Uhamisho wa uonevu TRA, Kamishna Mkuu tafadhali ingilia kati

Kuna kale kajamaa kafupiii kalikuaga kamishna hapo TRA kakatumbuliwa sasahivi knahangaika na madaladala ya mwendokasi kalikua kanaoneaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, kanahamisha tu watu ilimradi tu kutenganisha wake na waume zao etc etc , kimsingi TRA kuna shida sana hasa inapokuja suala la mtumishi kutotoa kitu kidogo kwa wakubwa zake na lile la rushwa ya NGONO ndio kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Tatizo Watu hudhani Kazi ya kukusanya Kodi TRA ni fursa ya kutajirika lakini wanasahau kuwa kutoza ushuru ni sehemu ya Ibada ilu Jamii iweze kustawi

Sijawahi kumuona Kamishna wa TRA aliyekuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu kuanzia enzi za akina Ndyetabula, Rutaitina, ST Masawe, Kapera, Kezilahabi, Sanare, Silla, Kitilya, Masamaki nk....nk

Rushwa hupofusha macho kwa mujibu wa Biblia
 
Mbona mnamsimanga sana wakati madai yake ni genuine.
 
TRA imebaki jina tu

Staff wanarogana kama hawana akili nzuri

Ukienda kwa Mwamposya utawakuta Mapolisi na Watoza ushuru ndio wanaongoza kwa kutolewa mapepo

TRA hawapendani kabisa

RIP Tarimo
Hiyo ishu sio TRA pekee sehemu nyingi zinazojaza watu pana mambo ya ajabu ajabu sana...wanamaindiana huko utadhani pana kitu cha maana wanapata kumbe kawaida tuu..
 
Yah..haijakaa SAwa hiyo
Uhamisho si jambo baya kwenye utumishi, ni kawaida mfanyakazi kuhamishwa kutoka kituo kimoja Kwenda kingine ili kuimarisha utendaji na kuleta ufanisi. Tatizo kubwa ni kuwa wafanyakazi tunahamishwa bila kulipwa stahiki zetu.

Mkuu wa Rasilimali aliyepo hapo anatulazimisha Kwenda kwenye vituo vipya bila kulipwa anasema kama huna hela za kuhama nenda kakope Benki au mahali popote ili mradi uende unakotakiwa Kwenda. Na anatishia kuwa usipokwenda utaona kitakachokukuta ikiwa ni Pamoja na kuhamishiwa TAMISEMI.

Inaonekana kuw TAMISEMI ndio sehemu ya kupeleka watu wasiotakiwa.
 
Mbona mnamsimanga sana wakati madai yake ni genuine.
Sasa mtumishi anapoambiwa atafute fedha zake ahame kana kwamba alijihamisha mwenyewe, je hii ni haki ?. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anajua kuwa kuna uonevu wa namna hii TRA ? Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa analijua hili, Mkuu wa Utumishi, na Waziri wa Fedha wanalijua hili ? Nakumbuka serikali ilishatoa agizo kuwa mtumishi akihamishwa lazima apewe stahiki zake kwanza ndipo ahame sasahii ya kujigharimia imetoka wapi na kutishana kwenda TAMISEMI ?
 
Mimi sifanyi kazi mamlaka ya zakayo lakin kuwalaumu katika kukusanya kodi ni tu unapungukiwa na ujuzi wa sheria wanazotumia kufanya kazi zao.
Kodi ni muhim kwa maemdeleo na ustawi wa nchi lakin adui mkubwa wa ulipaji huo ni watunga sheria au sera.
Kiuhalisia wakusanya kodi wakinyoosha rula jumuia yote ya wafanyabiashara ingekuwa na vilio kama vya msiba wa waliokula sumu kwenye shughuli. Aina ya rushwa zao ni scratch my back I scratch yours. Looser ni fuko kuu.
Nadhan umeshajua tatizo lilipo. Nadhan umeshamjua wa kupiga jiwe kwa kombeo!
 
Mambo sio marahisi hivyo bro ?
Boss, Halmashauri, Tamisemi na kufananako, wanaitwa kwenye vikao Dar au Dom kutokea chaka huko, wanajigharamia wakiahidiwa kulipwa, wengine wanamaliza miaka 2 hawalipwi, achilia mbali kukopwa mshahara wa kwanza na wa pili wa kuanzia kazi kwa kigezo cha Cheque Number.

Sema hata hivyo TRA mpo pazuri aisee, nimesikia kuanzia siku hizi basic ni kuanzia 5m kwenda mbele, sasa Disturbance allowance kama ni 10% ya gross ya mwaka mzima, unazungumzia kiasi kisichopungua 6m kwenye disturbance tu, bado usafiri, kujikimu n.k sio?

Si ajabu ndo maana unalalamika, mzigo wa maana huo! Tamisemi, watumishi wamekabidhi ATM card kwa wadai wao kwa mkopo wa Disturbance allowance yako tu teh teh teh teh
 
Mfanyabiashara akitunza kumbukumbu vizuri analipa Kodi kidogo sana
 
Acheni kulialia.
Wizi mnaoufanya kila mwananchi anaujua.
Hebu mjihamishe, acheni serikali kuipa mzigo mara 2.
Huyo mkuu wa rasilimali watu anaijua michezo yote inayofanywa na watumishi wake.
Tumieni ukwasi wenu kuhama, hebu kuweni na huruma kidogo.
Nendeni TAMISEMI msubiri OC muone moto wake
 
Acha wafu mzikane
 
Dadeki na nyie mashetani mnalia hii nchi imeshaenda kuzimu. Tulie wote potelea mbali kenge nyie mnatuumiza sana mbwa nyie
 
Hivi masamaki ndo yule alikuwa na nyumba za kisasa zaidi ya mia Daressalamm?
 
Tamisemi hakuna nidhamu diwani wa ccm mwenye darasa la saba anakutikisa vilivyo na masters yako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…