UHALISIA

UHALISIA

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
UHALISIA

: REALITY (uhalisia) tunautengeneza ndani ya fikra zetu,Tunaweza
Kuubadili uhalisia kwa kuanza kubadili mfumo wa FIKRA zetu.😎

: Usikubali kukosewa HESHIMA kabisa hata kutoka kwako wewe mwenyewe....

: Hupaswi kukaa karibu na watu ambao hawakuheshimu,wala kukuthamini.
TUmia kutokuwepo kwako(Absence),kuijenga thamani yako...Nimegundua hili neno "Mkuu sikuizi huonekani"
Lina thamani zaidi ya hili neno " Huyu fala amerudi tena"

: Kuna muda watu wanatakiwa kuona hatari yako,yaani wanapaswa kujua kabisa wakijitoa betri unauwezo wa kuleta machafuko kabisa...hapo mahali.

: Wewe mjinga unajaribu kumfurahisha kila mtu,Badala ya kuunda na kuishi kwenye ulimwengu wako,unataka kuishi kwenye ulimwengu wa wengine,huoni watatawala uhuru wako,?
Huoni unauza furaha yako?
Huoni unapiga mnada utu wako

Yaani unataka kumfurahisha kila mtu wewe ni nani?
Yaani unataka jambo ambalo Mungu wako halifanyi?
Mungu mwenyewe hamfurahishi kila mtu.....kwanini?
Tazama wakati wewe unacheka na kula na kunywa,kuna kapuku huko mtaani amelala kwenye mabaraza ya maduka unafikiri ukimweleza mungu anampenda atakuelewa kwa uzito ule ambao,mtoto wa mwenye nazo anavuta hewa ya kiyoyozi....😂😂😂😎

Wakati unapumua vizuri na Afya nzuri kuna mwenzako hospitali,anapumua kwa msaada wa vifaa
Usifikiri moyoni mwake ukimwambia tuna usawa atachukulia kwa uzito.

CODE:###1
Mwanaume anapokufundisha kuvua samaki...
Usijifanye mjanja ukaanza kuvua kwenye bwawa lake....
Niamin

Ahsante
Content created by : magical power
 
Back
Top Bottom