Kila ndoa ina tofautiana. Haimanaanisha kama ya fulani ina furaha na yako ikawa na furaha, na haimaanishi kama ya mtu fulani ina matatizo na yako ikawa na matatizo
Siku hizi watu wanaogopa sana ndoa kutokana na story za watu lakini muhimu ni wewe binafsi je unataka kuolewa kwa nini?
Ukishajiuliza hayo maswali na kama majibu yake yote unaweza kuyatimiza nje ya ndoa basi kaa hapo hapo ulipo kama unaona kuna furaha na kama kweli unaogopa sana mitihani ya ndoa.
Kama unataka kingia kwenye ndoa tafuta mtu ambaye naye yuko tayari kuingia kwenye ndoa na mjuane vizuri kwani tabia za huko ndio mtakazo ziamishia kwenye ndoa.na hakikisha swala la kuwa na watoto wote muwe tayai na mjadili mitihani inayokuja baada kupa mtoto.
Jinsi ulivyo uliza maswali majibu yote ni tofauti kwani watu tunatofautiana, vizuri kujaribu kama una mtu umeridhika nae na unaona na yeye yuko tayari. Au kama unaona moyo wako una wasi wasi sana basi achana na ndoa ,lakini kwa kifupi kuwa na ndoa yenye furah utahitaji ushirikiano wa pamoja kutoka kwa partner wako na sio juhudi zako binafsi.
Kila la kheri na Mungu akujalie ufanya maamuzi sahihi.