Uhalifu 2023: Zanzibar yaongoza ubakaji, Arusha yaongoza ulawiti

Uhalifu 2023: Zanzibar yaongoza ubakaji, Arusha yaongoza ulawiti

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Ripoti mpya kuhusu hali ya uhalifu nchini Tanzania imebaini ongezeko kubwa la kesi za ubakaji na ulawiti, ambapo mikoa ya Zanzibar, Arusha, na Morogoro inaongoza kwa kiwango kikubwa.

Ripoti hiyo, inayoshughulikia takwimu kutoka Januari hadi Desemba 2023 pia inaonesha kwamba Mjini Magharibi ya Zanzibar pia iko kati ya mikoa mitatu yenye kiwango cha juu cha ubakaji na ulawiti.

Ubakaji+ulawiti.jpg

Ubakaji na ulawiti uliongeza kiwango cha kutia wasiwasi 2023​

Mikoa yenye kesi nyingi za ubakaji nchini Tanzania:
  1. Zanzibar Urban West: 564
  2. Morogoro: 525
  3. Tanga: 519
  4. Kinondoni: 506
  5. Mbeya: 406
  6. Dodoma: 399
Mikoa yenye kesi nyingi za Ulawiti:
  1. Arusha: 251
  2. Zanzibar Urban West: 225
  3. Kinondoni: 210
  4. Kilimanjaro: 154
Kwa jumla, Tanzania iliripoti kesi 8,691 za ubakaji na kesi 2,488 za ulawiti mwaka 2023. Takwimu hizi zinaonyesha hali mbaya ya usalama na ulinzi kwa watu walioko hatarini, hasa wanawake na watoto, katika mikoa mbalimbali.

Chanzo: The Citizen
 
Ulawiti ubakaji

Zanzibar Urban west 564
Tanga 516


Hili nalo mkalitazame
 
Hatari mno. Kwa Zanzibar sishangai, Jamaa wanapenda kufirqna sana.
 

kule ukila mwanfunzi wa sekondari ni kesi kubwa, na unawindwa kabisa na ndio inaitwa ubakaji. wakati nipo hapa shinyanga mwezi sasa naona watu wanavyokata vichwa vya wanafunzi mpaka wa msingi kinoma ila linachukuliwa jambo la kawaida. Zenj ukishangaa nae mtaani tu unaweza kujikuta ndani.
 
Hatari mno. Kwa Zanzibar sishangai, Jamaa wanapenda kufirqna sana.
Hujashangaa Arusha kuongoza kundi la walawiti ila Zanzibar ambayo iko namba 2 ndiyo uliyoiona.
Arusha inatafakarisha.
 
Ulawiti ubakaji

Zanzibar Urban west 564
Tanga 516


Hili nalo mkalitazame
Arusha imeongonza kundi kwenye kesi za ulawiti, 251.
Zanzibar, Morogoro na Tanga zimeongoza kwenye kesi za kubaka.
Wakati mikoa hiyo yenye watu wachache inaongoza kitaifa kwenye kesi za uhalifu wa kingono Dar yenye idadi kubwa ya watu haimo.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Hujashangaa Arusha kuongoza kundi la walawiti ila Zanzibar ambayo iko namba 2 ndiyo uliyoiona.
Arusha inatafakarisha.
Kwa population yao, Zanzibar imetisha. Wangeweka matukio hayo kwa asilimia ya watu waliopo, ungekuta Zanzibar kila kaya ina mtu mwenye kesi
 
Zanzibar = Utalii
Arusha = Utalii

Je, kuna uhusiano kati ya utalii na matukio hayo?
 
Kwa population yao, Zanzibar imetisha. Wangeweka matukio hayo kwa asilimia ya watu waliopo, ungekuta Zanzibar kila kaya ina mtu mwenye kesi
Ni kweli, lakini muda mrefu matukio ya aina hiyo yalikuwa maarufu sana kwenye miji ya Pwani.
Dar es salaam, Zanzibar, Tanga na Mombasa, lakini sasa miji ya Arusha na Moshi nao hawataki kuachwa nyuma.
Arusha wapo namba moja Kilimanjaro wako namba 4.
Hali ni mbaya sana Kaskazini.
 
Back
Top Bottom