1.Huwezi kumjua Mungu na Yesu Bila kujijua wewe mwenyewe bwana John Q upoje! kwasababu Biblia imesema wazi Mwanzo 1:26,Mungu alikuwa anasemezana na kitu kingine na kukubaliana "na TUMFANYE mtu kwa mfano Wetu"! angekuwa pekeyake asingesema "Tumfanye" angesema "nifanye" hapo katumia wingi na sio umoja! sasa kujua Mungu alikuwa anasema na nani inatakiwa tumjue huyo mtu aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake ndio tutapata picha ya huyo aliyekuwa anasema naye hapo awali namna ya kumuumba mtu kwa mfano wao!
Namna Mtu alivyo, hapa nitatumia mfano wako mwenyewe, Wewe kama John i mean mtu John upo katika sehem tatu,Una Roho (binadamu woote wana Roho),una Mwili na pia una Nafsi soma Warumi 8:23 Na 2 Wakorintho 7:1, sasa Roho Hukaa ndani ya Nafsi (matendo 20:28,waebrania 4:12) na kwapamoja nafsi na roho hukaa ndani ya mwili ndio unakuwa wewe bwana John-Q,sasa wewe John Q una vitu vitatu una mwili ndio huo unao uona na ndani yako una roho na nafsi na ukitizama kwa makini huwa wakati mwingine mnabishana na hivyo viwili vilivyopo ndani yako,mwili wako unaweza ukawa unatamani kufanya jambo fulani lakini roho haipo tayari! au kinyume chake,mwili ni dhaifu siku zoote lakini sio roho (soma Mathayo 26:41) sasa tunaposema mtu kafariki ni pale Nafsi na roho vinauacha Mwili vinatengana ule mwili unabaki pekeyake hapa Duniani ukirudi mavumbini roho ndio inatangulia huko mbele kwenda kwenye hukumu,ndiomaana Biblia inasema tusijitaabishe na vya mwilini! mwisho wa siku tutaviacha!
Kwahiyo binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu ana hivyo vitu vitatu Roho,Nafsi na Mwili so na Mungu naye pia ana hivyo Vitu vitatu!
1.Mungu ana "NAFSI" (Mwanzo 22:16,1Samweli 2:27),ndio Mungu Baba huyo
2.Mungu ana "ROHO" ndio Roho mtakatifu,Roho wa Bwana (Mwanzo 6:3,waamuzi 3:10 Hapa kuna maandiko Mengi sana yanayo elezea Roho wa Mungu)
3.Mungu ana MWILI,hapa ndipo penye utata! mwili wa Mungu ndio Yesu kristo!,Biblia imesema wazi kabisa kabla Mungu hajaumba chochote kile aliuumba mwili wake,alimuumba Yesu kristo ,Wakolosai 1:15-16 "Ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyoooote" ndiomaana Mungu alimwita Yesu kama Mwanawe wa pekee "Yohana 3:16",Yesu alikuwepo tangia zamani(Yohana 8:58),Yesu ni Mungu katika mwili "1Timotheo 3:16!,Yesu ni Mungu kati yetu "Mathayo 1:23,Yesu ni Neno na neno ni Mungu!,Yohana 1:1-3,Mwanzo 1:1,Yesu alimtokea Ibrahimu wakati Mungu anataka kuangamiza Sodoma na Gomora "Mwanzo 18,Yohana 8:56,Yesu alionekana pamoja na Shadraka,Abednego na Meshaki katika tanuru la Moto" Daniel 3:23-25, kuna vifungu viingi vinavyoongelea U-Mungu wa Yesu ni wewe mwenyewe kusoma na kuamini katika biblia.
2.Jibu la swali lako la pili.,
Wakristo wengi wamekuwa kama Nyumbu hawasomi maandiko na kuyachunguza wanapokea kile wanachoambiwa na wachungaji wao kama kilivyo,kumbuka sio kila wachungaji unaowasikia na kuwaona ni watumishi wa Mungu,wachungaji wengi sana sikuhz ni mapandikizi ya shetani wanapewa na kuambiwa cha kufanya na kuhubiri kutoka chini,mithali 14:15 "mjinga huamini kila neno bali mwerevu hayachunguza" sio kila unaloambiwa kanisani lipo sawa nenda kalichunguze kabla ya kuliamini tunaishi nyakati za mwisho hizi Uongo ni mwingi makanisani,
3.Jibu la swali lako la tatu
Lengo la kuja Yesu ni kuikomboa dunia yoote kutoka kwenye utumwa wa dhambi na sio wayahudi tu,na ukisoma kabla ya kuja Yesu ilikuwa ni kuhusu taifa moja tu la israel na sio mengine ilikuwa ukombozi kwa wana wa israeli tuna sio wana wa mataifa yoote,mafundisho ya agano la kale kipindi kile yalikuwa kwa ajili ya wale wana wa israel na mafundisho ya agano jupya baada ya yesu kuja plus na yale ya agano la kale ni kwaajili ya kila mtu kujifunza ndiomaana Yesu aliwaagiza wanafunzi waki wakaihubiri injili mataifa Yooote na sio wayahudi tu! maagano yoote la kale na jipya yoote ni neno la Mungu lile lile linafaa kwa mafundisho,yesu alisema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza Mathayo 5:17