Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Uhalisia wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi kwa Waathirika wa Maporomoko, Hanang, Manyara
Uhalisia wa hali ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa waathirika wa maporomoko yaliyotokea katika Wilaya Hanang, Mkoa wa Manyara.
Kumekua na wimbi la waandishi uchwara na wapotosha taarifa bila kuchukua muda kuchambua na kutafiti kwa kina habari zao lengo likiwa ni kujipatia umaarufu "Kiki" na wafuasi wengi mitandaoni.
Pichani ni muendelezo wa ujenzi mzuri wa nyumba za makazi ambazo zipo kwenye hatua mbali mbali za ukamalishaji zinazojengwa katika kijiji cha Warret wilayani Hanang. Nyumba hizi 108 ni moja ya nyumba bora zilizoidhinishwa kujengwa na zinategemewa kumalizika na kukabidhiwa kwa wananchi walioathirika na makazi yao mwaka huu.
Tunaendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miongozo yake na kuridhia kwa ujenzi wa nyumba hizi.
Ni vyema kukawa na hoja na sio vihoja hasa tunapogusa maslahi mapana ya wananchi.Tukatae wapenda kiki mitandaoni.
Serikali ya awamu ya sita ipo kazini kweli kweli.