Kuanzia sasa, unatakiwa kutembelea mara kwa mara tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji Tanzania www.immigration.go.tz kufuatilia orodha ya majina ya pasipoti zilizokamilika, ambayo itawekwa kila siku.
Jina lako likiwa kwenye orodha, unatakiwa kufika katika sehemu husika ya Uhamiaji kuchukua pasipoti yako tayari kwa matumizi katika safari zako za nje ya nchi.
Alipoulizwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Paul John Mselle amesema “Tumefanya hivyo ili kuwakumbusha pia Wananchi kwenda kuchukua Pasipoti zao, mfano Dar es Salaam pekee kuna zaidi ya Pasipoti 4,000 hazijachukuliwa.”