Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Muungano uboreshwe hapo tunaongea lugha moja. Na ndiyo maana kuna Wizara inayoshughulikia kero za Muungano chini ya Makamu wa Rais. Halafu kuna Tume ya Fedha ya pamoja ndani ya Wizara ya Fedha ya JMT.
Swali limeulizwa hapa mara kadhaa, kwa nini wanaoona kero za muungano iwe ni Zanzibar peke yake? Kuna uratatibu gani wa kukusanya kero za muungano za Watanzania bara ili nazo zishughulikiwe, au haiwezekani kwa sababu bara hawana serikali?

Na pia, kwa nini utatuzi wa hizo kero 18 zilizoshughulikiwa hauwekwi wazi - je ni hofu ya kwamba hizo kero zimeshughulikiwa kwa namna ambayo watu wa bara wakijua kilichofanyika watachukia na kuona kuna upendeleo zaidi unafanywa kwa Zanzibar, au kwamba kero zimetatuliwa kwa namna ambayo inazidi kudhoofisha muungano? Na watu wanauliza, kwa nini kero za muungano zimeshughulikiwa nyingi na kwa kasi katika kipindi cha Raisi Samia, na huko nyuma marais toka bara walisita kuwakubalia Zanzibar juu ya kuondoa kile wanachoita kero za muungano?

Kwa mfano kero moja ya muungano upande wa bara - ni kitendo cha watu wa bara kutozwa umeme kwa bei ambayo inalenga kufidia hasara wanayopata Tanesco kwa sababu Zanzibar siku zote hawataki kulipia umeme. Lini hili litaisha? Kwa nini nilipishwe umeme kwa bei ya kuwabeba Zanzibar?
 
Mkuu kero nne za Jumbe alipokuwa raisi kwenye barua yake kwenda kwa Mzee wa Butiama hata moja hawajatatua...
Hapo bado hatujakumbushiia kikao cha AAK na mawaziri wake walipofunga safari kwenda Daslam kumuona mzee wa Butiama.....
Bado kero ya komandoo Amour ilipigwa tarehe hadi Leo......kero ni mingi aisee.
 
kama ndi hivyo mambo ya compound. Imekuwaje sasa zanzibar imegoma ku dissolve completely under so called chemical reaction ya huu muungano?
 
kama ndi hivyo mambo ya compound. Imekuwaje sasa zanzibar imegoma ku dissolve completely under so called chemical reaction ya huu muungano?
Kumbe chemistry unaipata mkuu! Pascal hana jibu hapo, maana kwenye compound reaction huwezi hata kujua components zilikuwaje kabla hazija react pamoja na kutoa kitu kimoja kipya na homogeneous!
 
Serikali 3 ni kurudi nyuma na madhara yatakuwa makubwa kwa raia. Bora kwenda mbele kwenye serikali moja.
Madhara ya erikali moja ni baadhi ya wanasiasa kukosa vyeo na madaraka.
Usisahau tulianza na vyama vingi, tukaenda chama kimoja, tukarudi kwenye vyama vingi. Tulianza pia na uchumi huria, tukaingia ujamaa, tumerudi uchumi huria, na sasa tuko uchumi wa serikali ya kifisadi.

Tuko flexible sana, gari letu lina reverse gear.
 
Tuna vyama vingi lakini hatuna katiba ya vyama vingi. Iliyopo ni ya kuhakikisha chama tawala kinabaki madarakani. Hata Bashiru alisema chama kilichopo kwenye madaraka kuondolewa ni uzembe.
 
Kuhusu UAE uko sahihi,mawazo yangu nilidhani mwaka huo 1930 ndio walianza oil extraction,kumbe huo mwaka ulikua wa research.
Ahsante kwa kunisahihisha ila kuhusu Zanzibar tusiipe umuhimu usiostahili.
 
Mnaunga mkono Muungano wa Afrika Mashariki wakati huo huo mnakomaa kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio! 😆
 
Issue kubwa ni kuwa Border ya Tanganyika to the East side of the country isn't clear. Please tuwekee hapa map of Tanganyika
 
Wakati wabunge 55 au G55 walipotoa hoja yakutaka uwepo wa serikali ya Tanganyika Nyerere aliwazuia kwa hoja wale ni wabunge waliotokana na Chama Cha mapinduzi hivyo hoja yao ilitakiwa ianzie ndani ya chama.
Jaji Warioba akizungumzia rasimu ya mabadiliko ya time ya katiba alisema ni heri uwape watanganyika serikali yao kabla hawajaidai.
Siku watanzania,aidi ya milioni 60 watakapoingiabarabarani kudai serikki yao hakuna atakayewazuia.
 
Rais Samia haingii mikataba Kwa lengo la kuwaudhi Watanganyika, Kwa sababu maudhi siyo economic and social benefit.
Bali Rais anafanya hivyo kufaidi tundu la udhaifu wa katiba ya Tanganyika kuhusu ulinzi wa raslimali zake ikiwa Rais atatokea Zanzibar kutawala Tanzania yote.
Sasa hapo bado yu ana haki kuendelea kuingia uwekezaji wa kubinafsisha hata KINAPA, Kwa kuwa bado havunji katiba.

Katiba Mpya haiwahusu wanaoipinga, tuendelee Kwa uelewa uliopo. Uzuri Ni kuwa Watanganyika wa ukanda wa pwani huwa Sisi tunajisikia kama ni Wazanzibari.

Kuhusu uchumi, Ni mwendo fikra za Yericko Nyerere tu!
 

Makubaliano ya milele kama yale ya DP na Bandari yetu, Kwahiyo unataka kutwambia na DP nao watakaa milele?
 
Mnaunga mkono Muungano wa Afrika Mashariki wakati huo huo mnakomaa kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio! 😆
Mbona jibu rahisi sana. Ni kwa sababu nchi za Afrika Mashariki ni wastaarabu kuliko wa-Zanzibar! Ulishasikia nchi ya Afrika mashariki inamtia mtu nguvuni kwa kosa la kula wakati wa mfungo wa Ramadhani?
 
Duh!
Leo nimekuwa jasiri wa kukusoma hadi kwenye hiyo aya niliyonyanyua na kuibandika hapa.
mimi ni mpenzi wa kusoma na kuandika, hivyo nasoma kila chenye interest yangu na nasoma hadi mwisho, asante kwa ujasiri wa kunisoma。
Umeeleza vyema huko juu, lakini ukaja kujichanganya kwenye hizi kemikali, ambazo ni dhahiri huna ujuzi nazo.
ni kweli sina ujuzi na kemia kivile,O-level nimepiga A ya siasa na B ya history halafu mathe,physics,chemistry,biology, geography kiswahili nimepiga makarai, nika opt for HGL, ila combi zote zilikubali!.
Asante
Ni kweli
hata huu muungano imebaki swala la muda tu. kama hakutatokea kiongozi mwenye ushawishi wa kutosha kuujenga upya na kuwashirikisha wananchi wake katika kazi hiyo, hatuna muda mwingi sana nao huu muungano.
Duh!, hakuna any provisions popote za kuuvunja muungano, huko kuuvunja kutaanzia wapi?.
Hata mimi sina jibu
Wakati mwingine manufaa ya muungano yasiyoonekana sasa, huko baadae ukishaleta neema watu wanasahau magumu waliyoyapitia. Confederate leo ukiwaambia wajitenge sidhani kuwa utawapata wengi.
Hii inaitwa positivism, positive attitude, this is affirmative, huu ndio uzalendo wa kweli
Leo nimekusoma mkuu P, na nimeona mantiki ndani ya andiko lako refu kiasi.
Asante, huu ni mwanzo mzuri, ukipata nafasi, nisome Mwananchi kila Jumatano, na Nipashe kila Jumapili, na Jumapili usiku, angalia KMT on Channel Ten. J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake
P
 
Duh!, hakuna any provisions popote za kuuvunja muungano, huko kuuvunja kutaanzia wapi?.
Soviet Union, ilikuwa na 'provisions' za kuvunja muungano wao?
Ngoja nikurudishe tena kwenye ile mifano yako ya kemikali. Usisahau 'new knowledge' inatengenezwa kila siku, ndiyo sababu akina Hydrogen ambao zamani zzziiiile alionekana hawezi kuwa mbali na mshirika wake Oksijeni katika tone la maji; sasa hivi ni tone hilo linalotumika kuzalisha Hydrogen, ambayo sasa inatumika kama 'Green Hydrogen' kuzalisha nishati.
Kwa hiyo hizo 'provisions' unazodhani wewe kwamba zimefunga kila kitu, fikiri tena.
 
Asante, huu ni mwanzo mzuri,
Hapana.
Labda nikusome kwenye maswala kama haya ya Muungano. Inapokuja kwenye vyama vya siasa, UCCM wako huondoa hamu ya kutaka nikusome.
Na naomba unielewe, sijajitangaza hapa mimi kuwa ndani ya CHADEMA, au chama kingine chochote cha kisiasa.
Chama changu pekee, nisichoweza kukivua, ni maslahi ya hii nchi inayoitwa Tanzania. Wakiuvunja huo muungano, basi nitaifia Tanganyika yetu.
 
Bongo nguvu ya umma ina safari ya karne kadhaa sio leo!! Muungano hauvunjiki kwa kizazi hiki cha kunguru, ni bora ungetumia muda vizuri kuwaza urithi wa wanao siasa za bongo hakuna azijuae zaidi ya Nyerere peke yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…