Jamani hayaotokeo ni ishara kidogo za uozo tuliojijengea wenyewe huku tukicheka kama MAZUZU! Nanukuu sehemu ya mchango niliouona kwenye fb leo na hakika ndiyo hali halisi japo kwa mtazamo wangu. "yu na kheri mwenye kumbukumbu! Vitu vingi vinachangia hali hii ya matokeo. Kwanza serikali. Mitaala imeharibiwa makusudi, walimu hawana sifa za kuwa walimu - wakiandaliwa walimu VODA FASTA wote mnakumbuka - waliokuwa wamefeli vibaya kidato cha 4 walipelekwa vyuo vya ualimu kwa miezi sita kisha wakaanza kufundisha sekondari-tutegemee nini? Wote tuliona na tukayafumbia macho na wenhine tulifurahia sana kwa kuwa watoto wetu, ndg zetu amba walikuwa hatujui pa kuwapeleka walipata vyeti vya ualimu na kazi. Serikali ilianzisha shule nyingi za kata ili kupata sifa na uhalali wa kisiasa - zilikuwa ni majengo ambayo hayakuwa na sifa hata moja ya kuitwa shule - nayo tuliyakubali kijinga au kinafiki! Serikali haiwajali tena walimu, nao wakaamua kutokujali kazi. - bora mshahara unaingia hata kama unachelewa miezi sita - LIWALO NA LIWE! Pili ni sisi ndg na wazazi wa hawa watoto kamwe hatutahepa lawama - hatuna muda na watoto wetu, tumemwachia mwalimu dunia atuandalie na kutulelea watoto, tunawanunulia watoto simu na ipads tukijidanganya kuwa tunawapenda. Asilimia 90 ya uda wao wa shuleni na hata nyumbani wanatumia kuandika texts hata kwa wapenzi (who knows and who cares?), wapo kwenye hizi social networks - fb, whatsap, na nyingine nyingi - social networks ni mwizi mkubwa wa muda kwa mtu asiye makini. Wote tunafahamu hilo. Nyumba na hata kwa majira, kwenye mabaa wstoto wetu nashinda na kukesha kuangalia mipira ya timu za ulaya (wazifahamu hata kuliko kuandika orodha ya 2), wangaangalia picha hizi wanazoita wenyewe series! Hizi tv zetu tunajua wanachoonesha, ni uharibifu zaidi kuliko kujenga, tunategemea miujiza? Tatu ni watoto wenyewe - hawajitambui na hawana malengo. Wamejitoa fahamu na wananata kuliko wakati kichwani ni watupu, wanasema uongo hadi wanajidanganya wenyewe! Kudanganya ni vibaya sana lakini kujidanganya mwenyewe ni kifo cha utu na nafsi. . . .na wote tunajua matokeo yake. Siasa zetu za kishabiki na kipuuzi za kushabikia upuuzi na kuacha ukweli ukipotelea mawinguni, tunategemea nini. . . ! ! !?" mwisho wa nukuu. Hivi tunaweza kuyatatua hayo matatizo kwa mkupuo mmoja? Tutafakari!