Uhakiki wa Wanachama Chama Kipya Cha Siasa 1993

Uhakiki wa Wanachama Chama Kipya Cha Siasa 1993

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WANACHAMA WA CHAMA KIPYA CHA SIASA WAMEKUJA KUHAKIKIWA NA MSAJILI WA VYAMA ARNAUTOGLO HALL 1993

Asubuhi na mapema tulikuwa tumeshafika Ukumbi wa Arnautoglo tumekuja kuhakikiwa kwa ajili ya chama chetu kipya cha siasa.

Ukumbi huu una historia kubwa sana katika siasa za kudai uhuru wa Tanganyika na katika historia ya Julius Nyerere.

Tarehe 17 April 1953 kwenye ukumbi huu ndipo Nyerere alikabidhiwa chama cha TAA baada ya ''kumshinda'' Abdul Sykes katika uchaguzi wa kugombea nafasi ya President wa TAA.

Wanachama kutoka sehemu tofauti za Dar-es-Salaam kuanzia Buguruni Kwa Mnyamani, Manzese Uzuri, Tandika, Temeke, Mbagala tumefika tumejikusanya nje ya ukumbi.

Maofisa wa Ofisi ya Msajili wamefika jua limepanda kidogo wametukuta tunawasubiri.

Niko pembeni na camera yangu naangalia yote yaliyoko pale.
Kwa mbali nikamuona Mzee Lumelezi anapita na shughuli zake.

Ukoo wa Lumelezi ni ukoo maarufu sana Dar-es-Salaam.

Mzee Lumelezi, Mzee Mavemba, Ally Sykes hawa wote mchezo mmoja na baba yangu na shule yao Al Jamiatul Islamiyya Muslim School Mwalimu Mkuu Sheikh Juma Mwindadi.

Nikamkimbilia kumwamkia.

Akaitikia salamu yangu lakini nikahisi kama vile anajiuliza hapa pana nini?

Sikusubiri aniulize nikamwambia, "Baba tumesajili chama cha siasa leo tunahakikiwa."

Siku hizo kuwa wewe si mwanachama wa CCM ilionekana kama usaliti vile.
Sasa mimi namtangazia hali ya hatari.

Niliona uso wa mzee wangu ukiporomoka kama vile kusema, "Mtoto ana kiranga huyu."

Mzee Lumelezi kainamisha kichwa chini hasemi kitu. Tukaagana.

Lakini Mzee Lumelezi si mjinga kayaona yote kwa macho yake. Kawaona waliotutangulia sisi na ndiyo wao na kashuhudia yote yaliyowafika.

Alikuwa kastaafu kazi Dar es Salaam City Council. Hawakupata chochote TANU ilichowaahidi.

Watoto wao wamesoma sana darasa la la 12 lakini kawaida wanamaliza darasa la saba ndiyo mwisho wao.

Alikuwa kwa ule ukimya wake ananiambia, "Tumeshindwa sisi mtaweza nyie?"

Maofisa wa Msajili wa Vyama Vya Siasa walikuwa hawajaona watu sampuli yetu.

Kwanza tuliokuwa pale umasikini wetu ulionekana dhahir haukujificha.
Nguo zetu zilitutangaza vizuri sina haja ya kusema mengine ila moja.

Sote wanachama tuliokuja kuhakikiwa tulikuwa Waislam watupu.

Nimekuwekeeni picha mfaidi kwani picha inasema maneno 1000 na picha inaonyesha kile jicho kiliona.

Maofisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kutuangalia wakawa tayari wameshakasirika.

Nyuso zao wamezikunja hawana tabasamu.

Leo naangalia nyuma nacheka na nashangazwa na ule ujasiri wetu kuwa sisi masikini ya Mungu tunasajili chama kije kushindana na Chama cha Mapinduzi, chama tajiri kilichokuwa na kila kitu achilia mbali kuwa kina serikali.

Kisa cha Daud na Jalut.

Jalut anajivuna kwa nguvu zake na uwezo wake wa kumuua kila aliyethubutu kukabiliananae kwenye uwanja wa mapambano.

Daud alipokuwa anakwenda kumkabili Jalut aliomba dua Allah amthibitishie miguu yake ardhini amkabili Jalut.

Chama chetu kilinyimwa usajili.
Lakini huo haukuwa mwisho wetu.

Tuliyokuja kufanya si tu yalimstaajabisha Mzee Lumelezi bali hata sisi wenyewe.

Nimeweka na picha ya mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Ghandhi Hindu Mandal mwaka wa 1955.

Fananisha picha hii na picha yetu.

334694252_1614180729102052_5833874265695232266_n.jpg

334709390_1352858755287545_2739443264799295865_n.jpg

330781784_621910456438604_3313645283185321560_n.jpg

334702773_146974518262849_5958340362266701242_n.jpg

331795436_147118884905105_1199791197814951944_n.jpg

 
Kilikuwa chama au baraza la Ulamaa.
 
Kilikuwa chama au baraza la Ulamaa.
Ngongo,
Kuna picha ya Mwalimu Nyerere mwaka 1957 kapiga na Baraza la Wazee wa TANU ni picha maarufu.

1678282862708.jpeg

Je, tubadili caption badala ya Baraza la Wazee wa TANU tuandike Baraza la Ulamaa?

Hii hapa chini nayo unaipa jina gani?
1678282999428.png


Hii picha ilipigwa mwezi Februari 1955 safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO na hafla ya kumuaga ilifanyika Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) hao akina mama wanamsindikiza Nyerere Uwanja wa Ndege Dar es Salaam.
 

Attachments

  • 1678283007210.png
    1678283007210.png
    1.8 MB · Views: 8
Back
Top Bottom