KERO Uhamisho Mkundi Mlimani Sekondari - Morogoro lazima uchangie kiti na meza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

anonymous12

New Member
Joined
Feb 13, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Nimeomba nafasi mwanafunzi ahamie shule ya Sekondari Mkundi Mlimani, Morogoro Manispaa ila nje ya michango mingine nimeambiwa nitoe laki moja kama "Mchango wa meza na kiti" kwakuwa Mkuu hapokei mwanafunzi ambaye anakaa chini.

Sasa, je hicho kiti na meza akimaliza kidato cha nne anaondoka nacho? Na Serikali haigharamii viti na meza?

Maana kwenye kufatilia kwa wazazi wengine kikao kilikaliwa na wazazi wakakubaliana kuchanga elfu tatu kila mmoja kuanzia mwezi wa saba mwaka 2025 hivyo kuwa na mchango wa elfu 19 kwa ajili ya ukarabati wa viti na meza. Mbona mimi naambiwa laki moja na mwingine aliambiwa laki moja?
 
Mkuu ni vile hizi shule zetu mnaziona kwa mbali tu mkiwa mnapita barabarani.

Toa hiyo pesa ila hakikisha mtoto anakabidhiwa hicho kiti na meza yake. Kuchangia maendeleo ya shule sio jambo la kujitenga nalo.
 
Nimeomba nafasi mwanafunzi ahamie shule ya Sekondari Mkundi Mlimani, Morogoro Manispaa ila nje ya michango mingine nimeambiwa nitoe laki moja kama "Mchango wa meza na kiti" kwakuwa Mkuu hapokei mwanafunzi ambaye anakaa chini.

Sasa, je hicho kiti na meza akimaliza kidato cha nne anaondoka nacho? Na Serikali haigharamii viti na meza?

Maana kwenye kufatilia kwa wazazi wengine kikao kilikaliwa na wazazi wakakubaliana kuchanga elfu tatu kila mmoja kuanzia mwezi wa saba mwaka 2025 hivyo kuwa na mchango wa elfu 19 kwa ajili ya ukarabati wa viti na meza. Mbona mimi naambiwa laki moja na mwingine aliambiwa laki moja?
Mkiambiwa muitoe sisiem mnajifanya mpo bize na kilimo
 
Back
Top Bottom