Pre GE2025 Uhamiaji: Mgeni Aliyeomba Uraia wa Tanzania anaweza kuwa Mbunge au Waziri ila haruhusiwi kuwa Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo viongozi wa ngazi ya RAISI wote walio hai ndio WATANZANIA?

Wavamiaji walishafariki kwa kushindwa kutimiza misheni?
 
Maana hata hao wanaopewa uraia huwezi jua mikakati yao iliyojificha, kwa sasa watanzania wapo wengi walioelimika na kuwa na uwezo wa mambo mbalimbali, kuna haja gani ya kujikomba kwa raia wahamiaji....​
Serikali iliangalie hili swala kwa mapana zaidi
 
Mbona jiwe mkabila umemuacha mpiga dili nae ,
 
Mwenye mamlaka ya kuzungumzia uraia ni nani kati ya CDF,UHAMIAJI AU IGP?
Ni yupi anazo takwimu za ndani kabisa za raia wa asili,kuzaliwa na kuomba ndani ya Nchi hii kati ya hao?
 
ni kweli kabisa .maana kuna makabila mengine wa nchi fulani wana agenda za siri za zaidi ya miaka 50.PK ni mmoja wao .
PK ana kiburi na dharau sana,nakumbuka aliwahi kumpiga biti JK akiwa Rais kuwa anauwezo wa kumpiga wakati wowote akiamua,ila baada ya wale mbwa wake M23 kule DRC kupokea kipigo cha shalubela toka wanajeshi wetu waliokuwa kule akapunguza makeke,lakini bado ana nia ovu sana na nchi yetu na kweli amepandikiza watu wake kila sehemu. Nakumbuka miaka kadhaa kuna ofisa mmoja wa Jeshi letu alitoroka na kwenda kusikojulikana alikuwa mtu wake aliyempandikiza kwenye jeshi letu. CDF amenusa hatari kubwa asipuuzwe.
 
Ukiwa ni mgeni Tanganyika unaweza ukashamgaa sana siasa zinazopigwa pindi ukaribiapo uchaguzi.
Hizi ni siasa tu huenda kwakuwa wana hofu na mtu flani hivyo CDF anatumika kisiasa ili km itatokea huyo mtu wanaemhofia akagombea,basi neno muhamiaji au mkimbizi litumike km sehemu ya prpaganda yao na lisiwe geni masikioni mwa mbumbu a.k.a wanyonge na iwe rahisi kutomkubali.

Km ilikusudiwa na kweli hao watu wapo kwenye ngazi za juu za maamzi lilikuwa siyo jambo la CDF kupewa autangazie umma bali kuwawajibisha walioruhusu hilo litokee ama kufanya marekebisho ya dosari zilizo jitokeza.

Nawarudisha nyuma mwaka 2010,hapa Mkamba Sr akiwa KM wa CCM halafu Slaa akiwa mioyoni mwa Watanganyika. Ghafla tu ikaonekana Slaa ana mke wa mtu na ikawa agenda ya wanyonge.

Fanyeni kazi acheni mijadala ambayo itakoma baada ya uchaguzi wa 2025.
 
Alberto Fujimori raia wa Japan aliwahi kuwa Raisi Peru na akaiongoza Nchi vizuri kuliko Maraisi "Wazawa" na hakumuuza hata Mwananchi mmoja Utumwani.

Hii sheria yetu ya kuzuia mtu kuwa Raisi wa Jamhuri ifutwe iruhusu vigezo kuwa lazima uwe raia wa AFRIKA.

iseme hivi kama wewe ni raia wa Nchi yoyote ya AFRIKA na umeishi TANZANIA kwa zaidi ya Miaka 10 basi Rukhsa kuwa Raisi wa Jahmuri.

Ndio maana kwenye wimbo wa Taifa tunasema "Mungu Ibariki AFRIKA"
 
Swala sio Asili Bali alizaliwa Zanzibar/Tanzania au hapana? Babu ndio wa Oman ila baba yake ni Mzanzibar.

Je waliozaliwa Nje ya Nchi na wakaletwa Tanganyika nani raia kati Yao na Samia aliyezaliwa Zanzibar ila ana mababu Oman? GwaB
Mnajichanganya sana nyie!. Kwa hiyo Samia kuzaliwa Tanzania wakati asili yake ni Oman sheria zinaruhusu Lakini watu waliotuhumiwa na Mkuu wa majeshi si wana asili ya nchi jirani? Si wana mababu zao huko pia? Hii double standard inatoka wapi kwa uhamiaji kutaka kuonyeshwa hata makaburi ya kizazi cha tatu nyuma kwa mikoa ya magharibi ya JMT ? 😳
 
Swala sio Asili Bali alizaliwa Zanzibar/Tanzania au hapana? Babu ndio wa Oman ila baba yake ni Mzanzibar.

Je waliozaliwa Nje ya Nchi na wakaletwa Tanganyika nani raia kati Yao na Samia aliyezaliwa Zanzibar ila ana mababu Oman? GwaB
Baba yake Samia mzanzibari hata kama alizaliwa Zanzibar si baba yake (Babu yake Samia) si ni muomani? ... Oman ni sehemu ya JMT?
 
Maana hata hao wanaopewa uraia huwezi jua mikakati yao iliyojificha, kwa sasa watanzania wapo wengi walioelimika na kuwa na uwezo wa mambo mbalimbali, kuna haja gani ya kujikomba kwa raia wahamiaji....​
Mbona Waasia (Wahindi Wachina Wabengali Wapakistani)ndio wanaomba Uraia kwa wingi sana kuliko hata Waafrika wenzetu lakini huoni watu wakihoji dhamira yao.

Lakini wakiomba Wahutu au Watutsi tu unaanza kusikia mara ooh...Wahima Empire mara ooh..Bakuba Empire Mambo ya kijinga sana.
 
Huu ujinga muwe mnadanganyana wenyewe uko.hizi sio zama zakuendekeza propaganda za kijinga.

In a serious note , taja mpinzani wa kumpa nchi badala ya CCM ?

Mbowe ?

ZZK ?


Tunataka kutoa nchi kutoka CCM , ila hatuoni wa kumpa

It is a naked and painful truth
 
Baba yake Samia mzanzibari hata kama alizaliwa Zanzibar si baba yake (Babu yake Samia si ni muomani? ... Oman ni sehemu ya JMT?
Ndio Sasa Samia anaweza kujivunia kuwa Mu Oman au Mtanzania? Obama ni Mkenya au Mu America?
 
Hata akiwa mfuasi wa Chadema anaweza kugombea udiwani tukiacha ubunge?
 
Ndio Sasa Samia anaweza kujivunia kuwa Mu Oman au Mtanzania? Obama ni Mkenya au Mu America?
Tunaongelea uraia pacha wa Samia vis à vis Tanzania na Oman ... Mfano wako wa Obama hauna mashiko! .... Swali ni Je, Tanzania inaruhusu uraia pacha?
 
In a serious note , taja mpinzani wa kumpa nchi badala ya CCM ?

Mbowe ?

ZZK ?


Tunataka kutoa nchi kutoka CCM , ila hatuoni wa kumpa

It is a naked and painful truth
Kweni TANU wakati wanakabiziwa walikuwa na uzoefu gani?

Hizi ni zama za Wapinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…