Uharibifu wa viti zaidi ya 200 uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba

Kwakweli ningekuwepo uwanjani na mimi ningekosa uvumilivu..uwezi kuvumilia ule ujinga..
 
Watanzania wana hasira nyingi sana rohoni mwao kutokana na misongo ya kimaisha. Kitu kidogo tu kinaweza kuziamsha na kufanya maamuzi ya ajabu ssana.
 
Ulitaka warushe biscuit kutuliza ghasia!
Kiukweli mwenye akili timamu huwezi kumlaumu refa apo swala ni kujitambua cc wantanzania bado sana .kama mtu umekaa nyumbani kwako na unaangalia mpira kwenye TV refa anapo kosea kwann hauvunji vitu vyako vya ndani huu ni ujinga tulionao watanzania
 
Hivi simba mna miaka mingapi hamjawahi kuifunga yanga?
 
Unajua pale ndio uwezo wa Tambwe ulipoishia,

Kiwango chake kiko chini sana.
 
Siku nyingine refa akileta ujinga tutaenda pale katikati kwenye pitch zile nyasi zote tutazilima....tff wanatakiwa kuacha upuuzi wasimamie soka sio wanaleta fitna..
Ni hiviii, hata mumlete refa toka mbinguni simba hamna uwezo wa kuifunga Yanga, kwa hiyo usijeenda uwanjani ukiwaza kuifunga yanga, sisi hua tunakua wapole kwa sababu tunajua ya kua tunajua mpira, hata ikitokea tukifungwa ni sehemu ya mchezo, hata mtufunge tunaona kama kunguru kumnyea binadamu sio kwamba mnajua mpira ila mmebahatisha tuu. Sasa msitake kulazimisha ushindi wakati uwezo wa kushinda hamkonao
 
Ingekua ni mtu wa yanga ndio kawaita mbumbumbu ningesema kawaonea ila kwa kua ni kiongozi wao mkubwa basi naamini kweli watu wa simba ni mambumbumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…