Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

CCM HAWAELEWI, KWENYE NCHI YOYOTE ILE UNAPOGOMBANA NA WAALIMU NA MADAKTARI UJUE KILA KITU KIMEISHA, NA PIA SERIKALI YA CCM IKUMBUKE KUWA UALIMU SIO KUFIKA OFISINI NA KUCHUKUA CHAKI NA KUANDIKA UBAONI BALI NI SAMETHING WITHIN DA HEART AND IT CAN NOT BE FORCED BY EXTERNAL PRESSURE SUCH COURT, GVT, INSPECTORS etc, HAPA ILIKUOKOA JAHAZI NI SERIKALI YA MAGAMBA IKAE NA VIONGOZO WA WAALIMU NA KUTEKELEZA HATA 3/4 YA MADAI YA WAALIMU THEN WAANGALIE MAMBO YATAKAVYOKUWA
 
Sisi wazazi ndio tulioumia maana kwa kuwapeleka hao watoto 240,000 waliopata zero ni ishu. Na kwa serikali hii iliyoshindwa hata kutupatia maji sidhani kama itajali kuhusu hatima ya hawa watoto.
 
huu msiba wa kitaifa

ikiwezekana bendera ipepee nusu mlingoti kwa siku 30 huku tukijitafakari kama taifa ni wapi tulipojikwaa,kwasababu hii si changamoto tena hili ni tatizo,lazima tuweke siasa pembeni na kusemezana kama taifa kwasababu taifa linaangamia mbele ya macho yetu.
 
Jamani hayaotokeo ni ishara kidogo za uozo tuliojijengea wenyewe huku tukicheka kama MAZUZU! Nanukuu sehemu ya mchango niliouona kwenye fb leo na hakika ndiyo hali halisi japo kwa mtazamo wangu. "yu na kheri mwenye kumbukumbu! Vitu vingi vinachangia hali hii ya matokeo. Kwanza serikali. Mitaala imeharibiwa makusudi, walimu hawana sifa za kuwa walimu - wakiandaliwa walimu VODA FASTA wote mnakumbuka - waliokuwa wamefeli vibaya kidato cha 4 walipelekwa vyuo vya ualimu kwa miezi sita kisha wakaanza kufundisha sekondari-tutegemee nini? Wote tuliona na tukayafumbia macho na wenhine tulifurahia sana kwa kuwa watoto wetu, ndg zetu amba walikuwa hatujui pa kuwapeleka walipata vyeti vya ualimu na kazi. Serikali ilianzisha shule nyingi za kata ili kupata sifa na uhalali wa kisiasa - zilikuwa ni majengo ambayo hayakuwa na sifa hata moja ya kuitwa shule - nayo tuliyakubali kijinga au kinafiki! Serikali haiwajali tena walimu, nao wakaamua kutokujali kazi. - bora mshahara unaingia hata kama unachelewa miezi sita - LIWALO NA LIWE! Pili ni sisi ndg na wazazi wa hawa watoto kamwe hatutahepa lawama - hatuna muda na watoto wetu, tumemwachia mwalimu dunia atuandalie na kutulelea watoto, tunawanunulia watoto simu na ipads tukijidanganya kuwa tunawapenda. Asilimia 90 ya uda wao wa shuleni na hata nyumbani wanatumia kuandika texts hata kwa wapenzi (who knows and who cares?), wapo kwenye hizi social networks - fb, whatsap, na nyingine nyingi - social networks ni mwizi mkubwa wa muda kwa mtu asiye makini. Wote tunafahamu hilo. Nyumba na hata kwa majira, kwenye mabaa wstoto wetu nashinda na kukesha kuangalia mipira ya timu za ulaya (wazifahamu hata kuliko kuandika orodha ya 2), wangaangalia picha hizi wanazoita wenyewe series! Hizi tv zetu tunajua wanachoonesha, ni uharibifu zaidi kuliko kujenga, tunategemea miujiza? Tatu ni watoto wenyewe - hawajitambui na hawana malengo. Wamejitoa fahamu na wananata kuliko wakati kichwani ni watupu, wanasema uongo hadi wanajidanganya wenyewe! Kudanganya ni vibaya sana lakini kujidanganya mwenyewe ni kifo cha utu na nafsi. . . .na wote tunajua matokeo yake. Siasa zetu za kishabiki na kipuuzi za kushabikia upuuzi na kuacha ukweli ukipotelea mawinguni, tunategemea nini. . . ! ! !?" mwisho wa nukuu. Hivi tunaweza kuyatatua hayo matatizo kwa mkupuo mmoja? Tutafakari!
 
ili shule za kata ziweze kufaulisha yafuatayo inabidi yazingatiwe:
  1. kupatia walimu mazingira mazuri ya ufundishaji ambayo ni vitabu, maabara,na mitaala maalum
  2. kuweka mshahara mzuri kwa walimu.
  3. wanafunzi kujitambua na kufanya yale walio yafuata shule.
  4. serikali iache kuchukulia swala la elimu kwa kisiasa.
 
ili shule za kata ziweze kufaulisha yafuatayo inabidi yazingatiwe:
  1. kupatia walimu mazingira mazuri ya ufundishaji ambayo ni vitabu, maabara,na mitaala maalum
  2. kuweka mshahara mzuri kwa walimu.
  3. wanafunzi kujitambua na kufanya yale walio yafuata shule.
  4. serikali iache kuchukulia swala la elimu kwa kisiasa.
 
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa
Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Daraja ; Idadi ya Wavulana; Idadi ya Wasichana
I. 1,073 568
II. 4,456 1,997
III. 10,813 4,613
I-III 16,342 7,178
IV 64,344 38,983
0 120,664 120,239
 
Huu mtihani urudiwe....aiwezekani awa wote watoto ni wajinga kias icho........mbaya zaid waziri bdo yupo salama kwenye kiti chake
 
KWELI SERIKALI ILIWAONA WALIMU NI PUNDA IKAWALAZIMISHA KWENDA MTONI KAMA KAWAIDA HAWAKUNYWA MAJI KWA HASIRA ZA KULAZIMISHIWA KUNYWA MAJI BILA KULA MAJANI.,Matokeo yake ndo haya,aibu kwa wote waliosimama upande wa serikali kwenye migomo ile.
 
Chenji ya rada iliyorudishwa toka Uingereza imeenda wapi kwani iliamuliwa kwamba ingetumika kwa hayo yaliyoorodheshwa.
 
ukichanganya na wliopata Four ambao pia wamefeli ingawaje CCM inaona wamefaulu kati ya asilimia 75 mpka 80 wamefeli mwaka huu.Tanzania inaangamia
 
Duuh hii ni aibu,au shule za kata zimechangia?Walimu wangekuwa wanalipwa vizuri mambo yangekuwa tofauti,kuna walimu nawafahamu walikuwa shule nzuri za hapa Tz,wote wamehamia shule zingine za private na wengine wanafundisha vyuo(wamejiendeleza ).Sasa hii baada ya miaka kumi jamii itakuwaje?

Serikali muongeze mishahara ya walimu ili walau wabaki kwenye fani hiyo,wengi wanaikimbia maslahi hakuna.Walimu kibao sasa wanasoma wauhame ualimu,matokeo yake matayaona in 10 years to come.
Ila na wanafunzi wa siku hizi kutwa facebook,twitter,jf,Tv shows na series(kila kipindi cha Tv wanaangalia) hata kusoma hawana muda.Maisha nayo tight wazazi busy hata muda wa kuwafuatilia watoto haupo.
 
Huu mtihani urudiwe....aiwezekani awa wote watoto ni wajinga kias icho........mbaya zaid waziri bdo yupo salama kwenye kiti chake

Watoe hayo makaratasi yasaishwe tena, nadhani necta wanatatizo.
 
ukichanganya na wliopata Four ambao pia wamefeli ingawaje CCM inaona wamefaulu kati ya asilimia 75 mpka 80 wamefeli mwaka huu.Tanzania inaangamia

Serikali inawaangamiza vijana!! wanasema haya yatapita tu!! maccm bana!
 
Toka nipate akili na kusoma historia ya Tanganyika toka ipate uhuru mwaka 1961, Sijawahi ona matokea mabaya ya form 4 kama haya. Nadhani inabidi yaingie kwenye kumbukumbu ya Majanga mabaya yaliyo wahi kutokea Tanzania toka tupate uhuru.
Kawambwa kama viongozi wa zamani wasingesimamia taaluma enzi hizo sidhani wewe kama leo ungekuwa na PhD. Kikwete na viongozi wengine wote kumbukeni mlipitia mfumo mzuri wa taaluma ndiyo maana leo hii mnatunyanyasha Wa-Tanganyika.
Ndugu zangu waalimu nguvu zenu tumeziona, maana haya ni matunda ya Mgomo wa kimyakimya ambao najua bado mnauendeleza maana serikali haijawatekelezea madai yenu. Sasa bandugu waalimu waoneeni huruma watoto wa watanzania wenzenu.
Hivi wabunge wetu tuliowachagua mna kauli gani kuhusu haya matokeo?
Inauma sana, inatia uchungu sana, inakera sana.
 
ni kilio kila sehemu, tulivyotegemea sivyo kabisa
 
Kilimo kwanza elimu baadae boss kama vipi badilisha chama iliyoko madarakani
 
Back
Top Bottom