Syston
JF-Expert Member
- Nov 6, 2017
- 243
- 351
Wadau, nimelileta hili maana limenivuruga akili haswa.
Ipo hivi: Niliingia tovuti ya Uhamiaji kwa ajili ya maombi ya passport ila mambo niliyokutana nayo huko yameniacha hoi na kunifanya niamini siasa siyo mchezo mzuri. Kero nilizoziona ni kama ifuatavyo:
1. Katika kujaza form kuna kipengele kimeniuliza dhumuni la safari na ninasafiri kwenda nchi gani. hapa najiuliza kila anayeomba passport ni lazima awe anasafiri au passport unatakiwa uwe nayo ili ikitokea unasafiri ndio unaomba Visa ya nchi husika.
2. Hiki ndo kituko zaidi, imagine kuna kipengele kinanielekeza uwezekano wa kuombwa uthibitisho wa tiketi ya kurudi, cheti cha kuzaliwa cha bibi.
Hivi mtu nina miaka 30 unaniambia kweli nilete cheti cha kuzaliwa cha bibi, nyie bibi zenu wana hivyo vyeti? Au ndiyo mwenye nguvu mpishe? Acheni kuweka siasa kwenye mambo yenye maslahi na maisha ya watu.
3. Ajabu ni kuwa utaratibu wa kuomba passport umewekwa uonekane ni lazima uwe unasafiri ndiyo uombe passport, lakini je, inapotokea mtu anatakiwa asafiri haraka iwezekanavyo kuna utaratibu wa uhamiaji kutoa passport haraka iwezekanavyo au ndo mtafuata taratibu zenu na kuharibu dili za watu?
4. Kwa sasa tuna vitambulisho vya taifa ambavyo kuvipata kuna mchakato mtu anapitia kama kuhakikiwa na uhamiaji wenyewe, amabapo wasio na vyeti vya kuzaliwa wamepeleka viapo na walipokidhi vigezo wakapatiwa NATIONAL ID, anapokuja mtu anataka passport jaribuni kurahisisha kwa huyu mwenye kitambulisho cha NIDA maana taratibu mnazotaka apitie tayari alizipitia wakati mnamthibitisha kuwa ni Mtanzania na mkampa go ahead kwenda NIDA kupata ID. Kiukweli uhamiaji nilijaribu kuona labda hata kun amahali inasema kwa Muombaji mwenywe kitambulisho cha taifa afuate hatua hizi, sikuona zaidi ya mahali tu mmeomba utambulisho wa taifa. Badilikeni muende na kasi ya technolojia sio kila siku mtu anarudia kufanya vitu vilevile, mbona tra, brela nk, hawana longolongo wanaomba tu namba ya NIDA basi mchezo umeisha.
There is no such a thing as a little freedom, either you are completely free or a total slave.