbili zitakutana mara moja tu katika raundi ya pili, je uhakika wa Simba kutwaa ubingwa msimu huu unatokana na nini?
 
Hakuna hata uhakika wa Yanga kuchukua, let alone Simba, its not over until its over.... (ingawa kuna high probability ya Yanga kuchukua)

Hayo ni maneno motivational ili wasikate tamaa (huenda hata Yanga wanawaambia watu wao kwamba Bado hatujachukua ndoo ili wasiwe overconfident)
 
Ngoja tuone ingawa kwa moto wa Utopolo msimu huu sidhani kama watapoteza point kuzidi point tatu.
hawa Utopolo a.k.a manyani f.c msimu huu ni wenye bahati kwao.
 
Binafsi ningetamani utopolo wabebe tu..miaka minne mingi sana jamani! Ngoja na wao angalau warudi kwenye ramani.
 
Mkuu, Mimi nikikutqna na mshabiki wa Simba ambao bado notion zao zinawaza ubingwa na kuhisi watabeba... Yaaan sibishani nao, Huwa nawacheka kwa Dharau alafu nawaambia hongereni kwa kubeba kombe mara ya 5 mfululizo.
 
Safi sana
Mkuu, Mimi nikikutqna na mshabiki wa Simba ambao bado notion zao zinawaza ubingwa na kuhisi watabeba... Yaaan sibishani nao, Huwa nawacheka kwa Dharau alafu nawaambia hongereni kwa kubeba kombe mara ya 5 mfululizo.
 
Lkn tusaidiane uelewa. Uhakika wa Simba kubeba ubingwa unatokana na nn hasa?
Binafsi ningetamani utopolo wabebe tu..miaka minne mingi sana jamani! Ngoja na wao angalau warudi kwenye ramani.
 
Ngoja tuone mwendelezo wa Simba SC kwa round hii ya pili, akikwaa kisiki tu na Yanga ikaendelea na wimbwi la ushindi basi tena..!
 
Lkn tusaidiane uelewa. Uhakika wa Simba kubeba ubingwa unatokana na nn hasa?
Kwenye soka lolote linaweza kutokea..Yanga anaweza kuflop simba akatake advantage..lkn kiuhalisia tayari bingwa alishapatikana tangu msimu unaanza kinachoendelea sasa hv ni ushahidi tu wa kukamilisha ratiba.
 
Maneno yatakayotamba baada ya ligi kuisha:TIMU YENYEWE IMEKAA MIAKA MINNE BILA UBINGWA TUMEWAACHIA TU
Na mkikosea mwaka huu msiwe Mabingwa, wallah kuna watu watazimia...!
 
Sababu za Simba kuamini watatwaa ubingwa ni hizi....

1. Mara nyingi Yanga huwa wana rekodi nzuri katika mzunguko wa kwanza na kupotea katika mzunguko wa pili.

2. Simba wanaamini kwa uhakika watapata point tatu katika mechi yao dhidi ya Yanga.

3. Soka la Tanzania kwa sehemu kubwa limefichwa katika kichaka cha rushwa, upendeleo, ujanja ujanja na ushirikina. Hizo ndio siri za mafanikio baina ya Simba na Yanga hususani ushindani unapokuwa mkali.
 
We Ngoja Tupige KMC Tupige Na Azam Na Mayele Atupie Mechi Zote Izo Kama Kawaida Yake...Af Tukutane Iyo 30 April Tuwape Jibu Kamili Kwanini Tunasema Sisi Ni Mabingwa Msimu Huu.
hata Mayele mwenyewe hajui km atafunga sembuse kuchukua ubingwa.

Ila mashabiki bhana utafikiri wao ndiyo watacheza hizo mechi, kumbe wanasubiri wachezaji wacheze.
 
Back
Top Bottom