Uhalali wa OFM ya Shigongo

Uhalali wa OFM ya Shigongo

Captain Phillip

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
894
Reaction score
538
Learned Brothers,

Ni kwa muda sasa nimekuwa nikiona udhalilishaji wa wazi wazi ukiendelea na kudakwa na magazeti pendwa kwa wingi ili kuuza na kujipatia fedha bila kujali damage inayoachwa kwa wahusika.Kuna hii kitu inayojiita OFM(oparesheni Fichua Maovu) ambayo inaendeshwa na Magazeti ya Shigongo kwa kushirikiana na polisi hasa wa Kinondoni.Ni mara kadhaa wamekwenda kuvamia watu walio faragha na kuwapiga picha ili kuuza magazeti japo huwa hatusomi ni nini kimeendelea baada ya watu hao kukamatwa.

Hoja yangu hapa ni kuwa hii oparesheni ni kwa faida ya nani na inamfaidisha nani in a free country na pale vyombo vya dola vinapotumika kwenda kukamata watu walio faragha labda tu kwa hisia kuwa huyu ni mke au mume wa mtu?Sijawahi kusoma popote pale kuona kama wanaoripoti kesi waliombwa vithibitisho kama cheti cha ndoa au cha kuzaliwa pale mzazi au spouse anapohusishwa.

Brothers kuna uhalali gani kwenye opareshi hii mbali na udhalilishaji?
 
Mi naelewa kwa mtu ambae anachapiwa mke wake
ila kama ni mchumba sijui msanii wa bongo, askari feki, dokta feki... haileti maana cz tuna Waandishi wa Habari feki na hakuna hata mmoja aliyefichuliwa. Maybe wangeanza na Waandishi wa Habari, Watoza Ushuru, Wala Rushwa na wale wachungaji wanaolala na kondoo wao
 
Uko on point mkuu ninaamini nguvu inayotumika hapo ingetumika kuwaweka wazi wanaoua tembo wetu na waingizaji na wauzaji wa madawa ya kulevya kuwaweka front pages angalau ingeleta maana.Tatizo ni Watz wa leo kukomali mabo yasiyo ya muhimu wakati watu wanapiga dili za mabilioni na bado wanaita ni vihela vya Ugoro
 
Ngoja siku waingie mtegoni na kutoa picha za aina hiyo na habari ambayo ni uongo kisha watu waweke wanasheria makini kama hiyo Global haijafilisiwa. Shigongo anatengeneza pesa kiujanja ujanja sana bila kujali kama kuna maumivu upande wa pili.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mkuu uko sawa sana...mimi mwenyewe kufikia kusema haya nimesikia mtu anamtishia mwenzake kuwa atamuitia OFM.Hawana mechanism za kufanya investigation achilia mbali mandate ya kufanya hivyo .But nani anafaidika hapa hasa pale tunapoona vyombo vya dola(Polisi) wakitumika?
 
Kaka yamekukuta nini? Udaku ulikuwepo tokea enzi za Agano la Kale....Kasome biblia!
 
hapo watu wako kibiashara zaidi, polisi na shigongo, kila mtu anakula kivyake.
 
Hawa OFM hawajitambui wanafanya mambo ya kitoto sana na cha kushangaza polisi wanashiriki utoto huo.
 
Back
Top Bottom