Kwanza kabisa ningependa niwasalimu kwa jina la jamhuri wa muungano wa Tanzania ndugu zangu wa jukwaa hili mahsusi huku lengo kubwa likiwa ni kupashana habari mbalimbali na kubadilishana mawazo yanayoweza kutufungua na kuleta tija zaidi kwenye jamii inayotuzunguka.
Kwanza kabisa ningependa nieleweke kwamba dhumuni la kuja na huu uzi sio kwa ajili ya kudhihaki imani za watu fulani HAPANA!!, bali ni kuhitaji ufafanuzi wa kina na kupata majibu sahihi ya haya maswali yangu. Pasipo kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye mada husika.
(1). UHARAMU WA KULA NGURUWE:
Nimekuwa nikiwaza kuhusiana na huyu kiumbe aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu na kuletwa hapa Duniani kama vile vilivyo viumbe wengine wa angani, baharini, na nchi kavu iweje aharamishwe? au kuna vitimbi alishawahi kuwafanyia baadhi ya watu kipindi cha nyuma na kupelekea kuwa chanzo cha yeye kuwa Haramu?
(2). KWANINI HAIRUHUSIWI KUZUNGUMZA UKIWA CHOONI?
Zipo baadhi ya dini ambazo ukifuatilia mafundisho yake yanakataza kabisa kuzungumza ukiwa chooni, kupiga mswaki na kusukutua kwenye tundu la choo, kama iyo haitoshi wakaenda mbele zaidi na kudai kwamba chooni ni moja ya maskani ya majini wa shari.
Hapa nikajiuliza vipi kwa wale waliopanga chumba kimoja na choo ndani al-maarufu kama MASTER inakuaje? Maana kuna nyakati nyingine unaweza ukajisahau kufunga mlango wa choo ivyo kuwa rahisi kwa hao majini kumuingia mwanadamu na kuleta dhohari ndani ya nyumba.
(3). KWANINI ASILIMIA KUBWA YA WATU WENGI WANAOIJUA DINI HUWA WANAKUWA NA ROHO MBAYA SANA ZILIZOJIFICHA?
KWa mujibu wa tafiti zangu nilizofanya kwa takribani miaka 10 iliyopita hasa kwa watu wanaozijua dini(WACHA MUNGU) nikianzia makazini, majumbani, na hata kwenye nyumba za ibada huwa wanakuwa na roho mbaya ambazo mpaka uwe na jicho kali sana ndio unaweza ukaziona wazi. Hadi Hii leo bado sijajua chanzo ni nini?
(4). KUSALIMIA VITU VISIVYOONEKANA
Hapa nitaenda moja kwa moja kwa ndugu zangu waislamu, huwa tunaambiwa kama unaishi kwenye nyumba yako ikatokea ukatoka ukaenda kwenye mihangaiko yako masalani asubuhi, ukirudi jioni basi wakati unaingia ndani kwako basi ni lazima utoe salamu(ASALAAM ALEIKUM). BADO NIPO NJIAPANDA
Najua wapo watakaokuja kunikejeli na kunirushia maneno ya kashfa na matusi lakini siku zote atafutae ukweli hachoki, hata akichoka keshapata. NAHITAJI UFAFANUZI KWENYE HAYA. Nawasilisha