Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Serikali nchini Tanzania imeamua kuunda kikosi Kazi maalum cha kufuatilia makosa yote ya uhalifu mtandaoni, baada ya kufanyika mkutano wa wadau wa mawasiliano Jana novemba 22 mwaka 2024.
Mkutano ulifanyika makao makuu ya mawasiliano Tanzania (Tcra) , Dar es salaam ukihudhuriwa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa habari mawasiliano na Teknolojia ya habari Jerry Silaa Pamoja na wadau wa mawasiliano na wawakilishi wa kampuni za simu.
Kikosi Kazi hicho kitahusisha wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za serikali na wizara husika kuweza kushughulikia changamoto za uhalifu wa mitandaoni kwa ufanisi zaidi alisema mhandisi Masauni.
Makosa mbalimbali kama vile
• miamala mbalimbali ya kieletroniki
• wizi wa aina yoyote mtandaoni
• simu za utapeli au sms za utapeli nk.
Waziri Silaa naye alisisitiza " umuhimu wa ushirikiano wa karibu baina ya serikalini, kampuni za simu na sekta binafsi Pamoja na wadau mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mtandaoni ambavyo vimeendelea kuwa tishio kwa usalama wa nchi.
Ukiona ujumbe wowote wa utapeli ripoti kupitia namba hii 15040.