Uhamisho wa Dodoma ulivyonufaisha watumishi

Davan

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
1,125
Reaction score
1,413
Huku mtaani kulikuwa na magofu mengi yamesimama ila watu baada tu ya kulipwa hela ya uhamisho ujenzi umeendelea na wengine wamemaliza kabisa.

Watumishi waliokuwa na ndoto za magari wamenunua hata ya mkononi kwa mtu.
Wengine wamenunua viwanja hata kama ni vidogo.

Wengine wamepauwa nyumba zao zilizokwama kwa miaka mingi. Watumishi wengi walikuwa na ndoto ila mifuko ilikuwa imetoboka. Jirani yangu alianza ujenzi 2010, ujenzi ukasimama 2014 kamalizia 2019 baada ya kupata hela ya uhamisho.

Kila jambo ni fursa.
 
Aisee kwamba pesa za uhamisho ni mamilioni mengi kiasi hicho sio?

Kweli sasa tuko uchumi wa kati.
 
Kwamba pesa za uhamisho wamejengea majumba na kununulia magari! CCM imewageuza mzombi nyie watu
 
Hela ya uhamisho haiwez kumaliza gofu wala kununua gari ya maana na jukum la kuhama bad linakukabili labda kwa watumishi wachache tu ndo wamenufaika kwa njia hiyo

Tena uhamisho wa Dar-Dom mbona ni pesa ya kawaida tu pengine ukaingia na hasara zingine kubwa zaid maana ukihama Ni kama vile unaenda kuanza moja
 
Kweli huwezi pata gari ya maana ndio maana nimesema wamenunua gari za mkononi 4-7 mill
 
Kwamba pesa za uhamisho wamejengea majumba na kununulia magari! CCM imewageuza mzombi nyie watu
Kama ndio unavyowaza sawa, ila jua kuna watu wamekunja 5-10 mill kutegemeana na ofisi
 
Nauli mke watoto wanne, hela ya mizigo, hela ya kujikimu na mambo mengine sio ndogo kiivyo.
Hata mimi nimejiuliza inamana pesa ya uhamisho ni nyingi kiasi hicho.
 
Huku mtaani kulikuwa na magofu mengi yamesimama ila watu baada tu ya kulipwa hela ya uhamisho ujenzi umeendelea na wengine wamemaliza kabisa.

Watumishi waliokuwa na ndoto za magari wamenunua hata ya mkononi kwa mtu.
Wengine wamenunua viwanja hata kama ni vidogo.

Wengine wamepauwa nyumba zao zilizokwama kwa miaka mingi. Watumishi wengi walikuwa na ndoto ila mifuko ilikuwa imetoboka. Jirani yangu alianza ujenzi 2010, ujenzi ukasimama 2014 kamalizia 2019 baada ya kupata hela ya uhamisho.

Kila jambo ni fursa.
Hiyo hela ya uhamisho ni kiasi gani hadi ujenge....sana sana 6m tena kwa afisa ngazi za juu.
 
Back
Top Bottom