Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

HATUTAKI SERIKALI ya Tanganyikana, hatutaki serikali tatu. Tunataka nchi ya Tanganyika,

Serikali tatu zinakupa Marais watatu, mabunge watatu, wabunge mia tisa, Majaji Wakuu Watatu, Makamu wa Rais watatu, Waziri Wakuu watatu.

HAKUNA formulation ya Muungano wa watu milioni 62 na watu milioni moja unusu halafu ikawa fair. Mkubwa atanyonywa na vilio havitaisha.

Huwezi kuunganisha shamba lako na mashamba ya Muhammed Dewji halafu muanze kugawana mavuno na mamlaka ya uendeshaji na amana za mikopo na nafasi za wakulima. Wewe unamwongezea thamani gani ?

Tuuvunje Muungano, for the love of God!
Najua kukiwa na serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar maana yake muungano haupo. Kama serikali tatu haifai basi serikali moja, kama tunaupenda muungano kweli
 
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya mambo ya muungano yanakoenda, yanaweza kusababisha mgongano (confrontation) mkubwa sana kati ya wakazi wa Zanzibar walioko bara na wakazi wa bara walioko Zanzibar.

Badala ya kujibu hoja zinazowekwa mezani, viongozi wameamua kwa makusudi kuwashambulia wale wanaozitoa, bila kuona kuwa kwa kufanya hivyo wanazidi kuchochea uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Kwa kumfurahisha nani?

Kama Tanzania bara wanaona kwamba kwao kero kubwa ya muungano ni kutokuwa na serikali ya Tanganyika, kwa nini hawasikilizwi? Wakati wa Nyerere huenda kulikuwa na sababu za msingi kuwa na serikali mbili, lakini ni wazi hilo halikubaliki kwa sasa, na huwezi kulilazimisha likaendelea kuwapo bila kuleta madhara.

Muungano tunaweza kulazimishwa uendelee kuwapo kwa kutumia nguvu ya dola, lakini haitazuia watu kuanza violence (kupigana) uhasama unaojitokea ukizidi kukua. Amini nawaambieni, huu muungano mnaodai uko imara unaweza kuvunjwa kwa nguvu na kuleta hali ya machafuko bara na visiwani. Watanzania bara walioko visiwani wataondolewa kule kwa nguvu, na wa-Zanzibar walikoko bara wataondolewa huku kwa nguvu, na hata kupoteza mali au uhai wao. Ndilo tunalosubiri? Au tunadhani haliwezi kutokea Tanzania, vitu kama hivyo vinatokea Rwanda tu?

Muungano ulifanyika zaidi ili Zanzibar kusiwe na counter-revolution ya Waarabu (wajomba) walipopinduliwa na kuchinjwa, na kwa Tanganyika kulinda usalama wake katika kuwa kitovu cha kupigania uhuru wa Afrika. Sasa hizi sababu sio hoja tena. Kama imefikia mahali Watanzania hawautaki muungano, basi ni bora uvunjwe kwa utaratibu na kuelewana, watu waulizwe je ungependa kubaki bara au kurudi visiwani, au ungependa kubaki visiwani au kurudi bara nk. Labda tuanze na "Referendum", wananchi ndio tuamue kidemokrasia kama tunataka au hatutaki muungano, sio serikali ituamulie kwa maslahi yake, au maslahi ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, au maslahi ya CCM.

Tusione aibu kukaa chini na kutafakari kuuvunja muungano, kama kuwa na serikali moja au tatu haiwezekani, kwa sababu mfumo wa muungano uliopo sasa hivi unazidi kukuza uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano.
Sidhani kama kuna uhasama....bali watu wanatoa maoni na kupendekeza muungano bora
 
Sheria iliyounda Senagambia, had provisions za kuuvunja. Ule ulikuwa ni mkataba, the same to UK kujitoa EU.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu ni Muungano wa dhima ya Muungano wa milele, zile Articles of the Union, sio mkataba, ni makubaliano ya milele, hakuna provision ya kuuvunja Muungano, tumeunganisha nchi mbili kwa kuchanganya udongo, na kuumwaga bara na Zanzibar, ili kuuvunja, lazima tuutafute ule udogo, tuupembue, punje za udongo wa Tanganyika, zirejeshwe Tanganyika na punje za Zanzibar zirejeshwe Zanzibar.

Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.

Lakini vitu viwili vinapoungana kwa chemical reaction, vitu viwili vile hufa na kuzaliwa kitu kipya kinachoitwa compound, huwezi tena kuvirejesha kwenye hali ya awali kama kuyeyusha sabuni ya unga kwenye maji, kunatokea chemical reaction, huwezi kutenganisha.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu, ume undergo chemical reaction kwa mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar kuungana, kupoteza utaifa wake.na kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo ni compound, halivunjiki tena!.

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
P
Pascal, mie nimesoma chemistry. Sasa ngoja nikupe somo kidogo la chemistry, rahisi tu.

Water is a compound, formed by two hydrogen atoms bonded to an oxygen atom. Now the beauty of it ni kwamba, you can break down water, a compound, into its two primary components, oxygen and hydrogen. All you need is the right amount of energy, and this can be quite substantial. That is why we don't usually generate hydrogen from water, for use as an energy source. It is too expensive compared to other sources of energy.

Sasa, kuna siku there will be the right amount of energy to break this compound called muungano. When that critical energy is attained - if you are a Tanganyikan in Zanzibar, or a Zanzibarian in Tanganyika - you may have to run for your life because that energy will be very, very, very exothermic!
 
Nadhani hujaelewa hili somo, kwa nini tumefikia hpa tulipo na tumefikia hapa tulipo leo na sio huko nyuma. Nataka nikueleze jambo moja very serious, ujue kuna mengi sana nyuma ya pazia. Makubwa ni matatu;
  1. Zanzibar kuna potential kubwa ya mafuta, na yakipatikana Zanzibar itakuwa kama Kuwait; kimapato, ukitumia GDP, the richest country in the world. Tangu ijulikane kuwa Zanzibar ina uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta, suala la nishati (mafuta na gesi) kuwa katika muungamo likawa ni kero ya muungano kwa upande wa Zanzibar, jambo la kuondolewa
  2. Zanzibar ni kisiwa cha kimkakati (strategic island) kiuchumi. Kuna mataifa kama Oman, UAR, Saudi Arabia nk, wako tayari kuingia makubaliano nao ili kiwe katika himaya zao na kuwaahidi Zanzibar mabilioni ya dola, kwamba wakikubali wataishi kama wako peoponi tayari na hakutakuwa na Mzaznibar masikini au asiye na nyumba ya kifahari, matibabu bire kwa wote, na kila mkazi atajengewa nyumba ya kisasa nk. Zanzibar hawawezi kuingia makubaliano kama hayo wakiwa sehemu ya Tanzania, na wakilazimisha basi itabidi JWTZ wachukulie ni uvamizi.
  3. Zanzibar ni kisiwa cha kimkakati (strategic island) kijeshi. Kuna mataifa kama USA, China, Russia nk, wako tayari kuingia makubaliano nao ili kiwe kituo chao cha kijeshi, na kuwaahidi Zanzibar mabilioni ya dola. Tanzania (bara) hawako tayari kuruhusu hili, kwa gharama yeyote ya kulinda muungano, hata kama ni kuwalea huku wanakukojolea kila siku.
Kwa hiyo basi, hizo ndio sababu za msingi zinafanya Zanzibar waone muungano kwa sasa unawazuia kuingia peponi, kulingana na ahadi wanazopewa kama wakiuvunja. Wanafanya kila njia ili kuwakera Tanzania bara kwa visababu vingi vidogovidogo lakini haya ndio mambo yaliyoko nyuma ya pazia.

Hawatasema sababu za kutaka kuvunja muungano, na haya mengine unayosikia ni kelele tu. Na aliethubutu kujaribu hili la kuiondoa Zanzibar katika muungano alikuwa ni Aboud Jumbe, ndio maana akaishia kutengwa kama mtu mwenye ukoma. In fact, ilitakiwa afungwe kwa uhaini. Aliyevujisha taarifa za kile Aboud Jumbe alitaka kufanya alikuwa ni Maalim Seif Sharif, hadi akazawadiwa Uwaziri Kiongozi. Lakini waliambiwa wazi, mtu mwingine yeyote akithubutu, JWTZ itaingia, na wakumbuke hatukitaji kuweka boots on the ground in Zanzibar wakifanya uasi. Tunaweza kuwapiga tukiwa Bagamoyo.

Sasa, theory nyingine ya kutisha iliyopo ni kwamba hata Raisi Samia huenda anatumika kama kichocheo cha kuvunja muungano, akitumia nafasi yake kuwaudhi watu wa bara ili wafikie hatua kusema hawataki tena muungano. Watu wana theorize kwamba anafanya makusudi kuingia mikataba kama ya bandari, kuleta Wa-Zanzibar waajiriwe bara nk, kwa lengo la kuchochea hasira upande wa bara, hasira ambayo mwisho wake ni kuvunja muungano.

Angalia kwamba theory ya Raisi Samia kutumika kama kichocheo cha kuvunja muungano linakuwa na logic fulani kwa jisni alivyong'ang'ania mkataba wa bandari. Ilikuwa ni kama ugomvi wa watu wa bara na Samia, na hakujali kuendelea kuwaudhi watu, hata viongozi wa dini, na wazee wa busara, kwa sababu hilo ndio lilikuwa lengo; wakasirike, waseme sasa muungano basi. Na kuna vitu vingine vingi vinavyohusu kuwafungulia waarabu fursa upande wa bara, pamoja na mambo ya mbuga za wanyama nk. Haya yote yalionekana kuwa ni strategy, kwamba hata kama muungano utavunjika, uwepo wa hawa waarabu upande wa bara, waarabu wanaoonwa kuwa wajomba wa Samia, utakuwa na manufaa kwa Zanzibar. Na hata kuna watu wanasema haya mambo yanafanyika kwa coordination ya Zanzibar na Uarabuni.

Kuna mengi sana nyuma ya pazia. Suala ni kwamba, ni thory tu au yana ukweli ndani yake? Nilitaka kupost hili jambo kama thread inayojitegemea, lakini wewe sasa ndio umefanya niliseme. Haya ni baadhi ya mambo Nyerere alijua, na akawa na msimamo muungano usivunjwe kwa gharama yeyote ile. Hofu yake ilikuwa ni ya kuisalama.
Umeongea mambo mengi ambayo ni nadharia mkuu.
Oman na Dubai hawana cha kuwekeza Zanzibar.
Oman na Dubai n.k n.k umuhimu wa Zanzibar ulikua zamani sio sasa hivi.
Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta more than 10 years back nenda katizame wako na hali gani.
Mafuta hayajawa critical energy resource kama ilivyo zamani.

Kuhusu kuwekeza kijeshi sasa hivi hakuna taifa litalothubutu kuja kuwekeza Zanzibar ilhali kimkakati wa geopolitics DJIBOUTI ndio kunafaa na ERITREA.
Umeeleza nadharia mkuu.
Zanzibar haina umuhimu kama unayoipa.
Oman na Dubai waje kuwekeza nini Zanzibar!?
Embu taja hizo potentials ambazo zitaifanya Oman ije kuwekeza Zanzibar?
Nchi za kiarabu zishahama huko unapopasemea embu kafuatilie vizuri.
 
Umeongea mambo mengi ambayo ni nadharia mkuu.
Oman na Dubai hawana cha kuwekeza Zanzibar.
Oman na Dubai n.k n.k umuhimu wa Zanzibar ulikua zamani sio sasa hivi.
Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta 10 years back nenda katizame wako na hali gani.
Mafuta hayajawa critical energy resource kama ilivyo zamani.

Kuhusu kuwekeza kijeshi sasa hivi hakuna taifa litalothubutu kuja kuwekeza Zanzibar ilhali kimkakati wa geopolitics DJIBOUTI ndio kunafaa na ERITREA.
Umeeleza nadharia mkuu.
Zanzibar haina umuhimu kama unayoipa.
Oman na Dubai waje kuwekeza nini Zanzibar!?
Embu taja hizo potentials ambazo zitaifanya Oman ije kuwekeza Zanzibar?
Nchi za kiarabu zishahama huko unapopasemea embu kafuatilie vizuri.
Ndio maana nimekuambia kuna theory. Ni suala la amini usiamini. Logic.

Kumbuka kwamba hakuna kisiwa kisichokuwa na thamani katika geopolitical strategies. Uingereza walipigana vita na Argentina kwa ajili ya Falk Islands, ambacho ni kisiwa chenye mawe tu. Kuna misuguano kama hiyo kati ya China na Japan kwa visiwa wewe kwa mawazo yako utaona havina thamani. Sembuse iwe Zanzibar, ambako inasemekana kuna potential kubwa ya mafuta ambayo haiendelezwi kwa sababu maalum?

Unafikiri ni nini kimeifanya Singapore kuwa taifa tajiri sana duniani?

Kuhusu "Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta 10 years back nenda katizame wako na hali gani" huko ni kufikiri kubaya. UAE, Dubai, walianza kuchimba mafuta baada ya Nigeria. Angalia kuna hali gani. In fact, huwa wanawacheka Nigeria. Mifano ya mafuta katika Africa haifai kabisa, kwa sababu utawasema pia Angola. Afrika tunajua tatizo letu tunapokuwa na mafuta. Watolee mfano Norway, Kuwait, Malaysia, etc
 
Juzi juzi hapa nilimsikia waziri tena dokta mzima akisema kero za muungano zimetatuliwa kutoka 15 Sasa zimebaki tatu tu😝
Kilichonidhi hakuzitaja kero zilizo tatuliwa na kero zilizobaki. Ni vizuri Sasa tuziweke kero zote hapa ili waziri amalizie home work yake.
Tusisubiri mpaka wanaokerwa na hizi kero wakawa wengi kuliko wasiokerwa.
 
Kama nilivyosema hapo juu, huenda wakiziweka wazi hizo kero wanazosema wamezitatua, Tanzania bara kwao itakuwa ni kero mpya zilizoingizwa kwenye muungano, hivyo sidhani kama watapenda kusema waziwazi ufumbuzi gani umetolewa kwa kero hizo.
 
Ndio maana nimekuambia kuna theory. Ni suala la amini usiamini. Logic.

Kumbuka kwamba hakuna kisiwa kisichokuwa na thamani katika geopolitical strategies. Uingereza walipigana vita na Argentina kwa ajili ya Falk Islands, ambacho ni kisiwa chenye mawe tu. Kuna misugiano kama hiyo kati ya China na Japan. Sembuse iwe Zanzibar, ambako inasemekana kuna potential kubwa ya mafuta ambayo haiendelezwi kwa sababu maalum?

Unafikiri ni nini kimeifanya Singapore kuwa taifa tajiri sana duniani?

Kuhusu "Mafuta hayachimbwi kama unavyochimba viazi,Senegal na Nigeria walianza uchimbaji wa mafuta 10 years back nenda katizame wako na hali gani" huko ni kufikiri kubaya. UAE, Dubai, walianza kuchimba mafuta baada ya Nigeria. Angalia kuna hali gani. In fact, huwa wanawacheka Nigeria. Mifano ya mafuta katika Africa haifai kabisa, kwa sababu utawasema pia Angola. Afrika tunajua tatizo letu tunapokuwa na mafuta. Watolee mfano Norway, Kuwait, Malaysia, etc
Unakosea sana mkuu.
UAE na Oman zimeanza muda sana kuchimba mafuta kabla ya Nigeria na Senegal.
Embu nenda kafuatilie vizuri UAE na Oman zimekua petroleum producing nations na nadhani ni member wa OPEC muda mrefu sana.
Nigeria na Senegal wameanza juzi juzi tu hapa mzee!?

Mapigano ya Argentina na UK yalitokea mwaka gani!?
Nipe jibu halafu tufananishe geopolitical interests zilikuaje kwa mwaka huo na sasa.
-Visiwa ambavyo Japan na China wanagombania as well as visiwa vya south-China sea vinavyosemekana kuwa vya Phillipines kuna utajiri mwingi wa sana wa gesi mkuu nenda kafuatilie.
-Mafuta yaliyokuwepo Zanzibar hayafikii hata robo ya reserve ya mafuta yaliyokuwepo UAE na Oman.
Hakuna kitu Zanzibar kipo Oman ama UAE hakipo.
Pia watu washaanza kuhama na kupunguza umuhimu wa petroleum mzee,hivyo mahitaji yake sio makubwa kama ilivyo nyuma.
- Singapore mzee imeendelea kwa science and technology.Pasi,deki,TV mpaka fridge unazotumia ama ulizokua unatumia brand ya PHILLIPS NI SINGAPORE MADE.Na taifa lililowekeza sana Singapore ni China,hawakuendelea kwa mafuta wale kama unavyodhani.
Pia kuna Macau imeendelea kwa uwekezaji mkubwa wa hanasa na starehe.

Yani unaleta nadharia za zamani sana mkuu.
Zanzibar haina huo umuhimu unayoipa.
Mafuta yapo maeneo mengi pia sasa hivi hayana umuhimu kama zamani.
 
Nahisi siwezi kulumbana na wewe haya mambo. Hatutafikia muafaka kwa sababu tuko level tofauti katika ufahamu. Labda wewe umenizidi sana, au mimi nimekuzidi sana.

Kukuaga, soma hapa chini;

Nigeria
Oil was discovered in Nigeria in 1956 at Oloibiri in the Niger Delta after half a century of exploration. The discovery was made by Shell-BP, at the time the sole concessionaire. Nigeria joined the ranks of oil producers in 1958 when its first oil field came on stream producing 5,100 bpd.

UAE
In the early 1930s the first oil company teams conducted geological surveys in the UAE. Thirty years later, in 1962, the first cargo of crude oil was exported from Abu Dhabi.
 
Pascal, mie nimesoma chemistry. Sasa ngoja nikupe somo kidogo la chemistry, rahisi tu.

Water is a compound, formed by two hydrogen atoms bonded to an oxygen atom. Now the beauty of it ni kwamba, you can break down water, a compound, into its two primary components, oxygen and hydrogen. All you need is the right amount of energy, and this can be quite substantial. That is why we don't easily generate hydrogen from water, for use as an energy source. It is too expensive compared to other sources of energy.

Sasa, kuna siku there will be the right amount of energy to break this compound called muungano. When that critical energy is attained - if you are a Tanganyikan in Zanzibar, or a Zanzibarian in Tanganyika - you may have to run for your life!
Tunaficha vichwa huku mwili wote uko wazi kama mbuni.
 
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya mambo ya muungano yanakoenda, yanaweza kusababisha mgongano (confrontation) mkubwa sana kati ya wakazi wa Zanzibar walioko bara na wakazi wa bara walioko Zanzibar.
Kama hupendi Muungano, hama nchi au kufa tu, there is nothing you can do dogo!! Muungano is here to stay.

Hata Seif Shariff Hamad, Christopher Mtikila, Aboud Jumbe, Haji Faki, Njelu Kasaka na wengine wengi hawakuupenda muungano na walikuwa na maneno ya shombo kuliko wewe. Wao wamekufa na muungano unaendelea
 
Utakuwa CCM wewe, unaua mbu kwa rungu, hata akiwa ametua kwenye nyeti za mtu, lazima mbu afe!
 
Utakuwa CCM wewe, unaua mbu kwa rungu, hata akiwa ametua kwenye nyeti za mtu, lazima mbu afe!
Hata China pamoja na ukubwa wote ule bado inadai kuwa Taiwan, Hong-Kong na Tibet ni sehemu za nchi yao.

Wanachofanya ni kuwapa special autonomy tu. Of course autonomy ya Taiwan haiko sawa na Hong-Kong, na ya Hong-Kong nayo haiko sawa na Tibet.

Akina Lissu na Jussa wa Taiwan, Hong-Kong na Tibet wanalalamika kila siku kuwa wanataka uhuru kamili. Na wanaungwa mkono na USA, UK, Germany etc.

Lakini waambie UK waiachie Scotland usikie muziki wao au USA waiachie Hawaii
 
Lakini waambie UK waiachie Scotland usikie muziki wao au USA waiachie Hawaii
Suala sio UK kuachia Scotland, bali Scotland kujitoa UK. Kumbuka kwamba hadi sasa Northern Ireland inafikiria kuendesha referendum kujitoa UK, na si mara ya kwanza hili jambo kuwekwa mezani. Wao sio kama sisi, hawaui mbu kwa kutumia rungu, bila kujali mbu ametua wapi.

Sijasema napenda muungano uvunjwe. In fact maoni yangu binafsi ni kwamba uimarishwe, ikibidi tuwe na serikali moja. Lakini suala la kuwa na muungano kama wa UK huenda ndio suluhisho. Sijui tofauti ya muungano wa Tanzania na wa UK. Labda unajua utufafanulie.
 
Wazanzibari wengi hawaufurahii muungano huu na hawana upendo wa dhati na watu kutoka bara, kilichobaki ni kuheshimu maamuzi ya wale wazee na protokali. Ukweli usemwe!
 
Muungano uboreshwe hapo tunaongea lugha moja. Na ndiyo maana kuna Wizara inayoshughulikia kero za Muungano chini ya Makamu wa Rais. Halafu kuna Tume ya Fedha ya pamoja ndani ya Wizara ya Fedha ya JMT.

Wakati East Africa Community inazidi kupata mvuto kwa nchi kujiunga kutoka zile 3 za asili (Kenya, Tanzania na Uganda) hadi kuwa na nyongeza za Rwanda, DRC, Burundi na South Sudan, huku Tanzania wanaharakati uchwara wanataka kuvuruga muungano uliotulia??

Mpaka Somali na Ethiopia wako kwenye mchakato wa kuingia EAC. Eti sisi tunaona ZNZ ni mzigo kisa hawalipi umeme auHamidu Shaka ni DC wa Ifakara.

Dunia nzima itatucheka. Mfumo wa Serikali 3 waonekana uko vulnerable kuvunja muungano ndiyo maana haushabikiwi sana.

Watu wanaogopa kilichotokea kwa Gorbachev alipobaki hana ardhi anayotawala

Senegal na Gambia walikuwa na Muungano wakaita Senegambia ila walidumu kwa muda mfupi
Suala sio UK kuachia Scotland, bali Scotland kujitoa UK. Kumbuka kwamba hadi sasa Northern Ireland inafikiria kuendesha referendum kujitoa UK, na si mara ya kwanza hili jambo kuwekwa mezani. Wao sio kama sisi, hawaui mbu kwa kutumia rungu, bila kujali mbu ametua wapi.

Sijasema napenda muungano uvunjwe. In fact maoni yangu binafsi ni kwamba uimarishwe, ikibidi tuwe na serikali moja. Lakini suala la kuwa na muungano kama wa UK huenda ndio suluhisho. Sijui tofauti ya muungano wa Tanzania na wa UK. Labda unajua utufafanulie.
 
Yes, ukweli wanajaribu kuficha maradhi lakini tuendako sio mbali kifo kitatuumbua wamuulize jaji warioba wananchi wengi wanataka nini juu ya mfumo wa muungano lakini kuna nguvu kubwa inatumika kulinda muundo wa muungano,lakini mengi kwa upande ya tanganyika kudai serekali ya tanganyika yamejitokeza baada kuwa rais mzanzibar
 
Back
Top Bottom