Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Najua kukiwa na serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar maana yake muungano haupo. Kama serikali tatu haifai basi serikali moja, kama tunaupenda muungano kweli
 
Sidhani kama kuna uhasama....bali watu wanatoa maoni na kupendekeza muungano bora
 
Pascal, mie nimesoma chemistry. Sasa ngoja nikupe somo kidogo la chemistry, rahisi tu.

Water is a compound, formed by two hydrogen atoms bonded to an oxygen atom. Now the beauty of it ni kwamba, you can break down water, a compound, into its two primary components, oxygen and hydrogen. All you need is the right amount of energy, and this can be quite substantial. That is why we don't usually generate hydrogen from water, for use as an energy source. It is too expensive compared to other sources of energy.

Sasa, kuna siku there will be the right amount of energy to break this compound called muungano. When that critical energy is attained - if you are a Tanganyikan in Zanzibar, or a Zanzibarian in Tanganyika - you may have to run for your life because that energy will be very, very, very exothermic!
 
Umeongea mambo mengi ambayo ni nadharia mkuu.
Oman na Dubai hawana cha kuwekeza Zanzibar.
Oman na Dubai n.k n.k umuhimu wa Zanzibar ulikua zamani sio sasa hivi.
Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta more than 10 years back nenda katizame wako na hali gani.
Mafuta hayajawa critical energy resource kama ilivyo zamani.

Kuhusu kuwekeza kijeshi sasa hivi hakuna taifa litalothubutu kuja kuwekeza Zanzibar ilhali kimkakati wa geopolitics DJIBOUTI ndio kunafaa na ERITREA.
Umeeleza nadharia mkuu.
Zanzibar haina umuhimu kama unayoipa.
Oman na Dubai waje kuwekeza nini Zanzibar!?
Embu taja hizo potentials ambazo zitaifanya Oman ije kuwekeza Zanzibar?
Nchi za kiarabu zishahama huko unapopasemea embu kafuatilie vizuri.
 
Ndio maana nimekuambia kuna theory. Ni suala la amini usiamini. Logic.

Kumbuka kwamba hakuna kisiwa kisichokuwa na thamani katika geopolitical strategies. Uingereza walipigana vita na Argentina kwa ajili ya Falk Islands, ambacho ni kisiwa chenye mawe tu. Kuna misuguano kama hiyo kati ya China na Japan kwa visiwa wewe kwa mawazo yako utaona havina thamani. Sembuse iwe Zanzibar, ambako inasemekana kuna potential kubwa ya mafuta ambayo haiendelezwi kwa sababu maalum?

Unafikiri ni nini kimeifanya Singapore kuwa taifa tajiri sana duniani?

Kuhusu "Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta 10 years back nenda katizame wako na hali gani" huko ni kufikiri kubaya. UAE, Dubai, walianza kuchimba mafuta baada ya Nigeria. Angalia kuna hali gani. In fact, huwa wanawacheka Nigeria. Mifano ya mafuta katika Africa haifai kabisa, kwa sababu utawasema pia Angola. Afrika tunajua tatizo letu tunapokuwa na mafuta. Watolee mfano Norway, Kuwait, Malaysia, etc
 
Juzi juzi hapa nilimsikia waziri tena dokta mzima akisema kero za muungano zimetatuliwa kutoka 15 Sasa zimebaki tatu tu😝
Kilichonidhi hakuzitaja kero zilizo tatuliwa na kero zilizobaki. Ni vizuri Sasa tuziweke kero zote hapa ili waziri amalizie home work yake.
Tusisubiri mpaka wanaokerwa na hizi kero wakawa wengi kuliko wasiokerwa.
 
Kama nilivyosema hapo juu, huenda wakiziweka wazi hizo kero wanazosema wamezitatua, Tanzania bara kwao itakuwa ni kero mpya zilizoingizwa kwenye muungano, hivyo sidhani kama watapenda kusema waziwazi ufumbuzi gani umetolewa kwa kero hizo.
 
Unakosea sana mkuu.
UAE na Oman zimeanza muda sana kuchimba mafuta kabla ya Nigeria na Senegal.
Embu nenda kafuatilie vizuri UAE na Oman zimekua petroleum producing nations na nadhani ni member wa OPEC muda mrefu sana.
Nigeria na Senegal wameanza juzi juzi tu hapa mzee!?

Mapigano ya Argentina na UK yalitokea mwaka gani!?
Nipe jibu halafu tufananishe geopolitical interests zilikuaje kwa mwaka huo na sasa.
-Visiwa ambavyo Japan na China wanagombania as well as visiwa vya south-China sea vinavyosemekana kuwa vya Phillipines kuna utajiri mwingi wa sana wa gesi mkuu nenda kafuatilie.
-Mafuta yaliyokuwepo Zanzibar hayafikii hata robo ya reserve ya mafuta yaliyokuwepo UAE na Oman.
Hakuna kitu Zanzibar kipo Oman ama UAE hakipo.
Pia watu washaanza kuhama na kupunguza umuhimu wa petroleum mzee,hivyo mahitaji yake sio makubwa kama ilivyo nyuma.
- Singapore mzee imeendelea kwa science and technology.Pasi,deki,TV mpaka fridge unazotumia ama ulizokua unatumia brand ya PHILLIPS NI SINGAPORE MADE.Na taifa lililowekeza sana Singapore ni China,hawakuendelea kwa mafuta wale kama unavyodhani.
Pia kuna Macau imeendelea kwa uwekezaji mkubwa wa hanasa na starehe.

Yani unaleta nadharia za zamani sana mkuu.
Zanzibar haina huo umuhimu unayoipa.
Mafuta yapo maeneo mengi pia sasa hivi hayana umuhimu kama zamani.
 
Nahisi siwezi kulumbana na wewe haya mambo. Hatutafikia muafaka kwa sababu tuko level tofauti katika ufahamu. Labda wewe umenizidi sana, au mimi nimekuzidi sana.

Kukuaga, soma hapa chini;

Nigeria
Oil was discovered in Nigeria in 1956 at Oloibiri in the Niger Delta after half a century of exploration. The discovery was made by Shell-BP, at the time the sole concessionaire. Nigeria joined the ranks of oil producers in 1958 when its first oil field came on stream producing 5,100 bpd.

UAE
In the early 1930s the first oil company teams conducted geological surveys in the UAE. Thirty years later, in 1962, the first cargo of crude oil was exported from Abu Dhabi.
 
Tunaficha vichwa huku mwili wote uko wazi kama mbuni.
 
Kama hupendi Muungano, hama nchi au kufa tu, there is nothing you can do dogo!! Muungano is here to stay.

Hata Seif Shariff Hamad, Christopher Mtikila, Aboud Jumbe, Haji Faki, Njelu Kasaka na wengine wengi hawakuupenda muungano na walikuwa na maneno ya shombo kuliko wewe. Wao wamekufa na muungano unaendelea
 
Utakuwa CCM wewe, unaua mbu kwa rungu, hata akiwa ametua kwenye nyeti za mtu, lazima mbu afe!
 
Utakuwa CCM wewe, unaua mbu kwa rungu, hata akiwa ametua kwenye nyeti za mtu, lazima mbu afe!
Hata China pamoja na ukubwa wote ule bado inadai kuwa Taiwan, Hong-Kong na Tibet ni sehemu za nchi yao.

Wanachofanya ni kuwapa special autonomy tu. Of course autonomy ya Taiwan haiko sawa na Hong-Kong, na ya Hong-Kong nayo haiko sawa na Tibet.

Akina Lissu na Jussa wa Taiwan, Hong-Kong na Tibet wanalalamika kila siku kuwa wanataka uhuru kamili. Na wanaungwa mkono na USA, UK, Germany etc.

Lakini waambie UK waiachie Scotland usikie muziki wao au USA waiachie Hawaii
 
Lakini waambie UK waiachie Scotland usikie muziki wao au USA waiachie Hawaii
Suala sio UK kuachia Scotland, bali Scotland kujitoa UK. Kumbuka kwamba hadi sasa Northern Ireland inafikiria kuendesha referendum kujitoa UK, na si mara ya kwanza hili jambo kuwekwa mezani. Wao sio kama sisi, hawaui mbu kwa kutumia rungu, bila kujali mbu ametua wapi.

Sijasema napenda muungano uvunjwe. In fact maoni yangu binafsi ni kwamba uimarishwe, ikibidi tuwe na serikali moja. Lakini suala la kuwa na muungano kama wa UK huenda ndio suluhisho. Sijui tofauti ya muungano wa Tanzania na wa UK. Labda unajua utufafanulie.
 
Wazanzibari wengi hawaufurahii muungano huu na hawana upendo wa dhati na watu kutoka bara, kilichobaki ni kuheshimu maamuzi ya wale wazee na protokali. Ukweli usemwe!
 
Muungano uboreshwe hapo tunaongea lugha moja. Na ndiyo maana kuna Wizara inayoshughulikia kero za Muungano chini ya Makamu wa Rais. Halafu kuna Tume ya Fedha ya pamoja ndani ya Wizara ya Fedha ya JMT.

Wakati East Africa Community inazidi kupata mvuto kwa nchi kujiunga kutoka zile 3 za asili (Kenya, Tanzania na Uganda) hadi kuwa na nyongeza za Rwanda, DRC, Burundi na South Sudan, huku Tanzania wanaharakati uchwara wanataka kuvuruga muungano uliotulia??

Mpaka Somali na Ethiopia wako kwenye mchakato wa kuingia EAC. Eti sisi tunaona ZNZ ni mzigo kisa hawalipi umeme auHamidu Shaka ni DC wa Ifakara.

Dunia nzima itatucheka. Mfumo wa Serikali 3 waonekana uko vulnerable kuvunja muungano ndiyo maana haushabikiwi sana.

Watu wanaogopa kilichotokea kwa Gorbachev alipobaki hana ardhi anayotawala

Senegal na Gambia walikuwa na Muungano wakaita Senegambia ila walidumu kwa muda mfupi
 
Yes, ukweli wanajaribu kuficha maradhi lakini tuendako sio mbali kifo kitatuumbua wamuulize jaji warioba wananchi wengi wanataka nini juu ya mfumo wa muungano lakini kuna nguvu kubwa inatumika kulinda muundo wa muungano,lakini mengi kwa upande ya tanganyika kudai serekali ya tanganyika yamejitokeza baada kuwa rais mzanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…