Uhamisho kwa walimu walio omba kuhama dec.2014

mkuu procedure/ vigezo vinavyotumikaukitaka kuhama.

Remote: Procedures za kuomba uhamisho hizi hapa.

Kazi ni kwako ww mtumishi unayetaka kuhama halimashauri yako kwenda halimashauri nyingine.

UTARATIBU WA UHAMISHO WA WATUMISHI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

KUNDI A: UHAMISHO WA NJE YA MKOA
. HATUA YA KWANZA –MAOMBI YA KUHAMA 1. Mtumishi anatakiwa kuandika barua ya maombi ya uhamisho kupitia kwa Mwalimu Mkuu, Afisa Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri anayotoka kama ni Mwalimu, au msimamizi wa kazi, Mkuu wa Idara na Mkurugenzie kwa watumishi wasio Walimu
2. Kwa nafasi ya Mkuu wa Idara, barua lazima zipitishwe na Mkuu wa Idara Mwenyewe au Kaimu aliyekaimishwa rasmi na Mkurugenzi
3. Kwa nafasi ya Mkurugenzi, barua za maombi zipitishwe na Mkurugenzi mwenyewe au Kaimu wake.
4. Barua ya maombi ya uhamisho iliyopita ngazi tajwa juu za Halmashauri ambayo mwombaji anataka kuhama itatumwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri anayoomba kuhamia.

HATUA YA PILI-MAOMBI KUKUBALIWA
5. Mkurugenzi Mtendaji atayachambua maombi ya kuhama mtumishi huyo, atamuandikia Katibu Tawala wa Mkoa yeye binafsi ama Kaimu wake juu ya kukubaliana na maombi hayo nakala anakokwenda.
6. Baada ya Mkurugenzi husika kupatiwa jibu kuwa mtumishi husika amekubaliwa kuhamia katika Halmashauri aliyoomba Mkurugenzi ataandika barua kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TSMISEMI akipitisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
7. Katibu Tawala wa Mkoa atakusanya barua zote zilizopitishwa kwake na kuzituma kwa Katibu Mkuu,OWM-TAMISEMI kila tarehe 30 Septemba na 15 Desemba kwa uhamisho wa Desemba, na tarehe 15 Machi na 15 Juni kwa uhamisho wa Juni. Barua za maombi hayo zitumwe na viambatisho vya barua za wakurugenzi na waombaji.
8. Mara baada ya uhamisho kutolewa, Katibu Tawala wa Mkoa atapewa nakala ya barua ya kila mtumishi aliyehamishwa na aliyehamia Mkoani kwake kwa ufuatiliaji na kumbukumbu za Ofisi.
9. Ni jukumu la kila Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kuwa watumishi waliohamia wanaripoti katika vituo vyao vipya vya kazi ndani ya siku kumi na nne kama ilivyoelekezwa kwenye barua ya uhamisho.
10. Mtumishi yeyote mwenye malalamiko kuhusu uhamisho ayapeleke kwa Katibu Tawala wa Mkoa na asiyehama ndani ya siku 21 hatua za nidhamu zianze kuchukuliwa.

KUNDI B: UHAMISHO WA NDANI YA MKOA
A. HATUA YA KWANZA –MAOMBI YA KUHAMA 1.Mtumishi ataandika barua ya maombi ya uhamisho kupitia kwa Mwalimu Mkuu, Afisa Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri anayotoka kama ni Mwalimu, au msimamizi wa kazi, Mkuu wa Idara na Mkurugenzie kwa watumishi wasio Walimu .
2. Kwa nafasi ya Mkuu wa Idara, barua lazima zipitishwe na Mkuu wa Idara Mwenyewe au Kaimu aliyekaimishwa rasmi na Mkurugenzi .
3 .Kwa nafasi ya Mkurugenzi, barua za maombi zipitishwe na Mkurugenzi mwenyewe au Kaimu wake.

B. HATUA YA PILI-MAOMBI KUKUBALIWA 5.Mkurugenzi Mtendaji atayachambua maombi ya kuhama mtumishi huyo, atamuandikia Katibu Tawala wa Mkoa yeye binafsi ama Kaimu wake juu ya kukubaliana na maombi hayo nakala anakokwenda.
6. Baada ya Mkurugenzi husika kupatiwa jibu kuwa mtumishi husika amekubaliwa kuhamia katika Halmashauri aliyoomba Mkurugenzi ataandika barua kwa Katibu Tawala Mkoa kumwombea mtumishi husika idhini ya uhamisho.
Uhamisho wa Ndani ya Mkoa unatolewa muda wote pale mtumishi anapokuwa amekamilisha taratibu zilizoelezwa hapo juu.
Note.Viambatanishi mhimu kwenye barua ya mwombaji Wa Uhamisho ni :Nakala ya kitabulisho cha kazi,Cheki Na,Barua pepe kama unayo,Anuani ya posta, na namba ya simu ya mkononi.
 
utaratibu huu na ule wa kubadilishana vituo upi mzuri?
 
Back
Top Bottom