Uhamisho wa watumishi wa serikali now umekuwa mgumu

Uhamisho wa watumishi wa serikali now umekuwa mgumu

Utanilipa ngapi baada ya kazi ukipewa Hadi barua na kuhama kabisaaa ndio unanilipa
Barua toka TAMISEMI sio ishu swala ni kwamba barua hiyo ni genuine? Wengi wanarudishwa kigezo kikiwa barua zao ni Fogery. Apambane kwenye ess huku kwingine ataliwa kichwa.
 
Habari za muda wakuu , poleni na majukumu,

Nije kwenye point wakuu ivi nawezaje kuhama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambako ndio home,, coz mm ni Mwalimu nipo MUFINDI IRINGA Kwa muda wa miaka 10+ mara kadhaa nimeangaika na swala la uhamisho Ili niende kwetu maana hapa sina mpango wa kuishi hivyo inaniwia vigumu kufanya uwekezaji

Ila swala la uhamisho limekuwa changamoto japokuwa taarifa zangu zipo TAMISEMI(zinazohusu kuhama) Ila naona siku zinaenda bila ishu yoyote naombeni msaada nitumie njia Gani Ili niweze kuhama huu mkoa?
10+ na Haujaanza kuishi?
Mufindi huko si ndio kuna mbao na miti huko?
 
Mkuu kumradhi kwa kutamka maneno haya ila ukweli ni kwamba elimu yako bado haijakukomboa.
Kila mtumishi akiwaza kufanyia kazi kwao umewaza kwamba hakutakuwa na uwiano sawa kwa idadi ya watumishi kwa kila mkoa.
Hii itapelekea mikoa fulani watumishi kurundikana na mingine kuwa na uhaba jambo ambalo halitakuwa na tija kwa Taifa.
Kwahiyo miaka 10+ uliyokuwa umeitumia kupambana kutafuta uhamisho na hizo fedha ulizotumia kuhonga ili uhame unhefanya uwekezaji hapo ulipo unaamini ungekuwa sawa na hapo ulipo sasa hivi?
Umewaza kurudi kwenu ili ukafanye nini? Hukumaliza kunyonya? Au unataka ukawavimbie wana kuwa na wewe upo kwenye payroll?
Unafikiria kwamba ukistaafu hautaishi hapo, sio jambo baya, ila piga mahesabu utakuwa mtumishi wa umma hadi utakapofika miaka 60 mbona unaweza kuwekeza hapo ulipo na baada ya kustaafu ukahamia kuishi popote unapotaka hata ikiwa nje ya nchi ukiwa na kibunda cha kueleweka tu.

Wewe nawe bwana.

Kila mtu ana haki ya kuamua ayapeleke vipi maisha yake. Yeye ameamua anataka arudi kwao wewe una manga. Acha hizo. Heshimu maisha yake na maamuzi yake. Kanuni za utumishi ziko wazi, baada ya miaka mitatu, mtumishi anaweza kuhama. Yeye amekaa 10+ Huoni kuwa anakua unproductive
 
Wewe nawe bwana.

Kila mtu ana haki ya kuamua ayapeleke vipi maisha yake. Yeye ameamua anataka arudi kwao wewe una manga. Acha hizo. Heshimu maisha yake na maamuzi yake. Kanuni za utumishi ziko wazi, baada ya miaka mitatu, mtumishi anaweza kuhama. Yeye amekaa 10+ Huoni kuwa anakua unproductive
Ukishakuwa mtumishi baadhi ya uhuru wa kujiamulia kuishi unavyotaka unakuwa limited.
Ndiyo maana ni busara kwenda na rythim ya mwajiri kwa kubadili changamoto kuwa fursa ila ukiona inakuwa ngumu unapiga chini ajira ili uwe na uhuru wa kuishi unavyotaka.
Ni kama hadithi ya mitete na mpapai, uchaguzi unabaki kwake aende na upepo au ashupaze shingo avunjike.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Ningekuwa nina asili ya kihaya ningekwambia jambo ambalo lingebadili kabisa hiyo picha yako ya kulamba asali nono ila acha tuendelee kuonekana kama majobless.
Wahaya Bhn ko unampiga Mkwala mzee wa watu afu unalia kwenye jukwaa la ajila hahaha 🤣 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom