Uhalali wa CCM kumiliki viwanja vya michezo

ccm na uporaji, wizi, ufisadi, uhujumu uchumi, uchawi, utekaji, mauaji, na kila aina ya uovu; havitenganishiki.
 
Kuna viwanja na majengo ambavyo kiuhalali sio mali ya ccm hata kdg!
viwanja kama Kirumba na majengo kibao yalitakiwa kurudi serikali kwani yalijengwa kwa raslimali za |Taifa na sio chama!
Ila siku zaja mali zote zitarudi na ccm ndio watajua kuwa maharage ni mboga au futari
 
Mkuu kwa vile gharama za harusi yako na kitanda unacholalia wewe na mme/mkeo vilitokana na michango chini ya kamati ya harusi kwa hiyo mme/mke ni wa watu wote walichanga?

Nyumba au viwanja vinajengwa kwa mawe- nyie CHADEMA mnahamasisha watu wasombe mawe ya kupopoa polisi; CHADEMA badala ya kuhamasisha watu wajenge viwanja mnahamasisha watu waandame, waache kutumia mtandao wa TIGO kisa uliibua UGAIDI wa Mbowe.

Sikiliza tunataka kuona CHADEMA Mkolani ikiwa sambamba na CCM Kirumba badala ya mawazo ya kijinga unayopendekeza. Ni bora ueleweshe mapema kuwa hizo ni mali za CCM kisheria. Hii haizuii kutaifishwa ila lazima fidia itolewe ikiaamanisha kuwa CCM itapata hela zaidi
 
Ukarabati huo wananchi wote wa Arusha tulilazimishwa kuchanngia hiyo CCM haikutoa hata senti moja.
Jukwa la kaskazini lilijengwa na hayati Phillip Olotu kwa fedha na ufundi wake
Haya majizi tuu
 
Kama kuna jambo linalokera sana ni pale viwanja vilivyokuwa vya umma kabla ya mfumo wa vyama vingi kuporwa na CCM ambayo imeshindwa kuviendeleza. Inaonekana kama wangekuwa na uwezo walitaka hata jengo la Ikulu liwe la CCM.

Natoa hoja kuwa viwanja vyote ambavyo vilikuwa vya umma kabla ya mfumo wa vyama vingi virudiswhe serikalini kama ilivyo uwanja wa Uhuru.

Mkwakwani, Amri Abeid, Kirumba, Ali Hassan Mwinyi, Nelson Mandela, Samora na vingine vingi virudishwe serikali mara moja; havikujengwa na CCM bali vilijengwa na wananchi wote. Uwanja wa Mkwakwani umekuwapo tangu wakati wa Ukoloni; uwanja wa Amri Abeid ulijengwa kabla hata CCM haijazaliwa; na hata vile vilivyojengwa baada ya CCM havikuwa vimejengwa kama vitega uchumi vya CCM bali vilijengwa kama viwanja vya burudani kwa wanachi wote.

Sijui kama nimeeleweka.
 
Naunga mkono hoja 100% ila hili suala ni gumu kutekelezwa bila msukumo wa kisheria na kijamii. Lakini una uhakika viwanja vyote ulivyotaja vilirudishwa serikalini? Mbona bado Kirumba unaitwa CCM Kirumba? Kuna ule wa CCM Liti upo Singida. Na serikali inapeleka fedha za umma kuviboresha.
 
hukunielewa
 
Itakavyobadilisha ni either katiba mpya au chama kingine Kishinev hatamu
 
Ccm lazima itaondoshwa kwenye hivyo viwanja na baada ya hapo lazima wataburuzwa mahakamani ili walipe damages kwa muda wote ambao wamevitumia hivyo viwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…