The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,092
Hapo kila mtu atasema anataka kurudi miaka kadhaa nyumaJana nlianzisha thread kuuliza wale ambao bado hawajoa/olewa kama wangependa kufanya hivyo mbeleni na kama ni ndio au sio kwanini??!
Majibu niliyopata yalikua yanatofautiana kwanzia waonataka kuwa na watu wa kushea nao maisha....mpaka wanaotaka kupendeza tu siku ya harusi na wa wanaotaka security!!
Nikajikuta najiuliza kwa wale ambao wapo kwenye ndoa je nini kilichowashawishi na je walipata yote waliyotarajia na kutamani kuyapata
kwenye ndoa???!
Kwahiyo naomba niwaulize kwa faida ya wale wote tuliopo nje...
...Je wewe ulitaka/kubali kuoa/olewa kwasababu gani??!
...Baada ya kuingia mambo yalikua kama ulivyotarajia!?
...Kama mambo yalikua tofauti na matarajio yako je ni kwa uzuri au kwa ubaya???!
...Umewahi kujuatua au kushukuru Mungu kumchagua uliyemchagua???!
...Ungepata nafasi ya kurudi miaka kadhaa nyuma mpaka ulipokua unaamua kufungwa pingu za maisha ukiwa inajua kila kitakachotokea mbeleni ungefanya uamuzi tofauti na uliofanya???
Please tupeni experince tujifunze kabla hatujaingia huko na matarajio kibao alafu tushindwe kuvumilia hali halisi!